Nini hatima ya Zanzibar?

Nini hatima ya Zanzibar?

Rufiji

Platinum Member
Joined
Jun 18, 2006
Posts
1,931
Reaction score
1,090
Wanabodi,

Ningependa kujua nini itakuwa hatima ya Zanzibar? Je uchaguzi utarudiwa? Au Maalim ataachiwa aunde serikali?
 
''Nimeridhika kwamba uchaguzi huu haukiwa wa haki na kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria na taratibu za uchaguzi," amesema Bw Jecha."Hivyo, kwa uwezo nilionao natangaza rasmi kwamba uchaguzi huu na matokeo yake yote yamefutwa na kwamba kuna haja ya kurudia uchaguzi huu."
Mara hii umesahau mkuu hilo tamko?
 
Matatizo kule yamekwisha. Wanataka kutangaza tarehe mpya ya Uchaguzi.Matatizo yamekwisha lakini sisi wanatuambia kwamba wanafanya majadiliano. Mimi nadhani JWTZ ndio tatizo. Mimi nimewahi kumsikia kiongozi mkuu wa jeshi akisema kwamba Zanzibar yakitokea maasi itakuwa very difficult kukabili. Mimi nadhani kukiwa na mazungumzo yanayowahusisha wanajeshi na wanasiasa,inaweza kupatikana ufumbuzi. UN haiwezi kusaidia. Au watu wowote wa nje. Wao wanaweza kusaidia kutekeleza jambo lililoafikiwa. Kama Jecha amekasirika kwamba Maalim Seif ametangaza matokeo bila ruhusa.basi Jecha awe appeased,na siyo aadhibiwe kama wengine wanavyosema,halafu aagizwe kutangaza matokeo. Kwa sababu delay inaleta hali ya wasi wasi. Ideal hapa ingekuwa Rais aapishwe leo halafu kesho amtaje Waziri. Mkuu au at least katika week end amtaje Waziri Mkuu baada ya kudurusu sifa za wagombea.
 
CUF wakikubali kurudia uchaguzi watakuwa wamefanya kosa kubwa sana! Na kusema ukweli awatashinda na ndio watajua nini maana ya goli la mkono.
 
Matatizo kule yamekwisha. Wanataka kutangaza tarehe mpya ya Uchaguzi.Matatizo yamekwisha lakini sisi wanatuambia kwamba wanafanya majadiliano. Mimi nadhani JWTZ ndio tatizo. Mimi nimewahi kumsikia kiongozi mkuu wa jeshi akisema kwamba Zanzibar yakitokea maasi itakuwa very difficult kukabili. Mimi nadhani kukiwa na mazungumzo yanayowahusisha wanajeshi na wanasiasa,inaweza kupatikana ufumbuzi. UN haiwezi kusaidia. Au watu wowote wa nje. Wao wanaweza kusaidia kutekeleza jambo lililoafikiwa. Kama Jecha amekasirika kwamba Maalim Seif ametangaza matokeo bila ruhusa.basi Jecha awe appeased,na siyo aadhibiwe kama wengine wanavyosema,halafu aagizwe kutangaza matokeo. Kwa sababu delay inaleta hali ya wasi wasi. Ideal hapa ingekuwa Rais aapishwe leo halafu kesho amtaje Waziri. Mkuu au at least katika week end amtaje Waziri Mkuu baada ya kudurusu sifa za wagombea.

Kwa maana yako hio ni kwamba Kikwete ndio tatizo Zanzibar. Kikwete ndie amiri jeshi mkuu na ni yeye ndie aliepeleka jeshi kule. Tumeshuhudia vifaru na nguvu kubwa ya kijeshi ikielekezwa visiwani. Kikwete ni mwenyekiti wa CCM na Rais wa JMT. Tusifanye kuzungumka mbuyu hapa, ina maana root souce ya matatizo ya Zanzibar ni CCM.

Ni kweli kabisa tatizo la zanzibar ni Ufashisti wa Watawala. Watawala hapa ni CCM!
WatawalaKule Zanzibar kwamba wameshindwa kisiasa na wanajaribu kutumia nguvu na mabavu kutawala ile nchi.
Watawala kule wanatumia vyombo vya dola (Polisi na Vikosi vya SMZ) kuwanyanyasa wananchi kwa kisingizio cha upinzani. Watawala wa Zanzibar wanawaona wapinzani ni sawa na mahaini!
Kwao kuvunja katiba ama kuua raia ni jambo dogo sana.

Watawala Zanzibar wanataka dunia nzima iamini ya kwamba vile visiwa ni mali yao ! na hakuna mtu mwengine anaeweza kuongoza Wazanzibari isipokuwa awe ni mwana CCM! Hilo ndio tatizo kubwa la zanzibar
 
''Nimeridhika kwamba uchaguzi huu haukiwa wa haki na kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria na taratibu za uchaguzi," amesema Bw Jecha."Hivyo, kwa uwezo nilionao natangaza rasmi kwamba uchaguzi huu na matokeo yake yote yamefutwa na kwamba kuna haja ya kurudia uchaguzi huu."
Mara hii umesahau mkuu hilo tamko?

hapo mkuu irudie hio kauli ya jecha kusema amefuta matokeo yote ya uchaguzi wa zanzibar,kwa maana hio matokeo ya uraisi na wabunge wa jmt zanzibar pia yamefutwa na kauli hio,lakini mwenyekiti wa nec yeye anayatambua matokeo ya ubunge na uraisi jmt kuwa ni halali kama alivyoletewa kutoka kwa mawakala wao zec zanzibar.
hii inamaanisha nini?
 
Kete yetu ya dhahabu wana mabadiliko wote ni Maalim Seifu kwa sasa, yeye ndie akomalie urais wa Zanzibar mpaka apewe haki yake na baadae ataitisha kura ya maoni juu ya muungano ili kuleta serikali tatu, hapo ndio utakuwa mwisho wa ccm huku bara pia,
 
Zanzibar uchaguzi utarudiwa kabla ya mwisho wa mwaka huu and it is apparent who will win this round
 
CCM walishasema nchi haiwezi kuchukuliwa kwa karatasi. Msikilize hapa Asha Bakari akimwaga sera ya CCM: www.youtube.com/watch?v=nQW3VP1W5hU
Wao wana sera inayosema "Mapinduzi daima". Kilichotokea Zanzibar ni mapinduzi. Uchaguzi utarudiwa na watahakisha "wanashinda". Kama CUF wakishinda tena uchaguzi utafutwa tena! Huu ndiyo ukweli.
 
Leo tunamuaga rasmi aliekua rais wa TAnzania Kikwete ,
Tutamkumbuka vyema
tunamtakia heri magufuli.....
 
Mkuu nmesoma post yako hakika inatia uchungu na cha kusikitisha zaid naangalia jins viongoz wetu wa kiimani walivyojaa unafki na wanajifanya kuomba kana kwamba hawajui kilichotokea kwny huu uchaguz na wala sijasikia kiongoz yyte akizungumzia hili,sijui huyu Mungu anayekubali udhalimu huu ni yupi,tuendelee kumuomba naamin anasikia kilio chetu naye hujibu kwa wakat muafaka.

Ndiyo maana ninasema kiongozi ye yote wa dini aliyealikwa na kwenda kuomba ni mnafiki na msaka tonge tu wa kawaida. Hivi walikuwa wapi kukemea uovu wa wazi uliokuwa unatendeka? Wanadhani Mungu anadhihakiwa. Wanasubiri sasa kuteuliwa makamishna kwenye taasisi mbalimbali pamoja na kualikwa ikulu kunywa na kula. Shame upon their faces.
 
Taasisi kama Bakwata zimeanzishwa kwa maslahi ya Watawala na sio kwako wewe mlipa kodi. Kama hivyo unategemea nini hapo?
 
Kwa maana yako hio ni kwamba Kikwete ndio tatizo Zanzibar. Kikwete ndie amiri jeshi mkuu na ni yeye ndie aliepeleka jeshi kule. Tumeshuhudia vifaru na nguvu kubwa ya kijeshi ikielekezwa visiwani. Kikwete ni mwenyekiti wa CCM na Rais wa JMT. Tusifanye kuzungumka mbuyu hapa, ina maana root souce ya matatizo ya Zanzibar ni CCM.

Ni kweli kabisa tatizo la zanzibar ni Ufashisti wa Watawala. Watawala hapa ni CCM!
WatawalaKule Zanzibar kwamba wameshindwa kisiasa na wanajaribu kutumia nguvu na mabavu kutawala ile nchi.
Watawala kule wanatumia vyombo vya dola (Polisi na Vikosi vya SMZ) kuwanyanyasa wananchi kwa kisingizio cha upinzani. Watawala wa Zanzibar wanawaona wapinzani ni sawa na mahaini!
Kwao kuvunja katiba ama kuua raia ni jambo dogo sana.

Watawala Zanzibar wanataka dunia nzima iamini ya kwamba vile visiwa ni mali yao ! na hakuna mtu mwengine anaeweza kuongoza Wazanzibari isipokuwa awe ni mwana CCM! Hilo ndio tatizo kubwa la zanzibar
kikwete si amirijeshi mkuu
 
Kiukwl ka seif atakbal uchaguzi urudiwe bc asahau ushnd mana jamaa nguvu yte ya bara inapelekwa znzr, naomba xn mungu seif akomae ad aapishwe huo utakuw mwanzo mzur kuwamegua ccm kiulain
 
Ndiyo maana ninasema kiongozi ye yote wa dini aliyealikwa na kwenda kuomba ni mnafiki na msaka tonge tu wa kawaida. Hivi walikuwa wapi kukemea uovu wa wazi uliokuwa unatendeka? Wanadhani Mungu anadhihakiwa. Wanasubiri sasa kuteuliwa makamishna kwenye taasisi mbalimbali pamoja na kualikwa ikulu kunywa na kula. Shame upon their faces.
kama unaweza kupata ombi alilo omba Askofu malasusa hebu lisikie vizuri mkuu kuna message kali sana
 
Kwa Zanzibari tunasubiri siku 90 uchaguzi mwingine ufanywe, kama Maalim Seif alishinda kihalali basi atashinda tena kihalali. tatizo naloliona ni kwamba wanasiasa hawana tatizo na wanacheka pamoja, ila mashabiki wao ndio wanaotaka kuleta matatizo kama Makongoro alivyosema awali.
 
Back
Top Bottom