NINI ASILI YA MIEZI YETU HASA JANUARY

NINI ASILI YA MIEZI YETU HASA JANUARY

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,348
Reaction score
1,097
JANUARY ni mwezi wa kwanza wa mwaka . asili ya jina hili au mwanzo wake ni MUNGU wa kiroma aliyekuwa anaitwa JANUS .

JANUS ni Mungu ambaye waroma , walimuabudu,( Roman empire kipindi hicho takribani miaka 700 Bce).

Mungu huyu ni Mungu wa mwanzo na mpito yaani ni Mungu wa malango na mwisho wa Muda. Anasadikiwa ana sura mbili , mbele na nyuma , Roman empire waliamini kuwa anaangalia future and past ( zamani na kipindi kijacho).

mungu huyu Janus viwakilishi vyake katika ulimwengu wa roho ni MILANGO, MAGETI,MADARAJA , yaani vitu vinavyoashiria kupita .

Mara nyingi mungu huyu wa kuzimu yupo kazini kipindi cha Mwisho wa mwaka, anakaa katika mabarabara , madaraja .

mungu huyu Janus huwa anapitisha maazimio ya Yale uliyoyafanya na yale unayotarajia . anapenda sana kukumbukwa kwa sherehe kwa matukio yaliyopita au yajayo ... January na December ni kipindi chake.

mungu huyu anahusika sana na mtembeo , mabadiliko na muda.

Ukisoma maandiko mbalimbali hasa Roman mythology, alikuwa mungu wa mwanzo wa dunia na alilinda geti la mbinguni ..... Kuonyesha ni wa hila na ni Lucifer mzima , alijiita god of god ( diuom deo).

wakristo wengi walikataa kumuabudu mungu huyu , ila wengine walitekwa na mungu huyu . Leo hii wanasherehekea pasipo kujua ...... Ni vyema ukasherehekea ukiwa na wokovu kuliko ukachotwa na mazingira .... Kumbuka maandiko ya biblia matakatifu kipindi cha Eliya nabii , manabii walikuwa zaidi ya 400 fake.....

Refer matendo 13:6-7, 14:11-13 , 16;16-18

Kwa taarifa yako mwanzo wa mwaka ulikuwa ni mwezi wa march lakini kwa hila za mungu Janus imekuwa January , mpaka Leo.

Maana ya kila mwezi

1. January---- janus mungu
2. February---mungu wa kirumi februus kwa ajili ya utakaso( god of purification)

3. March---mars , mungu wa vita

4. April--- Aphrodite , mungu wa uzuri au neno la kilatini aperire , kipindi maua mimea inachipua.

5. May --- maia mungu wa dunia kipindi mimea inakua.

6. June---juno mungu wa ndoa na mke wa sayari Jupiter mfalme wa miungu , mwezi huu ndiyo mwezi wa sherehe za ndoa ,,,,inaaminika kwa hii miungu kuwa kila atakayeoa mwezi huu atapata mafanikio.

7. July--- zamani ilijulikana kama Quintilis( neno la kilatini fifth 5 kwa kuanzia march). Baadaye ulijulikana kwa jina la Julius Caesar kwa heshima ya kupangilia kalenda mwaka 46bce.

8. August--- august Caesar kwa heshima ya binamu na mrithi wa Julius Caesar.

9. September--- kutoka neno la kilatin , September ( seven ukianzia mwezi march) . ulikuwa mwezi wa saba kwa mujibu wa kalenda ya kirumi.

10. October--- kutoka neno la kilatini octo ( 8 kuanzia mwezi march kalenda ya kirumi)

11. November--- kilatini novem (9)

12. December---- kilatin decem (10)

Ayoub 22:21 "mjue sana Mungu , ili uwe na amani ; ndivyo mema yatakavyokujia....

be inspired
 
Hii calender ina mambo makubwa sana
Hata ukiangalia mchakato wa kuitengeneza imekubikwa na siri kubwa sana!! Babadiliko yake mawili ya mwishoni yanaonyesha wazi dunia inaongozaa na Wapagani...... Hii ni calenda ya KIPAGANI yenye siri nzito za Roma
 
Back
Top Bottom