tinno criss
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 112
- 56
Harakati Zipi Zifanyike Ili Kuokoa Kuzama Kwa Jahazi Bongo Movie??
Vizuri Sana, pa oneWaachane na siasa wafanye movie
Vipi wamekutuma uje uwasemelee??Harakati Zipi Zifanyike Ili Kuokoa Kuzama Kwa Jahazi Bongo Movie??
Mdau umeongea yote...Utengenezaji wa filamu ni changamoto kubwa, hakuna professional producers. Mtu ana andika story, anakuwa producer, director na main actor kwenye movie moja! Ujinga huu unakuta mtu mmoja anamiliki muvi peke yake bila resources, bila ujuzi.
Swala la cameras na lights ni shida tupu, muvi zina vivuli, background mbovu, resolution mbovi, wana shoot kwa camera moja au mbili. Hakuna 3D camera, au drone za kushoot. Waangalie video za bongo fleva za sasa hivi na zile video za kipindi cha mwananchi video.
Sounds kwenye muvi ni shida, movies zina mwangwi na unnecessary sounds, wanaongea kwa kupayuka. Sound range haizingatiwi.
Kuvaa uhusika, actors wengi ni wababaishaji, hakuna vipaji kuna wauza sura. Mtu anaigiza yuko kijijini ila nywele zinawaka wave na usoni scrub ya maana! Wana over-actor. WANAIGIZA KUIGIZA! Movies hazina uhalisia hata 50% percent!
Kingine wanatengeneza filamu zao, means hawaangalii soko linataka nini. Wanafanya kwa kuangalia wao wanaeza kufanya vipi. Muvi mtu ana amka, anaoga, anavaa, anakunywa chai, anawazaa... Ansingia garini.. Anatoka nyumbani hadi kazini ni scene hiyo moja tu! Ujinga huu ndio unakuta movie ya dk. 15 inakuwa na part 1 na 2! Kisa script za kipuuzi. Scene ndefuu na hazina maana.
Mwisho most of them wana maadili mabovu sana. Watu wa costumes kwenye hii tasnia wanawavalisha nguo za ajabu! Utupu utupu sana kuonesha mapaja na vitovu.. Ndio maana wengi huko wanaringia "chura" zao! Scenes za vitandani sasa.. Zinachukua almost 60% ya muvi nzima! Watu wanadaradarana, kunyonyana.. Mara kitandani.. Kidume juu ya jike shuka tu wamejifunika kiunoni! Hata mtoto wa la 2 anajua kinachoendelea..
Na mengineyo kibao... Inahitajika marekebisho makubwa na ya kiujumla.. Watengeneze kazi nzuri, kwa budget nzuri.. Wakikosa hela ndio walalamike... Sio hizi movies za kushoot chumbani na kamera moja.