Nini kifanyike walimu wapate heshima kama watumishi wengine?

Lenatuschacha

Senior Member
Jul 29, 2015
156
36
Kuna ujumbe unasambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba rais atoa tamko walimu waongezewa mshahara na marupurupu, badae mwishoni unasema sio Tz nchi flani, walimu mtasubiri sana.

Sasa mimi naona kama ni zarau kubwa sana wanafanyiwa walimu kwa kufanywa kama ndo wenye njaa sana humu Tz. Je nini kifanyike ili waalimu wapate heshima katika jamii.
 
Hakuna wa kuwasaidia kupata heshima zaidi yenu wenyewe! Hamjui cha kufanya mpaka mje mtulilie humu?! Kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe!
 
Kinachouwa walimu ni CWT kimeshindwa kuweka mikakati ya dhati kupambana na maslahi ya walimu kwa mfano Kenya chama cha walimu kina sauti sana
 
Kinachouwa walimu ni CWT kimeshindwa kuweka mikakati ya dhati kupambana na maslahi ya walimu kwa mfano Kenya chama cha walimu kina sauti sana
Watanganyika wanaamini kila kitu cha Kenya ni bora. Ulisikia walimu Kenya waligoma na kupewa order na mahakama warudi kazini bila madai yao kusikilizwa, sijui nguvu ya chama chao uliwasaida nini. Bado maslahi ya walimu Kenya sio mazuri kulinganisha na kada Zingine

Duniani kote walimu wanachukuliwa poa kulinganisha na mchango wao kwenye jamii, si Tz au Africa tu hata nchi za Ulaya na Marekani hali ni hiyo hiyo

Kwa Tz hali ni mbaya zaidi sababu kwanza ualimu imekua kimbilio la waliokosa nafasi sehemu zingine na pili walimu wenyewe wengi wao ni kama weridhika au wamekata tamaa ya kuomba haki zao na kukosa sauti ya pamoja. Serikali imesahau kabisa hii jamii
 
Kuna ujumbe unasambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba rais atoa tamko walimu waongezewa mshahara na marupurupu, badae mwishoni unasema sio Tz nchi flani, walimu mtasubiri sana.

Sasa mimi naona kama ni zarau kubwa sana wanafanyiwa walimu kwa kufanywa kama ndo wenye njaa sana humu Tz. Je nini kifanyike ili waalimu wapate heshima katika jamii.
1.Mbadilike MJISOMEE na mpate maarifa makubwa ya kweli kuitwa WAALIMU.
2.Msimwelezee kila mtu matatizo yenu hata mtu ambae hana uwezo wa kuwasaidia.Mfano:Sasa kila mtu hata mtoto mdogo anajua mna shida na ndio maana ANAWADHARAU.
3.Msiwe wanyonge mishahara yenu siyo midogo kiasi hicho,ila wengi mnalalamika kwa vile hamjui mishahara ya wengine,wanaopenda kukaa na kutatua matatizo yao kiutaratibu.
4.Mfano:Daktari(MD) anayeanza mshahara wake HAUFIKI 1M baada ya kusoma miaka 6 wakati Mwl. anapata 600,OOO BAADA YA KUSOMA miaka 3 Tu.
KAZI NJEMA.
 
Kinachouwa walimu ni CWT kimeshindwa kuweka mikakati ya dhati kupambana na maslahi ya walimu kwa mfano Kenya chama cha walimu kina sauti sana
SIYO CWT NI WALIMU WENYEWE MAANA VIONGOZI WA CWT WANACHAGULIWA NA WALIMU WENYEWE KWA KURA KWA MUJIBU WA KATIBA YA CWT.
CWT NI CHAMA CHA WALIMU NA KINAENDESHWA KWA FEDHA ZA WALIMU.KAMA HAKIWATENDEI HAKI NENDENI MAHAKAMANI
 
1.Mbadilike MJISOMEE na mpate maarifa makubwa ya kweli kuitwa WAALIMU.
2.Msimwelezee kila mtu matatizo yenu hata mtu ambae hana uwezo wa kuwasaidia.Mfano:Sasa kila mtu hata mtoto mdogo anajua mna shida na ndio maana ANAWADHARAU.
3.Msiwe wanyonge mishahara yenu siyo midogo kiasi hicho,ila wengi mnalalamika kwa vile hamjui mishahara ya wengine,wanaopenda kukaa na kutatua matatizo yao kiutaratibu.
4.Mfano:Daktari(MD) anayeanza mshahara wake HAUFIKI 1M baada ya kusoma miaka 6 wakati Mwl. anapata 600,OOO BAADA YA KUSOMA miaka 3 Tu.
KAZI NJEMA.
Sawa mkuuu lakini sio kwamba waalimu wana mishahara midogo kiasi hicho ila jamii inachukulia kwamba uwaalimu ndo kazi mbaya kuliko zote hilo ndo tatizo
 
Kuna watu wana fikra kwamba walimu ni kundi lilokuwa na malengo mengine likashindwa kufikia huko,likaangukia kwenye ualimu,hawajui kuwa UALIMU ni TAALUMA inayosomewa chuoni.Si kila mtu anaweza kuwa MWALIMU.
 
Mshara tu waweza walau kununua Vigari vidogo mana katika watumishi wanaongoza kwa kusugua ndala ni walimu Hii kazi inabeba sana future ya taifa ila ndio hivo uongozi umeifumbia macho kwa vile matokeo yake si hapo kwa hapo ila baada sasa tunajenga taifa ovyo kwa kutodhamini walimu
 
Sawa mkuuu lakini sio kwamba waalimu wana mishahara midogo kiasi hicho ila jamii inachukulia kwamba uwaalimu ndo kazi mbaya kuliko zote hilo ndo tatizo
Ni kwasababu walimu wenyewe ndio wanawaambia watu hivyo.Huwezi kutangazia watu shida zako ambao hata hawawezi kukutatulia ,halafu wasikudharau.Ndio binadamu TULIVYO.
 
Walimu inabidi wapatiwe elimu ya ujasilia mali ili waepuke kuwa salary dependant. Hata ukilipwa 1M na hauna chanzo kingine cha mapato hali itakuwa ngumu tu.Tatizo lao wengi wakianza kazi tu Bayport wanawawahi kwa mikopo then vijana wana hangaika na madeni yao mwisho anaanza kuona salary haitoshi. Kwa sisi watanzania ukipata ajira tu wategemezi wanakuwa wengi sana mpaka mshahara wako unauona mdogo ila kama ukiutumia kwa matumizi yako wewe kam wewe unakutosha kabisa.
 
Ni kwasababu walimu wenyewe ndio wanawaambia watu hivyo.Huwezi kutangazia watu shida zako ambao hata hawawezi kukutatulia ,halafu wasikudharau.Ndio binadamu TULIVYO.
Hiyo mkuu ni sychologia imejengeka kutoka kwa jamii kwa mfano wengi wanaami kwamba mshahara wa mwl ni laki mbili tu
 
Waongezwe mshahara, bhaaas!
Inashangaza hawa watu walitakiwa waheshimiwe sana maana mchango wao ni mkubwa! Kila mtu mwenye busara lazima apitie kwao kupata maarifa.
 
Hiyo mkuu ni sychologia imejengeka kutoka kwa jamii kwa mfano wengi wanaami kwamba mshahara wa mwl ni laki mbili tu
Sasa walimu ndio wanapaswa kuibadilisha jamii na wana uwezo huo.Tatizo lao wanapenda mno KUJILIZALIZA Kama manesi.Walimu ndio wamelikomboa TAIFA Hili na sasa tuna RAIS Mwl. na Waziri Mkuu Mwl. "Hii inferiority Complex" walimu wanapaswa kuliepuka hili Zimwi.
 
Waongezwe mshahara, bhaaas!
Inashangaza hawa watu walitakiwa waheshimiwe sana maana mchango wao ni mkubwa! Kila mtu mwenye busara lazima apitie kwao kupata maarifa.
Unafikiri mshahara unaotosha ni kiasi Gani??
 
Unafikiri mshahara unaotosha ni kiasi Gani??
Sifahamu mshahara wa walimu ila kwa shule ya msingi labda walipwe laki 8 kama kiwango cha chini kabisa na stahiki zao zingine wazipate bila kubaniwa baniwa, pia mashuleni nako kuboreshwe miundo mbinu na taratibu nzima ya ufundishaji, mwalimu mwenyewe atakapojisikia anathaminika, malalamiko yake yatapungua.
Wengi wanaosema mitaani kuhusu walimu kuwa na maisha duni ni REFRECTION ya wao walimu wenyewe kutokana na kulalamika kila kukicha.
 
Back
Top Bottom