I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,730
- 10,033
Binafsi sioni tofauti yoyote iliyopo siku hiyo ya tarehe 1 mwezi wa kwanza, ingawa nimezaliwa na kukuta utamaduni wa kuitukuza sana siku hiyo upo. Utaratibu huu wa kuikuza siku hiyo sijui umeanzia wapi.
Ukiangalia kwa umakini siku hiyo haina lolote jipya tofauti na siku nyingine za mwaka. Au shida ni namba ambayo mzungu aliipa siku hiyo?? Siku inakuzwa sana hii.
Imezoeleka kuonwa watu mbalimbali wakimsifu Mungu na wengine kulia kwa furaha, wengine wanalazimika hata kugharimika vitu ambavyo walikuwa hawafanyi siku zote yote hiyo ni ili kuonekana nao wapo katika msafara wa kufuata mkumbo ila yote hayo kisa tu wameweza kuiona siku inayofuata baada ya tarehe 31 disemba. Khaaaa! Huu ni upumbavu uliokubuhu. Hayo yanayofanyika tarehe hiyo yaendelezwe pia na siku zinazofuata italeta maana zaidi.