NINGEKUA RAIS WA Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NINGEKUA RAIS WA Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mmzalendo, Mar 5, 2011.

 1. mmzalendo

  mmzalendo Senior Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 165
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi ningekuwa rais ningejari shida za wananchi na ningetimiza ahadi zangu zote pia nisingetoa ahadi zisizotekerezeka wakati wa kampeni,ili kuwa na kazi rahisi wakati wa urais wangu na pia
  wakati wa kugombea awamu ya pili nisisumbuke na makapeni.

  mimi ningekuwa na rais hakuna urafiki na fisadi mafisadi wote ningetumia sera za mwalimu
  kufirisiwa tu hawa ni waujumu uchumi na sera bi kuwaogopa kama ukoma, nisingejali nina wajua
  au siwajui wao wangekwenda jela tu kufanya kazi ngumu

  mimi ningekuwa rais kila waziri ninayemchagua angenipa barua ya kujiudhuru kwanza ningezifungia sehemu na siku hakiwauzi wananchi kwa kuboronga barua hiyo ningeitoa fasta
  na yeye kaisha kazi yake mpaka hapo hana bao, huu sio udikiteta jamani ningekua nafuata ya wananchi maana wao ndio wenye nchi.
  mimi ningekua rais ningeondoa upendeleo wa huduma hakuna cha vigogo wala vijiti wote wangetibiwa na kuishi maisha sawa na kama ili la umeme mgao ungekwenda mpaka ikulu maana sisi ndio tulioshindwa kazi na kuonja shubiri yake itanifanya kufanya kazi kwa juhudi, pia hii itanisaidi kujua kama kuna mgao huko kwa wananchi, katika hiyo nitatunga sheria waziri atakaye sababisha mgao ikulu hata kuwa ameujumu uchumi na hatakwenda jela.
  ningelikuwa rais singeweka maisha ya watu wangu kwa mafisadi bei za bidhaa zingedhibitiwa na serikali na vinapanda kwa sababu muhimu tu na lazima zisibitishwe.
  mimi ningekuwa rais ningemfukuza kazi waziri wa nishati na madini na waziri wa fedha na waziri wa ulinzi, pia magufuli na mwakyembe nisingewaweka wizara moja, sita ningempa utawala bora.
  ningekua rais kila kinacho andika gatezini ningekifanyia kazi na wala sito sema sifanyii kazi magazeti maana haya ndio kiungo cha jamii wao niwatafuta na watoa taarifa kwa hiyo taarifa zao zote ningezifanyia kazi na kama ningedungua uongo ningetoa adhabu kali
  mimi ningekuwa rais mawaziri na wabunge wangetumia magari yao binafsi mbona waingereza wana hela kuliko sisi wanafanya hivyo sio watu kugombea vyeo kuishi kifisadi badala ya kusadia umma, hakuna matumizi ya kijinga sisi ni watumishi wa umma
  mimi ningekuwa rais mikopo ya elimu ya juu ningetoa kwa wenye uwezo wa chini tu na wenye uwezo wazazi wao wagewalipia
  mimi ningekua rais ningekomesha foleni maana tanzania kunafoleni kila sehemu kwa mfano bank fole masaa mawili, barabarani masaa mawili, kisimani fole masaa mawili, kulipia umeme foleni masaa mawili , kwenye ATM foleni masaa mawili, huo muda ni wa uzalishaji na hapo unapotea
  ningeakikisha hii hali inakufa maana inaua nchi
  ningekuwa rais ningejiounguzia madaraka, sio kila mtu nimchague mimi na katiba mpya ningekuwa nimeshaipitisha maana hii ni ya mkoloni, imejaa kinga kwa viongozi hata kama ameamisha pesa zote benki kuu.

  ningekuwa rais kila kiongozi anatakaye beza wananchi atakua amejifukuzisha kazi siku hiyo hiyo hapo hapo.
  ningekuwa rais bomoa bomoa ingekoma maana ninge hakikisha kila mji umepangwa vizuri na maeneo ya hifadhi ya barabara na viwanja vya michazo kwa watoto vinalindwa sio mtu anavamia anakaa miaka 60 harafu unakuja kumwambia bomoa bomoa na unamlipa pesa

  ningekuwa rais ningetumia sera ya ''mwananchi ndiye mwenye mahamuzi'' na sio hii ya sasa ya hari mpya na ningetekere matakwa na wananchi ningekuwa na makundi ya kutetea wa kulinda


  source: www.lifeofmshaba.com
   
 2. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tutakuchagua 2012 baada ya kutoka Kiwete wetu
   
 3. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Te he te he! I love this! By the way hello magafu!
   
 4. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Huyu Kikwete ingefaa ajiuzuu kwa kukiri mwenyewe kuwa amekaa miaka mitano hakumaliza matatizo na atakaa mingine mitano hatamaliza... je ni kwa nini aliwapa ahadi lukiki watanzania wakati wa kampeni ili hali akijua kwamba ahadi hizo anazozitoa hatazimaliza?

  Inafaa ashtakiwe kwa Deception na misrepresantation... sijui akina Tendwa WAKO WAPI ILI WAMKUMBUSHE kwamba inafaa yale yote yalioahidia yatekelezwe maana kwa kuwaahidi watanzania ili wamchague (kama kweli walimchagua) ilikuwa ni kuweka mkataba kati ya wachaguaji na wachaguliwa na mkataba tayari umevunjwa kwa mchaguliwa kukiri hadharani kwa mchaguaji kwamba hawezi kutimiza yale waliyokubaliana wakati wa kampeni na wakati wa uchaguzi....
   
Loading...