kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,635
- 7,005
Niliwahi kushangaa wakati fulani kuona mama mmoja anajiita "mfalme zumaridi" anawafuasi wengi kiasi kwamba unaweza kujiuliza jinsi akili za binadamu zilivyo dhaifu na kuna watu wanaweza kuzifanya vyovyote wanavyotaka.
Hata hivyo nikakumbuka mtu mmoja aliitwa Kibwetere jinsi alivyowarubuni watu kule Uganda hadi akauunguza moto katika hekalu lake wao wakiwa wanasubiri kuja kwa Yesu.
Kama haitoshi nikakumbuka yale makundi ya kigaidi yanayofanganya watu wa mrengo wa dini fulani kuwa yanampigania Mungu wao kwa njia ya kuchinja binadamu waliowatambua kama makafiri.
Sijui kwanini leo ninawashangaa wasomi wengi (kama kweli ni wasomi au wahitimu sijui) wanahoji tena kwa hasira na chuki eti ni kwa nini CAG anayasema haya wakati mwenda zake hayupo! Wanafikia mahali pa kusema mwenda zake amesalitiwa kisa ukweli wa kuwa ATCL inajiendesha kwa hasara.
Hivi kumbe inawezekana kuwafanya hata waliohitimu digrii kuwafanya wasiweze kufikiri vizuri?
Kweli ubinadamu ni kazi sana, ndio maana hata Mungu aliwanyooshea mikono binadamu.