Ningekuwa ndio nchi wahisani, ningefanya hili

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,673
149,858
Nisingeangaika kushinikiza sijui utawala wa sheria/utawala bora wala kuhimiza au kuweka mashariti yenye kushinikiza uhuru wa habari,n.k bali ningetoa shariti moja tu la kutotoa msaada wala mkopo wa aina yoyote kwa nchi yoyote ya kiafrika isiyokuwa na Tume Huru ya uchaguzi.

Mbali na nchi wahisana,hata mashirika ya fedha duniani kama IMF na Benki ya dunia wanapaswa kutazama upya sera zao hasa kuelekea nchi za kiafrika na kuweka mashariti mapya likiwemo hili la kutaka nchi yoyote inayoomba msaada/mkopo ni lazima iwe na Tume Huru ya Uchaguzi.

Ikiwezekana waweke na shariti la ziada kuwa Tume Huru ni ile ambayo itakuwa imekubalika na vyama vyote vya siasa katika nchi husika ili kuondoa uwepo wa Tume Huru jina.

Tukiwa na Tume Huru haya mengine yote yatawezekana maana kikwazo kubwa ni watawla/vyama dola na si kitu kingine.
 
Sijui kwanini nchi wahisani hawalioni hili.
Mkuu naamini sisi wenyewe tunaweza kulimaliza hili. Siamini sana katika suala la wafadhili. Hawa wafadhili huwa hawana nia njema na nchi zetu hizi za kiafrika, wao kwao ni maslahi yao binafsi. Kuna nchi hazina demokrasia lakini hawafanyi lolote ili mradi tu maslahi yao yapo salama.
 
Ndio kazi ya chadema siku hizi kuombea kila aina ya maovu yatokee Tanzania.

Tume inakuwa nzuri na huru inapowatangaza washindi Mbowe, Lisu, Lema, Mdee etc

Lakini tume hiyo hiyo inakuwa siyo huru inapowatangaza Magufuli, Zungu, majaliwa, Nchemba etc
 
Ukweli ambao hata wewe hutaki kusema ni kwamba hao nchi wahisani wanaendeshwa na maslahi yao kwanza.
Usitegemee kwenye kichwa chako kwamba ipo siku Marekani, Uingereza, Uchina au Canada watakuja kukuendeleza bila kuangalia maslahi yao kwanza. Mathalani hakuna nchi yoyote hapa duniani ambapo Demokrasia yake, Haki za binadamu na Utawala bora vimejengwa na nchi nyingine, hasa kwa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi: Kama ipo itaje hapa ili uwe mfano halisi.
 
Sijui kwanini nchi wahisani hawalioni hili.
Mkuu naamini sisi wenyewe tunaweza kulimaliza hili. Siamini sana katika suala la wafadhili. Hawa wafadhili huwa hawana nia njema na nchi zetu hizi za kiafrika, wao kwao ni maslahi yao binafsi. Kuna nchi hazina demokrasia lakini hawafanyi lolote ili mradi tu maslahi yao yapo salama.
 
Mkuu naamini sisi wenyewe tunaweza kulimaliza hili. Siamini sana katika suala la wafadhili. Hawa wafadhili huwa hawana nia njema na nchi zetu hizi za kiafrika, wao kwao ni maslahi yao binafsi. Kuna nchi hazina demokrasia lakini hawafanyi lolote ili mradi tu maslahi yao yapo salama.
Mkuu,katika hili,nasema, "the end justifies the means."
 
Nchi wahisani zinaangalia maslahi yao kwanza. Na inapotokea vyama vya upinzani vina viongozi dizaini ya akina Freeman Mbowe ambao hawaandiki hata "papers" au kufanya dialogue za mara kwa mara na hawa watu, wanaweza wasijue kinachoendelea. Huenda hadi sasa hawajui kama Lema amefungwa, huenda hawajui kama tumeambiwa tubebe mzigo wetu, wakati wao wanajaribu kutusaidia mzigo
 
Back
Top Bottom