Nini kifanyike kuwainua Developers wa Tanzania?

Pendo Julliet

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2017
Posts
243
Reaction score
324
Nimeona hili la developers wa kitanzania kutokuwa na ushirikiano mzuri kati yao na hivyo kurudisha nyuma mafanikio na mchango wao katika ukuaji wa TEHAMA kwa maendeleo ya taifa letu Tanzania.

Nilifanikiwa kugundua tatizo la developers wengi Tanzania ni wabinafsi sana.

Developers na maprogrammer hawa hawataki hata kushirikiana ili kutatua changamoto zinazowakabili kwa kazi zao amabazo ndiyo zinawaingizia kipato.
Wapo wale wanaoingia kwenye fani hawa ni upcoming programmers nao wanakosa msaada kutoka kwa wakongwe wa fani!

Yani wakongwe wao wanachojali ni pesa tamaa imewajaa na wanapenda sana pesa ya mkato.
Ubinafsi na tamaa ya pesa ya haraka vitawaua! Shauri yenu..

Nia yangu hapa siyo kumtafuta mchawi nani nimekuja kueka mambo sawa.
Nakuomba tulia, soma kwa umakini, tafakari changia sababu mawazo yako yanahitajika sasa.

Nini kifanyike ili tuondokane na matatizo haya makubwa ya ubinafsi kwa devs wa kibongo?
Ili kushirikiana kwa pamoja na kueza kuifanya Tanzania kuwa great hub of IT Afrika.
 
Waache ubinafsi, washirikiane watafanikiwa
 
kwanza kabisa kama hawana chama wangeanzisha hata umoja wao kama ilivyo kwa watu wakada mbalimbali mfn walimu(cwt)wafanyakazi(Tucta),wamiliki wa mabus,wasanii n.k halafu kutokea hapo wangejadili mambo mengi zaidi yenye kuleta mshikamano na umoja
maana kuna watu waposingle na wanakomaa na maproject makubwa peke yao kitu ambacho kinaweza kupunguza ubora
 
Ubinafsi na ugomvi haufai...Tunajenga nyumba moja ya nini kugombana??? Maendeleo ya Sayansi na teknolojia yapo juu yao halafu wao kwa wao wanazozana....waache hizo la sivyo jitihada zao zitaonekana bure
 
Ukitaka kwenda mbali nenda peke yako ila kama unataka uende mbali zaidi nenda na wenzako ndio maana tz teknolojia inachelewa kutokana na madeveloper kwenda peke yako ila kama wanataka tufike mbali kam India na Afrika ya Kusini waondoke na chikupizi na mshikamano.kwenu wajuvi
 
Si kweli. Tatizo sio ubinafsi tatizo fani haina hela, nchi zinazofanya vizuri kwenye Tech zina Venture Capital, hawa ni wawekezaji wa awali kwenye kampuni ambao wako tayari kurisk hela zao kwenye makampuni chipukizi (Startups) wakiwa na matumaini ya moja ya hizo kampuni kuwa big.

Mfano waliwekeza $62 million kwenye WhatsApp mpaka ikaja kununuliwa na Facebook kwa $20 billion.

Mpaka sasa hivi wamewekeza $15 Billion! kwenye Uber kampuni ambayo haijawahi kupata faida, wakitegemea itafanya maajabu huko mbele.

Kuwa na Tech sector ya kweli unahitaji hela, matatizo mengine yote yanatatulika.
 
Ukiwa na idea nzuri na ya kipekee hauwezi kukosa mwekezaji, shida ni kwamba watu wanakujanna vicopy & paste halafu wanataka uwekenhela yako huko.
 
Ukiwa na idea nzuri na ya kipekee hauwezi kukosa mwekezaji, shida ni kwamba watu wanakujanna vicopy & paste halafu wanataka uwekenhela yako huko.
Idea za kipekee ni myth kwenye tech, tatizo ni execution sio idea ya kipekee. Wako wapi hao investors Tanzania?
Kuna mwekezaji bongo anaweza kukupa $5 million (Billioni zaidi ya kumi za kitanzania) ukimwambia kampuni itapata hasara kwa miaka 5 ya kwanza na hauna asset ya kufidia chochote?
 

India wanajitahidi siyo siri. Ukitafuta tutorials youtube au sites zingine huwezi kukosa wahindi. Jinsi ya kuhack na mautundu mengine wahind wapo vizuri.
Huwa hawafichi kila kitu wanaweka wazi.
TZ ubinafsi ndiyo unawasumbua. Mtu anataka kufanya project yy ili hajulikane. Mpaka sasa hakuna lolote zaidi ya kuiga mambo.
Ukitafuta program ya kuunlock modem za huawei utapata za wazungu na wahindi tu.
Kuna mmoja niliona ya CALVIN Power lkn upande wa flash code alichemka. Na yenyewe ameshafuta link
ndiyo maana mm km nakitu nakitafuta na search in English.
Hebu jiulize sites za pirates km kickass, piratebay, piratecity n.k wana mioyo gani kutoa free software? Ww na bando lako tu. Unadownload utakacho.
Bongo wakitoa program basi ni vya simu tena vya kuiga kwa wenzao.
Mfano. Instagram na yy anatoa hiyo hiyo
 
Ni kweli hela inahusika lkn ukitengeneza app nzuri itajiuza yenyewe wala hautangaika.
Ukitengeza program km ya kutrack simu iliyoibiwa, kuunlock simu zote, modem n.k hata nje ya nchi watanunua.
Mbona Kaspersky na bitdefender watu wananunua? Ubora wa kitu na umuhimu wake ndiyo utafanya watu wakinunue.
Angalia Easeus data recovery
 
Reactions: P.J
Tatizo sio ubinafsi tatizo fani haina hela

Fani hii ina hela ndugu.

nchi zinazofanya vizuri kwenye Tech zina Venture Capital, hawa ni wawekezaji wa awali kwenye kampuni ambao wako tayari kurisk hela zao kwenye makampuni chipukizi (Startups) wakiwa na matumaini ya moja ya hizo kampuni kuwa big.

Kwenye hizo nchi natumaini wawekezaji hao wanakubali kutoa hela kwa makampuni yanayochipukia baada ya kucalculate risks na kuona future ya project husika ni very promising.
Project ikiwa ni nzuri popote pale ukiinadi kuwa unatafuta hela wawekezaji wanakuja wenyewe hapa ni wazi kuwa tatizo siyo hela kama ulivyoeleza.
Tulifahamu tatizo vizuri ndiyo tutaeza kutafutia ufumbuzi.

Kuwa na Tech sector ya kweli unahitaji hela, matatizo mengine yote yanatatulika.
Matatizo hayo mengine ndiyo kikwazo na yakitatuliwa ndiyo sector hii itakuwa kwa mafankio sana.
 
Ni kweli, project nzuri zinajiuza hivyo kujifund zenyewe.
Shida ni pale kila mtu anataka kuonekana yeye master ni ubinafsi tu.

Niliskia hata wakuu fulani walitaka kutuletea IT guys kutoka Rwanda!
 
Asante kwa mawazo mazuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…