Nini chanzo cha kuvimba mwili ghafla pasipo kusikia maumivu?

Ulirchdov

JF-Expert Member
Apr 4, 2019
356
258
Wakuu salamu ziwafikie

Kwanza nianze kutoa shukurani kwa Mungu muumba aliyetujalia uwezo wa kuiona leo wapo wengi waliotamani kuiona leo lakini kwa mapenzi ya Mungu wametangulia mbele za haki, walale pema wanapostahili. Wengine ni wagonjwa wapo hospitalini kwa ajili ya tiba ila wapone Mwenyezi Mungu awalejeshee tumaini na kuwapa afya njema.

Baada ya hayo yote nipende kuwashirikisha tatizo linalomsumbua mdogo wangu(tafadhali naomba nieleweke kuwa ni mdogo wangu usiseme ni mimi ila nimeogopa kujitaja la hasha, tatizo linamsibu mdogo wangu) tatizo lenyewe ni kwamba amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda wa miaka miwili sasa, maradhi ambayo chanzo chake hakijulikani kwani tumempleka hospitali kufanya vipimo tujue nini hasa chanzo cha tatizo lake na tiba gani inaweza kumsaidia kurudi katika hali yake ya kawaida kwasababu huwezi ukaanza tiba pasipo kujua chanzo ni nini.

Mdogo wangu anasumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu,kichwa,mikono, tumbo na vinginevyo kiufupi anavimba mwili mzima licha ya kukumbwa na tatizo hili hakuna maumivu yoyote anayosikia hii ni kwa mujibu wa maelezo yake, tatizo limedumu kwa miaka miwili ambapo awali lilianza akiwa shuleni akafikiri labda ni hali ya kawaida, alianza kuvimba miguu baadae kichwa hatimaye mikono tatizo likawa kubwa hadi kuanza kuvimba mwili mzima.

Mwanzoni hatukuweza kubaini chanzo, baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya tukaamua kumpeleka hospitali ili kufanya check up kwasababu kuna baadhi ya watu waliokukuwa wakimwona walidai huenda tatizo lipo kwenye figo, baada ya kufanyiwa check up madaktari walibaini kuwa hakuna tatizo linalomsumbua figo ziko vizuri, hatukuishia hapo tukampeleka hospitali nyingine majibu yalikuwa yale yale kama mwanzo, hatukukata tamaa tukampeleka hospitali nyingine tena(hospitali ya mkoa) majibu yalikuwa yale yale ya hospitali za awali.

Mwisho wa siku tuliamua kurudi nyumbani tukakae chini tena ili kuja na uamuzi ambao unaweza ukamsaidia mdogo wangu apone baadhi waliamua tumpeleke kwa wachungaji akaombewe wengine wakasema tumpeleke kwa sangoma anaweza akamsaidia maana huenda wapo waliofanya michezo yao michafu ili Dogo ateseke.

Wakuu naomba kujua mwenye uelewa kidogo wa hili tatizo au ambae alishawahi kukumbana na hii hali aweze kunishauri mbinu za kitabibu ili mdogo wangu apone na kurudisha furaha yake maana amekuwa mtu ambaye anasononeka kila uchao ameathirika kisaikolojia, ni mwanafunzi anatakiwa awe shuleni lakini haya maradhi yamefanya asitishe masomo kwanza hadi atakapopata nafuu.

Ushauri wako ni muhimu, naombeni mawazo yanu ndugu zangu.

Nawasilisha!!
 
hata mimi nimesoma headline nikajua ni figo maana ndo inasababisha water retention mwilini,
 
hata mimi nimesoma headline nikajua ni figo maana ndo inasababisha water retention mwilini,
Mkuu watu wengi wakimwona dogo wanasema moja kwa moja tatizo linaweza kuwa kwenye figo lakini madaktari wa hospitali zote tatu tulizoenda wanasema figo ziko vizuri hazina tatizo kabisa
 
Mimi niliwahi kuvimba miguu, mashavu, ukibonyeza mwili kinatokea kitundu kwa mda hafu kinapotea nilienda hospitari nikapewa dawa ya kupunguza maji mwilini kwa njia ya kukojoa sana tatizo likaisha ila sikujua chanzo kilikuwa ni nn
 
Mimi niliwahi kuvimba miguu, mashavu, ukibonyeza mwili kinatokea kitundu kwa mda hafu kinapotea nilienda hospitari nikapewa dawa ya kupunguza maji mwilini kwa njia ya kukojoa sana tatizo likaisha ila sikujua chanzo kilikuwa ni nn
Awali tulipompeleka hospital alipewa dawa ambayo itamsaidia kukojoa kwani ilidhaniwa kuwa huenda uwingi wa maji ndiyo humfanya avimbe ila tatizo halikuisha hali ilizidi kubadilika
 
Back
Top Bottom