Ningemu'ua mama

salum mabura

Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
67
Reaction score
5
Yaani leo nimeamka asubuhi ile natoka nje tu nakutana na mama anatoka jikoni kashika kibakuli mkononi!
Huku akiwa nawasiwasi mwingi akaniuliza hivi ''kwenye hili bakuli kulikua na samaki ulikula wewe?"
Nikamuuliza yule samaki ambaye hakufunikwa!?
Akanijibu ndiyo! Nikamwambia
Nilikula kichwa tu na mkia kidogo basi!
Akasema kwa hofu na huku akionesha kuchanganyikiwa, Mungu wangu wee nimeua mwanangu!
Nikamuuliza kwa mshangao kwa nini mama?!
Akanijibu nilimtegeshea panya! nikamwambia usihofu mama nilipomuona huyo samaki hapo juu niliamua kumchanganya na wenziwe ndani ya sufuria!
Akanambia kushaniua!nimetoka kuonja sasa hivi!
Na mimi nikachanganyikiwa, nikamwambia hapa mtaani hakuna mtu anaefuga ng'ombe ili tupate maziwa na maduka yako mbali!
Akaniuliza sasatufanyeje?
Nikamwambia nikienda kukuchukulia mimi tutachelewa kwa hiyo twende wote utanywea hukohuko!
Tukaanza kukimbilia dukani tunafika njiani nikakumbuka jana usiku!
Mdogo wangu alitahadharishwa na mama kuhusu hiyo sumu ya panya lkn mama mimi hakuniambia!
Kwahiyo mdogo wng alinitahadharisha!
Nikamwambia mama turudi!hata baada ya kumuelewesha aligoma hadi alipohakikisha kanywa maziwa!
Halafu akanambia watoto wa siku hizi hamuaminiki!

JF:THE HOME OF GREAT THINKER!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…