Ninauliza tu jamani!

Ninauliza tu jamani!

laigwenan

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2012
Posts
325
Reaction score
80
Hivi ni halali kwa VIWANJA VYA MCHEZO INCHINI KUMILIKIWA NA CCM! ikumbukwe karibia viwanja vyote vya mpira vipo chini ya ccm japo vilijengwa na serekali enzi zile za chama kimoja na wasimamizi wakuu walikuwa ni serekali lakini sasa vimehodhiwa na CCM hebu tuvitaje kidogo,CCM KIRUMBA -MWANZA,SAMORA-IRINGA,Ali Hassan mwinyi-Tabora,Lake Tanganyika-kigoma,Namfua-Singida,Mkwakwani-Tanga,Jamuhuri_Morogoro,Jamuhuri-Dodoma,Nelson Mandela-Rukwa,Kambarage-Shinyanga,Umoja-shinyanga,Ilulu-Lindi,Ushirika-Kilimanjaro,Uhuru-Dar,Karume-mara,Mao-ze-tung-ZNZ,Amaan-ZNZ na Gombani Pemba,Swali la kujiuliza ni kwanini viwanja hivi havija taifishwa baada ya utaratibu wa chama kuongoza inchi kuachwa! hapa ninahisi CCM wanatudhihaki sana.

My take:ni bora Viwanja hivi vingekuwa chini ya Wizara ya utamaduni na michezo ili kila mtu anae hitaji avitumie kwa manufaa ya wote
 
Virudishwe kwenye halmashauri husika.

Moshi wameweza kurudisha majengo yaliyojengwa na wananchi wote halafu CCM wakajimilikisha. Hii imezekana baada ya Manispaa ya Moshi kuongozwa na CDM.

Sijui CUF wanashindwaje kurudisha uwanja wa Gombani Pemba!
 
vyote hivyo ikiwemo na yale majengo yote ya ccm ( bila kusahau ofisi ndogo lumumba ) vitarejesha wiki 1 tu baada ya uchaguzi 2015 .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom