Nini kimemkuta Ommy Dimpoz?

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,879
7,382
Mimi ni mshabiki wa Ommy Dimpoz kitambo kidogo tangu anatoa nainai lakini siku hizi ananiangusha sana tangu wanjera na hii mpya ya sasa achia body ambayo kimsingi nyimbo imekosa ubunifu, nyimbo imefanana na shikorobo ya Shetta hasa beat, melody nyepesi mno haivutii.

Ommy rudi kwenye identity yako utakuwa zaidi hata uko kimataifa unakota kwenda, umemtoa Vanessa mdee na amepiga hatua kuliko wewe, wake up Dimpoz.
 
Nyimbo ya ndagushima ilikuwa kali sana ila hizi nyingine nahisi anahitaji zaidi ya mubenga
 
Nyimbo ya ndagushima ilikuwa kali sana ila hizi nyingine nahisi anahitaji zaidi ya mubenga

Upo sahihi mkuu sijui tatizo ni utunzi au meneja nae hajui muziki hivi kweli cabinet inakaa na kupitisha nyimbo kama hii achia body? hii nyimbo itasahulika mapema sana
 
Sometimes kujishusha ukakubali kujifunza inasaidia sana. Alipokua karibu na Diamond, akatoa kichupa Ndagushima kilikua poa atleast....
Baada ya hapo ni Wanjera eeeeeeh baaas
 
Afu kingine kikubwa ni kujifanya amekuwa mkubwa sawa na Diamond...

Maana kipindi ni marafiki wakubwa Diamond alikuwa anambeba saana akisafiri kwenda kushoot video wapo nae, mambo mengi sana alikuwa anajifunza kwa Diamond...

Sasa baada ya kuona amekua na kuanza kuvimbiana na Chibu ikawa tatizo, licha ya kupunguza upendo kwa baadhi ya mashabiki, amekosa pia maujanja ya kulishika game vizuri, anaishia anavyofanya hivisasa.. Wanaishia kusikia tu Diamond ananyimbo kaaaali 5 zenye video tayari, 3 zake 2 za kushirikishwa, haya maujanja anayakosa ommy maana watu anaoambatana nao hawampi hizo challenge, anaishia kusema ana album kadhaa kumbe ni nyimbo mbovu..
 
Ommy alikuwa kila akitoa wimbo ni hit, ila kaanza kuharibu trend yake pale kwa Wanjera, but mi bado naamini Ommy ni talent ajipange tu
 
Afu kingine kikubwa ni kujifanya amekuwa mkubwa sawa na Diamond...

Maana kipindi ni marafiki wakubwa Diamond alikuwa anambeba saana akisafiri kwenda kushoot video wapo nae, mambo mengi sana alikuwa anajifunza kwa Diamond...

Sasa baada ya kuona amekua na kuanza kuvimbiana na Chibu ikawa tatizo, licha ya kupunguza upendo kwa baadhi ya mashabiki, amekosa pia maujanja ya kulishika game vizuri, anaishia anavyofanya hivisasa.. Wanaishia kusikia tu Diamond ananyimbo kaaaali 5 zenye video tayari, 3 zake 2 za kushirikishwa, haya maujanja anayakosa ommy maana watu anaoambatana nao hawampi hizo challenge, anaishia kusema ana album kadhaa kumbe ni nyimbo mbovu..

Sasa unaacha kukaa na Diamond ujifunze unaenda kukaa na Idris Sultan na Wema Sepetu unategemea nini?? Mambo mengine huwa ni ya kujitakia tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom