Viongozi wa USA ni mfano mzuri sana katika kuchukua hatua pale unapoona huendani na misimamo ya Rais. Wengi tu kule USA walishachukua hamsini sana kiroho safi baada ya kumuona Donald Trump anazingua.
Wamefanya hivyo kina John Kelly, Ryan Zinke, James Mattis nk
Hali ni tofauti sana kwa Africa. Sisi unafiki tunauweza.
Kwa hapa Bongo CAG kajitoa muhanga japo ni kwenye jambo ambalo lipo wazi sana kila mtu anajua bunge halipo huru.
Ukiangalia ghazabu aliyokuja nayo Spika ni wazi kuwa watu hawa hawawezi tena kufanya kazi kama kitu kimoja. Wameshazinguana. Chukulia pia taarifa ya Zitto Kabwe kwamba Spika ameziambia kamati zisifanye kazi na CAG wala wasaidizi wake.
Sasa kuna nini hapo......
Ingekuwa mimi ndiyo Prof. Assad nakuachia tu kibarua chako. Kwani nini bwana