Nini chanzo cha vijana wengi Dar kupoteza mwelekeo wa maisha?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,183
3,547
Tunaposema mtaani hali ni ngumu ni ngumu kweli ni vigumu kuamini lakini ndo ukweli hapa watu washio jiji la Dar wameshapoteza mwelekeo wa maisha.

Nilijaribu kupita maeneo mengi hapa Dar nikagundua watu wengi wameshapoteza dira kutokana hii imeshakuwa mfumo wa maisha ya vijana wengi hapa Dar.

1. Kuna kundi la vijana ambao wanawaza kuuza nyumba na pesa ikipatikana wagawane ili kila mtu awe na maisha yake.

2. Wadada wengi wamejiingiza katika biashara ya ngono kwa ajili ya kujitafutia kipato.

3. Baadhi ya vijana waliopo Dar wanaishi kwa kuokota makopo na kula majalalani.

4. Kuna vijana ambao hadi sasa wameshakata tamaa maisha wao wamejiamulia tuu kuvuta unga na kukaba watu mitaani.

5. Kuna vijana ambao wapo mitaani baada ya kukosa kazi za kufanya wao wamejikita katika kufatilia maisha ya watu.

6. Kuna vijana huku mtaani wao maisha yao wanategemea kucheza michezo ya kamali, pool table, kubeti ili kujipatia kipato kwa ajili ya kuendesha maisha na familia .

7. Kuna vijana wasomi ambao hawakubatika kupata ajira wengi wao wameishia kukaa vijiweni, madalali, wanywa kahawa vijiweni na wengine ni matapeli.

8. Kuna vijana wa kiume sasa hivi wameamua kuishi na wamama waliowazidi umri maarufu kama majimama just becouse kutafuta unafuu wa maisha.

9. Kuna vijana ambao wao ambao wameamua kuvuta bangi na kuvuta unga ili kupunguza stress na mawazo katika maisha.

10. Kuna vijana wao wamejingiza katika ulevi viroba na gongo kama pombe kali wanakunywa just kupunguza stress katika maisha.

11. Kuna vijana wao wameamua kuvunja undugu na ndugu zao wenye uwezo kwa sababu wameshidwa kuwasaidia either katika ajira na mengineyo hivo wameona bora undugu ufee.

12. Kuna vijana hadi leo hii bado wanawaza kujiunga na freemanson ili waweze kuwa na maisha mazuri na huwa hawaogopi kutoa wazazi wao maisha kwa ajili ya huo utajiriii.

13. Kuna vijana hapa mjini wao wanaishi maisha ya MDANANDA wao kazi yao ni kuwatafutia WATU MASHUHURI NA WENYE PESA kama vile akina WABUNGE AU AKINA PAPA wanawake wazuli wazuli kwa ajili ya kujipatia kipato.

14. Kuna kundi la vijana wao wanategemea kuishi MAISHA FITINA NA UNAFIKI kwa ajili kujipatia kipato kazi yao ni kutoa maneno huku na kuyapelekaa.

Ni mengi ya kuzungumza. Je, unadhani nini chanzo hadi kuishi maisha aina hii? Na, je ni wapi walikosea?
 
Ili kujenga taifa bora lenye watu makini wanazuoni wanahitajika kufanya tafiti kwenye hili, ili kusaidia jamii inayowazunguka. Otherwise itakuwa tunatengeneza bomu kama brazil vijana welivyokuwa vibaka na waporaji kipindi cha worldcup. Hata hao wenye kipato na kufurahia maisha wataishi kwa wasiwasi na ulinzi mkali.
 
jamaa amejaribu kuonesha amegushwa na suala la vijana kupoteza mwelekeo. Hivi vizazi vyao vitakuje
 
Hayo mambo darisalama yapo tangu na tangu na bado mji unaendelea kutanuka na kukaribisha wageni kama wewe muje kushangaashangaa,kamari na uhuni wote uloutaja hapo juu sio mgeni mji huu,kilichobadilika skuiz ni teknolojia tu,na ndo mji unaoongoza kwa kulipa mapato TRA,kwahyo ujue tu kuwa wapo vijana wenye shuhuli zao na ni wengi kuliko hao wasio na shuhuli
 
Mm namba tano ndo imeniacha hoi....yaani vijana baaada ya kufanya kazi kwa bidiii wao wanatumia nguvu nyingi kuchunguza umbea na maisha ya watu?
 
Hali ngumu haijaanza leo na hayo makundi uliyotaja yapo miaka yote tena miaka ya nyuma ukabaji na uporaji ulikuwa mara dufu hapa Dar.Utafiti wako ni wa kishamba sana siku nyingine sema tu ni maoni yako maana utafiti unahitaji details za maana
 
Hali ngumu haijaanza leo na hayo makundi uliyotaja yapo miaka yote tena miaka ya nyuma ukabaji na uporaji ulikuwa mara dufu hapa Dar.Utafiti wako ni wa kishamba sana siku nyingine sema tu ni maoni yako maana utafiti unahitaji details za maana
unachozungumza ni sawa lakini twende mbele turudi nyuma kwa miaka ya nyuma haya mambo kweli yalikuwepo lakini kwa sasa yameongezekaa not only uporaji pia kuna mambo mengine ya kuzungumza kuhusu maisha inakuwaje hatukubaliani na ukweli
 
Mm namba tano ndo imeniacha hoi....yaani vijana baaada ya kufanya kazi kwa bidiii wao wanatumia nguvu nyingi kuchunguza umbea na maisha ya watu?
Rwankomezi hii kitu isikie tuu huku mitaani bana kuna watu wanajua kuchunguza maisha ya watu sio hivo tuu unaweza ukawa mambo yako kwa siri lakini ukashangaa watu wamejuaje na ni nani amewambiaa
 
15.Kuna vijana wamekua makaka poa kujipatia kipato
dah hili swala ni zito sana kulielezea coz linatia uchungu lakini utafanyaje hivi mpaka anafikia hatua hii huyu tena basi kabisaa sii ndugu yetu
 
Hii apelekewe Makonda ameshindwa kabisa kuweka mikakati walau yakupunguza hizi kero.

Sijui kajichimbia wapi huyu mtu..?
 
Umesahau ongezeko la machoko aka mashoga na wasagaji.. kila baada ya nyumba moja kuna shoga au afananae na shoga.

Dar bana...!
 
Back
Top Bottom