Nini kifanyike kuboresha elimu yetu

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,502
6,403
Salamu wakuu

Imekuwa kawaida kwa watanzania na wasomi wa nchi hii kulalama kila uchwao kwamba elimu ya Tanzania haimjengei mwanafunzi uwezo wa kujitegemea mwenyewe pia mambo mengi yaliyopo katika mtaala hayana mlengo wa kumwendeleza kijana kwa maendeleo yake na taifa kwa ujumla.

Inawezekana kweli hata mimi hapa nimepitia elimu hii hii na bado natafuta kuajiriwa ndio niweze kujitegemea tofauti na hapo elimu hii niliyoipata inaweza kuwa kazi bure tu!

Sasa nimejiuliza sana, elimu yetu hii inakosa nini zaidi ili iweze kumjenga mwanafunzi kiteknolojia, kiutamaduni, kiuchumi, na kijamii kwa ujumla wake?

Mtaala tuliona uongezewe nini kitakachompa mwanafunz mashiko?
Huenda haya yote wadau wakuu wa madaliko hawayajui (serikali)

Uzi huu itapendeza utolewe mawazo chanja yamfikie waziri mwenye dhamana Ndalichako nini afanye kumwezesha msomi wa badae
 
Watawala waache kuingiza siasa katika elimu yetu waachwe wataalamu watoe mapendekezo kuhusu mambo ya kielimu kinyume na hapo hakuna kitu
 
Ngono zembe itokomezwe
Ndo walau tz tutainuka
Las vyo n mimba tu

Na skuhiz,znaanzia standard 7
 
Umeeleza vizuri kabisa ila umeharibu mwisho hapo

Ndalichako hana uwezo wa kubadilisha elimu hii zaidi ya matamko!

Ukiona unawaza hili tu basi ni elimh hii uliyoipata ndio inatumika
 
Mamlaka ya elimu ihuishwe, iitishwe forum ya kujadili elimu yetu, mitaala na falsafa ya elimu.
Mitaala yetu imeigwa kutoka mitaala ya uingereza miaka ya 50 iliyopita. Wakati wenzetu wazungu mitaala yao ni hai, yaani inaendana na mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi, teknolojia, siasa za ndani na nje, sisi mitaala yetu bado ni traditional. Nitoe mfano, wakati sisi tunahangaika kuprove g = 9.81 N/kg, kwa kutumia simple pendulum, wenzetu wao wamekubali g= 9.81 N/kg hawahitaji kuprove tena, bali wanaitumia katika kufanya discovery na some corrections. Tukija kwenye matumizi ya teknolojia: wenzetu baada ya mtoto kujua kusoma, kuandika, na kufanya hesabu( reading, writing, arithematic) hufundishwa kutumia tools km calculator na computational tools kurahisisha na kuokoa muda, sisi bado tunawapotezea muda watoto wetu kuwataka watumie maths tables tools ambazo kwa wenzetu zipo museum. Pili, wanafunzi wetu tunawalundikia masomo eg 11 kwa sekondari. Ni kumpotezea muda mwanafunzi. Wenzetu wapo focused tangu katika madarasa ya chini. Wanafundishwa masomo kutokana na carrier wanayoihitaji sio kijana anayetaka kuwa injinia unamfundisha majimaji war ...ya nini...you can't be master of all...tatu, tuandae walimu waliofaulu sana. Ushauri: kabla ya kufanya mabadiliko ya education system iitishwe forum katika vyuo mbali mbali ili tuandae mitaala kutokana na mahitaji ya jamii na mabadiliko ya teknolojia, uchumi, siasa, na mahusiano ya kimataifa....
 
Undugulization upungue kwenye kupeana majukumu,unakuta ofisi inakuwa na kabila moja au ukoo mmoja ,jambo hilo likomeshwe kwanza.
Salamu wakuu

Imekuwa kawaida kwa watanzania na wasomi wa nchi hii kulalama kila uchwao kwamba elimu ya Tanzania haimjengei mwanafunzi uwezo wa kujitegemea mwenyewe pia mambo mengi yaliyopo katika mtaala hayana mlengo wa kumwendeleza kijana kwa maendeleo yake na taifa kwa ujumla.

Inawezekana kweli hata mimi hapa nimepitia elimu hii hii na bado natafuta kuajiriwa ndio niweze kujitegemea tofauti na hapo elimu hii niliyoipata inaweza kuwa kazi bure tu!

Sasa nimejiuliza sana, elimu yetu hii inakosa nini zaidi ili iweze kumjenga mwanafunzi kiteknolojia, kiutamaduni, kiuchumi, na kijamii kwa ujumla wake?

Mtaala tuliona uongezewe nini kitakachompa mwanafunz mashiko?
Huenda haya yote wadau wakuu wa madaliko hawayajui (serikali)

Uzi huu itapendeza utolewe mawazo chanja yamfikie waziri mwenye dhamana Ndalichako nini afanye kumwezesha msomi wa badae
 
Nnavyoona Mimi siasa haiaffect elimu directly ila ina interfere mifumo ya kiutendaji ambayo ina operate huu mfumo wa elimu....
sasa kumbe hata tukisema tuiondoe siasa kabisa isikaribiane na mfumo wa elimu tutakuwa tuna purify mifumo inayoongoza mfumo wa elimu, kwa hiyo bado mfumo wa elimu utabaki na matatizo yaleyale mfano. Suala kushindwa la kujiajiri baada ya kuhitimu ngazi flani ya elimu..

Kwahiyo cha kufanya Ni kurekebisha au kubadili kabisa mfumo mzima elimu na kuweka mfumo utakaoweza kuwa applied kwenye real life field ..

Mapungufu yaliyopo kwenye mfumo wa sasa Ni kwamba, mfumo umejikita zaid kwenye nadharia pia haumuandai mwanafunzi kuweza kuitumia elimu yake katika ngazi za chini kabla ya chuo ( hapa ndipo tunapoanza kufail)

Mfano. mtu anasoma physics kuanzia form one hadi six lakin hawezi hata kubadilisha shitch ya Umeme ikiwa amesoma topic ya Umeme tangu olevel hadi A-level

Kiufupi Kuna mapungufu mengi katika mfumo uliopo kutokana Na maendeleo ya dunia tuliyopo
 
Warudishe mitihani yenye tija darasa LA nne na Iwe na mchujo,,, pili. Waondoe mtihan wa kubet ule wa darasa LA saba,, Tatu,, kidato cha pili kuwe na mtihan wa mchujo na uwe wastani wa kuanzia 30 hapo tutapata watu wanaojua mwisho,,, wanasiasa wasiingilie masuala ya elimu kila awamu na kuyabadili,,,,,,,,,,,,,,,,, uozo huu wote politicians ndo wawe blamed
 
Pia warudishe masomo ya biashara na kilimo, pia watoto wsfundishwe kazi za mikono wakiwa shule itasaidia kuja kujiajili baadae
 
Mamlaka ya elimu ihuishwe, iitishwe forum ya kujadili elimu yetu, mitaala na falsafa ya elimu.
Mitaala yetu imeigwa kutoka mitaala ya uingereza miaka ya 50 iliyopita. Wakati wenzetu wazungu mitaala yao ni hai, yaani inaendana na mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi, teknolojia, siasa za ndani na nje, sisi mitaala yetu bado ni traditional. Nitoe mfano, wakati sisi tunahangaika kuprove g = 9.81 N/kg, kwa kutumia simple pendulum, wenzetu wao wamekubali g= 9.81 N/kg hawahitaji kuprove tena, bali wanaitumia katika kufanya discovery na some corrections. Tukija kwenye matumizi ya teknolojia: wenzetu baada ya mtoto kujua kusoma, kuandika, na kufanya hesabu( reading, writing, arithematic) hufundishwa kutumia tools km calculator na computational tools kurahisisha na kuokoa muda, sisi bado tunawapotezea muda watoto wetu kuwataka watumie maths tables tools ambazo kwa wenzetu zipo museum. Pili, wanafunzi wetu tunawalundikia masomo eg 11 kwa sekondari. Ni kumpotezea muda mwanafunzi. Wenzetu wapo focused tangu katika madarasa ya chini. Wanafundishwa masomo kutokana na carrier wanayoihitaji sio kijana anayetaka kuwa injinia unamfundisha majimaji war ...ya nini...you can't be master of all...tatu, tuandae walimu waliofaulu sana. Ushauri: kabla ya kufanya mabadiliko ya education system iitishwe forum katika vyuo mbali mbali ili tuandae mitaala kutokana na mahitaji ya jamii na mabadiliko ya teknolojia, uchumi, siasa, na mahusiano ya kimataifa....
Well said mkuu!!
 
Husein bashe amepitishia petition kuhusu kujadiliwa upya kwa mfumo wa elimu... Ikishafikisha akidi ijadiliwe bungeni kama hoja binfsi ili raisi akubali kuunda tume ya kupitia upya mfumo wetu wa elimu.....link iko kwa page ake ya fb
 
Back
Top Bottom