Nini kifanyike kwa ahadi hewa za viongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kifanyike kwa ahadi hewa za viongozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maneno Anania, Jan 21, 2012.

 1. M

  Maneno Anania Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inapotokea kiongozi tunampa kura kwa ahadi lukuki na hazitekelezi kwa kipindi cha miaka mitano, yeye hana hasara ila sisi wananchi. Anakuja mwingine na ahadi lukuki kutoka chama hicho hicho na ahadi lukuki naye hazitelelezi kwa miaka yote mitano na hapo pia ni sisi wananchi tunaumia na hapa nahitimisha kuwa tatizo linakuwa ni la chama kinachotuletea viongozi wabovu. Ni hatua gani sisi wananchi tuchukue fikiria na hiyo miaka mitano ya mateso!
   
 2. T

  TUMY JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo si chama tatizo ni nyie mliopiga kura kwani chama ndio kinapiga kura, hakuna chama kinachokushikia bunduki kumchagua mtu msiyemtaka, mkichagua kiongozi mbovu ni juu yenu na mateso ni juu yenu mpaka siku mtakapo badilika na kumchagua mtu kwa kuangalia utendaji wake sio kuangalia chama chake anachotoka.
   
 3. M

  Maneno Anania Member

  #3
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini inawezekana pia tukamchagua tunaye amini kwa wakati ule ndiye anayetufaa. Akianza kusuasua kwenye ahadi zake na kumsubiria mpaka miaka mitano iishe ndiyo tumwajibishe kwa kumnyima kura ni muda mrefu. Ni utaratibu gani wa kumfanya awajibike kabla ya kuondoka badala ya kusubiri mpaka miaka mitano ipite?
   
Loading...