Nini asili ya neno bodaboda?

Sio kweli, asili yake ni kutoka uganda mkuu na sio Kenya kama walivyoeleza wadau hapo juu
 
Umemaliza kila kitu mpaka nimekosa cha kumuongeza.
 
Wadau nawasabahi Nimekuwa nasikia Waendesha Pikipiki za biashara wanaitwa BODABODA binafsi sijui kwanini wanaitwa jina hiyo .Ombi kwenu nini Asili ya jina hilo mpaka Wakaitwa hivyo?
Kwa watu wa Kyela ni jina la miaka na miaka enzi za kina Kaka, mabasi ya Kyela yalikuwa yakifika karibu na Kyela mijini akina Matemabeach, Zainab, Railway na mengineo yanasimama njiapanda ya kwenda Kasumulu ambako ni mpaka wa Tanzania na Malawi, hapo njiapanda walikuwepo vijana wenye baisikeli zenye viti vipana kwa kubeba abiria, basi likisimama vijana hao huanza kuita abiria kwa kusema "BODA" wakiwa na maana ya kuwapeleka Kasumulu kwenye mpaka wa Tanzania na Malawi, hicho ndicho chanzo cha jina Bodaboda.
Dar na kwingineko kusikokuwa na mpaka wa nchi na nchi wameiga tu jina bila kujua ili uite Boda lazima uwe na mpaka, hata hivyo jina ni jina litumikapo halina tafsiri tena.
 
BH
Ni kweli, kwa kuongezea tu; ilianza na baiskeli, ndio zilikua zinaitwa bodaboda, hata Kampala mjini.
 
Mara ya kwanza kuona bodaboda ni uganda 2005 kwenye nyimbo ya chameleon SHIDA ZA DUNIA..!!2005 Tz biashara hio hakuna na ukimiliki pikipiki wewe ni gumzo mtaani mana hata Kumiliki TV nyumba 50 mtaani kwenu wenye tv hawazidi 7..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…