Mimi ni kijana wa miaka 23, kwa miezi kama 7 hivi nimekuwa nikishambuliwa na chunusi na upele usoni.
Upele wenyewe ni mkubwa na nikiuminya yanatoa usaha. Nimejaribu kutumia sabuni na mafuta aina mbalimbali lakini yamekuwa yakipona alafu yajirudia tena.
Wadau ninaomba msaada ninawezaje kuondokana na tatizo hili?
RTI,
Aise pole niliwahi kushambuliwa pia kila aina ya sabuni nilitumia wapi. Vilikuja kuisha nilivyokuja Dar maana nilikuwa naishi mikoa ya baridi (Iringa na Mbeya).
Aise pole niliwahi kushambuliwa pia kila aina ya sabuni nilitumia wapi. Vilikuja kuisha nilivyokuja Dar maana nilikuwa naishi mikoa ya baridi(iringa na mbeya)
Tumia Baby Vaseline husafisha makovu, asubuhi saa moja kabla ya kuoga paka mate(kabla hujapiga mswaki) husaidia kuivisha vichunusi vizuri na pia kabla ya kulala paka mate. Chunusi usiikamue kama haijaiva. Niushauri tu waweza jaribu.