Nini kimetokea kwenye muziki Bongo Fleva?

njundelekajo

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
310
227
NI, NINI KIMETOKEA KWENYE MUZIKI WA BONGO FLEVA?

NA NOEL NGUZO.

Mpaka sasa mjadala mkali unaendelea kuhusu nani hasa aliyeupa jina la "bongo fleva"muziki wa kizazi kipya.Wengine wanamtaja mtangazaji mkongwe wa radio, Mike Mhagama kama mhasisi wa jina hili miaka ya tisini alipolitaja kwa mara ya kwanza baada ya kuucheza wimbo wa kundi maarufu la Unique Sisters akiwa studio kwenye kwenye radio aliyokua anatangaza wakati huo.

Lakini pia,lipo kundi lingine wanamtaja Mkongwe mwingine, Taji Liundi(Master T) kama mwanzilishi wa jina hili la muziki huu ulioanzia miaka ya 1990,huku baadhi wakiwataja kina Joseph Kusaga Boniface Kilosa( Dj Boni Love).Mpaka sasa umekosekana ushahidi nani aliyetamka kwa mara ya kwanza neno "bongo fleva"kuwakilisha muziki huu.

Lililo wazi ni katika historia ya muziki huu huwezi kuyakwepa majina ya wasanii kadhaa kama Adili au Nigga One,Salehe Jabri aliyetumia mdundo wa wimbo wa "Vanila Ice,Ice,"Ice Ice Baby",kisha kughani kwa lugha ya Kiswahili,Otham Njaidi,Eliud Pemba,Columba Mwingira,Sindila Assey,Joseph Mbilinyi(2 proud wakati huo),Sygon,Pamela kama baadhi ya waasisi na waanzilishi wa muziki huo.

Muziki huu ulioshika hatamu miaka ya 2000 ukichagizwa na album bora ya wakati wote ya kundi la H.Blasters likiundwa na wasanii Nigga J(sasa hivi Prof J),Fanani na Big Willy inayoaminika kuleta mapinduzi makubwa ya kimtazamo kwa jamii kutokana na vibao vyake vikali ikiwemo Ma Msapu,Niamini,Bongo Dar-es-Salaam iliyobeba jina la album,hauonekani tena kujifinyanga na jamii ya kitanzania kama kipindi cha nyuma.

Wakati ule wa uhai wa bongo fleva katika jamii ya watanzania hakukua na fungiafungia ya nyimbo za wasanii wa muziki huu.Ilizoeleka kusikia Baraza hilo la sanaa nchini likipambana na wasanii wa filamu.Unawezaje kufungia wimbo kama "wauguzi" wa Wagosi wa kaya?au "mama mubaya"wa Mataluma na pengine "Malumbano" wa Twenty percent a.k.a Twenty Paaa a.k.a Amilalile?

Bundi wa mashairi ya nyimbo za bongofleva kujitenga na masuala kuntu ya jamii alitua rasmi juu la paa la muziki huu baada ya kuingia kwa "watu wa kati"maarufu kama mameneja.Hawa wameivuruga kama sio kuiondoa kabisa taswira kubw iliyobebwa muziki huo miaka ya nyuma kati ya muziki huo na jamii ya watanzania kutokana na kuufanya muziki huo kua na malengo ya kibiashara zadi kuliko maadili na ujumbe wenye kuikanya jamii ama kuipa tahadhari katika mambo mbali mbali yakiwemo magonjwa kama ukimwi,matumizi ya madawa ya kulevya nk.

Hebu fumba macho yako rudisha nyuma masikio yako zikumbuke nyimbo hizi:- Mshkaji mmoja(Jose line),Kama ntapata Ukimwi(Afande Sele),Majobless(BIG DOG POZ),Ana miaka chini ya 18(2 proud), Maisha ya Boarding(Jay Moe),Machoni kama watu(Lady Jay Dee ft A.Y),Mke wa mtu ni sumu(LWP),Tutakukumbuka (Crazy Gk ft T.ID,)Alikufa kwa ngoma (Mwana Fa),Kazi yake Mola(Madee),Kamanda(Daz Nundaz),Kosa la Marehemu(Uswahilini Matola),Mwanangu huna nidhamu(Dudu Baya),Ntoke vipi(Bwana misosi),Nipende kama nilivyo(Chelea man)

Fumbua macho vuta pumzi kwa nguvu ndani,washa redio yako sikiliza nyimbo hizi Nampa Papa(Gigi Money),Hakunaga Ushemeji (Manifongo),Kibamia(Rostam),Nyegezi (Diamond ft Rayvan),Ntakupwelepweta(Ya Moto Band),Kijuso(Queen Darlin).

Umegundua nini? jibu ulilolipata ndio sababu iliyofanya tusisikie wimbo wa msanii wa bongo fleva wa kizazi cha sasa hata mmoja ukipigwa wakati rais alipotangaza siku nne za maombelezo kutokana na kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere ziwa Victoria tarehe Septemba 20 mwaka jana.

Nyimbo zote zilikuwa zinapigwa redion katika siku nne za maombolezo ni za wasanii wa bingofleva kundi la kwanza .Wasanii wa kipindi wapo mbali na jamii yao.Wamejitengenezea dunia yao peke yao ambayo haina kifo ndo mana hawatungi nyimbo kuhusu vifo, haina njaa wala ukimwi ndo mana hawaoni umuhimu wa kutunga wimbo kama usinitenge ya Profesa Jay,kwa nini waimbe madawa ya kulevya mabaya kwenye dunia yao ya vibamia?Ukikuta wimbo wenye muktadha wa kijamii au taifa basi ni"project"maalum

Wapo Bali sana na jamii, wamemezeshwa maneno na mameneja wao kwamba nyimbo za mapenzi peke yake ndizo zinazolipa na kutamba,huu hutumwa wa pesa kwa nini mnaifanya kuisaliti familia zenu zinazotaka muwakumbushe wenzenu juu ya ukimwi?Kama kila Niagara yoyote inayolipa ni sahihi kuifanya kwa nini biashara ya madawa ya kulevya inakatazwa?Kuna tofauti gani kati ya mfanyabiashara wa madawa ya kulevya na msanii anayepanda mambo ya hovyo katika vichwa vya jamii yake?

Uasi mkubwa uliofanywa na mameneja katika mziki huu ni kuubadlisha mfumo wake kutoka kwenye kuuza albamu na kua muziki unaotegemea biashara ya matamasha.Na hili halikufanyika bahati mbaya,mauzo ya albam yalikua hayana faida kwa meneja zaidi ya msanii mwenyewe na msambazaji.Badiliko hili likaondoa focus ya wasanii kutunga nyimbo wakiiwaza jamii yao na badala yake wanatunga nyimbo za kuwafurahisha watakaokuja ukumbini,wanyanyue mikono juu,watingishe kama imekwisha na mambo mengine ya pale kati patamu tamu.

Ukumbini haiwezekani ukaeleweka kama utawaimbia watu"Nikianguka" wa Afande Sele,nani atake umuimbie Swahiba wa marehemu Jebi badala ya Kababa ye na wowowo?. Ndio maana kina Nash Mc,Songa na wengine kama kina Nick Mbishi hawawezi kua na mameneja kwa utaratibu wao wa kuendelea kufanya biashara ya muziki kwa kuuza albam.

Meneja gani hakuruhusu utunge wimbo kama barua wa Das Nundaz wakati kuna wimbo wa "katika",uandike mashairi yenye verse nne kama wimbo wa simu yangu wa Solo Thang mbele ya Konk yenye verse moja na nusu wa Dudu Baya? .Ni kweli mambo yanabadilika sawa lakini ni bora kusiwe na mabadiliko kama mabadiliko hayo hayana tija kwa jamii.Tunatambua kamuziki huu umetoa ajira kubwa sana kwa vijana wengi pasipo kutengeneza heshma ajira hizo hazitakua na maana yoyote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom