Wana JF
Uteuzi uliofanyika kumwingiza Prof Kabudi na Bulembo bungeni, unaweza kuwa maana nyingi. Mimi naona haya:
-Prof. Kabudi alikuwa Tume ya Warioba inayotetea serikali tatu.
-Prof. Kabudi alitetea kwa nguvu zake zote na kuchukia sana pale bunge lilipoburuzwa kukataa mawazo yao
-Kabla yake kuingizwa serikalini, alichukuliwa Humphrey Pole Pole - wote watetezi wa serikali tatu.
-Rais Magufuli hakuhudhuria sherehe za Mapinduzi juzi na haieleweki anasimama wapi juu ya Muungano
-Rais magufuli alipoulizwa juu ya katiba mpya alisema, siyo kipa umbele chake kwa sasa.
Kwa hiyo:
-Uteuzi huu waweza kuwa kitanzi cha Kabudi na Polepole ili wale matapishi yao; au
-Uteuzi huu ni kifo cha Muungano kuwatumia Kabudi na Pole Pole kuua muungano.
LAKINI:
-Muungano ni kama uchi wa mama wa serikali yetu, huwezi kuuona uchi huo ukabaki na macho
-Kwa hiyo, Kabudi na Polepole wamechukuliwa kumpandisha presha Warioba.
-Kupona na kufa kwa hoja ya serikali tatu vimo mikononi mwa Kabudi na Polepole baada ya Mzee Warioba.
Kuhusu Bulembo, mawili/matatu yaweza kuwa nyuma ya uteuzi wake:
-Jumuia anayoiongoza inakufa/futwa, kwa hiyo anapozwa na kufutwa machozi
-Atapewa ukatibu wa wabunge wa CCM bungeni ili aingie Kamati Kuu kwa vile jumuia yake inayomwingiza Kamati Kuu inafutwa
-Alimtetea mteuzi wake mpaka kujidhalilisha mbele ya wenzake na anatoka kanda yenye haki ya kuteuliwa kwa sasa bila kuhojiwa.
Vijana wa kazi, mkamateni Max tena kwa kuruhusu uchochezi huu kuandika JF🙂
--Baija