Ninapoitafakari Tanzania na Watanzania chini ya utawala wa CCM

Ninapoitafakari Tanzania na Watanzania chini ya utawala wa CCM

namkweche

Member
Joined
Aug 19, 2009
Posts
42
Reaction score
5
Nilizaliwa katika awamu ya pili ya uongozi wa muasisi wa nchi yetu. Nyerere amemaliza utawala wake mwaka 1985 nikiwa na uwezo wa kubaini baya na zuri. Utawaka wa awamu ya kwanza ulikuwa wa kizalendo. Chama cha mapinduzi kilikuwa kweli ni mali ya wakulima na wafanyakazi.

Awamu ya mzee A.H. Mwinyi ilianza kugeuza mambo taratibu. Rusha iliongezeka, wakulima na wafanyakazi taratibu walitengwa na chama. Tulianza kuwaabudu wafanya biashara na kuwapa majukumu makubwa chamani. Mabadiliko ya maisha ya mtanzania yalikuwa ya mwendo wa konokono, viongozi walijilimbikizia mali kwa jinsi walivyoweza kwani walionekana kuwa juu ya sheria.

Awamu ya Mkapa, kulikuwa na mabadiliko kadhaa ya kijamii na kiuchumi, hali ya ufisadi iliongezeka, awamu hii ukiwepo ufisadi unaokihusicha chama chenyewe.

Ikaja awamu ya kaka yetu J.Kikwete. Ilikuwa awamu iliyojengwa katika matumaini makubwa, matumaini ambayo kama yangetekelezwa yangeibadili Tanzania kutoka nchi masikini kuwa nchi ya uchumi wa kati. Hata hivyo matumaini haya yaliyeyuka na kufanya watu wajute kumchagua.

Rushwa ya kitaasisi iliongezeka na wala hakuna hatua madhubuti za kisheria zilizochukuliwa.

Kwa mwendelezo huo sina imani na CCM tena na sina matumaini kuwa mgombea yeyote wa chama hicho anaweza kutuletea maendeleo ya kweli.

#NITACHAGUA MABADILIKO
 
Umesema kweli.TANU na ASP vilisimamia haki za wanyonge hadi vilipoungana na CCM kuzaliwa mwaka 1977.CCM ilikuwa chama cha mapinduzi kweli kweli na kilielekeza nguvu zake kumkomboa mwananchi hadi Nyerere alipong'atuka rasmi.Nyerere aliporudi kijijini ndipo CCM ilipowageuzia mgongo wananchi na kujivika usultani.mwananchi akageuzwa kuwa kiraka katika taifa lake!
 
Back
Top Bottom