Baija Bolobi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 1,093
- 1,727
Wana JF,
Uteuzi uliofanyika kumwingiza Prof. Kabudi na Bulembo bungeni, unaweza kuwa maana nyingi. Mimi naona haya:
-Prof. Kabudi alikuwa Tume ya Warioba inayotetea serikali tatu.
-Prof. Kabudi alitetea kwa nguvu zake zote na kuchukia sana pale bunge lilipoburuzwa kukataa mawazo yao
-Kabla yake kuingizwa serikalini, alichukuliwa Humphrey Pole Pole - wote watetezi wa serikali tatu.
-Rais Magufuli hakuhudhuria sherehe za Mapinduzi juzi na haieleweki anasimama wapi juu ya Muungano
-Rais Magufuli alipoulizwa juu ya katiba mpya alisema, siyo kipa umbele chake kwa sasa.
Kwa hiyo:
-Uteuzi huu waweza kuwa kitanzi cha Kabudi na Polepole ili wale matapishi yao; au
-Uteuzi huu ni kifo cha Muungano kuwatumia Kabudi na Pole Pole kuua muungano.
LAKINI:
-Muungano ni kama uchi wa mama wa serikali yetu, huwezi kuuona uchi huo ukabaki na macho
-Kwa hiyo, Kabudi na Polepole wamechukuliwa kumpandisha presha Warioba.
-Kupona na kufa kwa hoja ya serikali tatu vimo mikononi mwa Kabudi na Polepole baada ya Mzee Warioba.
Kuhusu Bulembo, mawili/matatu yaweza kuwa nyuma ya uteuzi wake:
-Jumuia anayoiongoza inakufa/futwa, kwa hiyo anapozwa na kufutwa machozi
-Atapewa ukatibu wa wabunge wa CCM bungeni ili aingie Kamati Kuu kwa vile jumuia yake inayomwingiza Kamati Kuu inafutwa
-Alimtetea mteuzi wake mpaka kujidhalilisha mbele ya wenzake na anatoka kanda yenye haki ya kuteuliwa kwa sasa bila kuhojiwa.
--Baija