Ningekuwa Mzee Mukama-SG wa CCM...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ningekuwa Mzee Mukama-SG wa CCM...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by pinguli, May 2, 2012.

 1. p

  pinguli Senior Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilipopata kujua nini maana ya kuwa katibu mkuu wa Chama, ndipo nilipopata kuwaza haya ninayoyawaza.,kwa kauli ya waziri wa fedha Ndugu Mkulo, iliyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari wiki moja iliyopita ni kuwa, mheshimiwa huyu anadai kuwa yeye hawajibishwi na chama ama kamati za chama.,na kwa maana hiyo chama hakina nguvu juu yake..,kauli hii inanifanya niikumbuke kauli ya wadau wanaojiita wanaharakati walipowahi kusema kuwa chama cha mapinduzi (ccm) ni chama legelege na kauli za mwalimu kuwa chama legelege huzaa serikali legelege ndio haya yanadhihiri leo.

  Kama ningelikuwa Mukama.,nisingelidharau kauli hii na kuifanya ni ya kupita, nisingelikubali kuona kuwa watu wanachama wanakuwa na nguvu na uwezo wa kukejeli nguvu ya chama, nisingelikuwa tayari kuona kuwa serikali yangu inakuwa legelege kwa kuwa chama changu ni legelege. Ningelimuita Mkulo na kumuonya na hata kumtaka arudishe kadi ya chama ili iwe ni fundisho kwa wengine,nisingelikubali kuona viongozi wa serikali wanavimba vichwa kupitia mgongo wa chama na huku wanadharau chama. Ningelikuwa Mukama nisingelikubali haya...!
   
Loading...