Ningekuwa kikwete, hotuba yangu mwisho wa mwezi huu ingekuwa hivi

baluhya M.

Member
Apr 22, 2011
33
79
Ndg wananchi leo hotuba yangu ya mwisho wa mwezi tofauti na miezi mingne itakuwa fupi sana, itahusu mambo mawili tu yaliyotikisa taifa katika huu mwezi unaoisha, nayo ni Kifo cha Daudi Mwangosi na Dr Swakala na sign 200 za kuombea msamaha.. Ndg wananchi Sitaki kuongea mengi juu ya kifo cha Daudi Mwangosi maana mengi yamesemwa, mimi leo nataka nitangaze tu kuanzia leo waziri wa mambo ya ndani Dr. Nchimbi, IGP- Mwema, RPC-kamuhanda, MSAJILI wa vyama vya Siasa- TENDWA nimewafukuza kazi na watatakiwa kukamatwa mara moja, nataka hili liwe fundisho kwa wateule wangu wanaojipendekeza kwangu kwa gharama yoyote ikiwemo kuua raia ambao nimeapa kuwalinda kwa mujibu wa katiba. Kuhusu nafasi zao, nitatangaza wiki ijayo watakao jaza nafasi hizo. Kuhusu Dr SWAKALA na kikundi chake cha watu 200 nimeagiza vyombo vinavyohusika kuwa kamata mara moja na hukumu yao nimeelekeza iwe kati ya kifungo cha maisha na kunyongwa, hili litakuwa fundisho kwa watanzania wote wanaoshiriki migomo halafu wanaishia kusingizia watu kwamba waliwashawishi. Kimsingi ndg wananchi haingii akilini mtu ugome karibu mara 4 ktk kipindi cha miezi 7 halafu uje uende habari maelezo kusema kuwa ulipotoshwa na MAT. Mwisho kabisa natangaza kuwasamehe madaktari wote waliosimamia Ukweli hadi mwisho wakiongozwa na Dr. ULIMBOKA, DR. Chitage, Dr. Godbles na Dr. Namala, hvyo madaktari wote ambao wako na Jumuiya madaktari ya Dr. Ulimboka, wanapaswa kuanza kuripoti katika vituo vyao vya kazi mapema iwezekanavyo. Leseni zao na malipo yao ya usumbufu yatawakuta hukohuko kazini. Nawaahidi kuwa serikali yangu imebaini madai yao yalikuwa ya msingi na yenye lengo la kuleta mapinduzi ya sekta ya afya,hvyo nitawapa ushirikiano wangu binafsi na wa serikali yangu katika kuhakikisha tunaleta mapinduzi ya kweli katika sekta ya Afya. Asanteni kwa kunisikiliza.
 
Hayo maoeno ndiyo anayopenda kuyasema...lakini atakayo yasema ni haya

"ndugu wananchi na wafia nchini, heri mwenzenu nimetembea tembea kidogo huko.... Baada ya kuruka juu sana tena mara nyingi kama yule ndege mwerevu mbayuwayu, nimeona nije na swagger ya mabasi yaendayo baru. Ndugu zangu mnataka nini tena? Mradi ndio hivyo kama mlivyoona na jana nimeweka jiwe la ufunguzi...wenye wivu wa mandeleo haya, wachimbe shimo wajifukie.

Pili wazaramu wenzangu wa kule Bagamoyo toka mkoloni hadi leo hamjawahi kupanda gari moshi...sasa mnapokuja kushangaa shangaa hapa mjini, tembeleeni Ubungo...ingieni kwenye mchuma wa chuma kwa chuma...hadi Posta, nanyi mlimbuke mwaka...sawa ndugu zangu wakina Kombo, Uzegeni, Mwanahawa na Siyawezi....hahahaha nalo ni jambo kubwa kabisa, halijawahi kufanyika kabla ya Uhuru na Baada ya Uhuru.

Tatu, wale wa Kigamboni ambao walikuwa wanashindwa kuvuka kwa kutumia Pantoni kwakuwa nauli iliwashinda...hadi nikamwambia waziri wangu machachari awanange kuwa 'muogelee na Kupiga mbizi..' nimetafakari kauli ile na kuona kuwa mliudhika sana..nanyi sitawaacha mbugie maji..ninawajengea daraja..mtavuka bure...bureee bila hata senti moja. Chapaa zenu kidogo mlizokuwa mnatumia basi mnunue hata vivocha vya simu ile mlonge longe...si ndio wandugu?

Nisiwachoshe msinichose...tuchape kazi...na wale wenye viwanda vya kutengeneza uwongo...tafuteni uwongo mwingine...Dar itakuwa kama mamtoni ndugu zangu.

Asanteni sana kwa kunisikiliza"
 
Angeongezea na kuwataja wale wauza dawa za kulevya ambao alisema majina yao anayo maana wale wanauwa wengi kuliko policcm.
 
Huyu bwana hawezi, kwanza anataka aongeeeeeeeeee ndo anapata raha, kurasa kama 100 za "empty words"
 
ongezea hii, mke wangu na mwanangu wamepita bila kupingwa kwenye uchaguzi wa ndani wa ccm,hii inaonyesha demokrasia nene sana kwenye chama changu cha ccm
 
Aiseeee babaangu baada ya hotuba iyo fufi nape lazima aunge mkono hoja hama kweli akili za nepi ni kama za mbuzi kondo
 
Hiyo itakuwa hotuba ya Mhe Rais au Mhe Rahisi?

Back
Top Bottom