Ninani Profesa Mbele??

Ninani Profesa Mbele??

Josephine03

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2012
Posts
752
Reaction score
302
Aliandika makala aliyoipa kichwa cha habari "Safari za JK Nje ya Nchi" 2 June 2009?

Embu isome unisaidie nisichokijua maanake hata jinsi ya kuuliza sijui

Profesa Joseph L. Mbele

Leo nimeamua kuongelea safari za Rais Kikwete, maarufu kama JK, katika nchi za nje. Suala hili linazungumzwa sana na waTanzania. Wako wanaodai kuwa JK anatumia muda mwingi mno nje ya nchi badala ya kubaki nchini na kushughulikia masuala ya nchi. Wako wanaodai kuwa JK anaenda kuomba omba *misaada. Wengine wanasema kazi ya kuzunguka nje ni ya waziri wa mambo ya nchi za nje, na kwamba kwa vile JK alizoea kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje, bado hajabadilika, hata baada ya kuwa rais. Basi, kila mtu anasema yake, nami nimeona nichangie.

Naanza kwa kukiri kuwa nchi ya nje ninayoifahamu kuliko zote ni Marekani. Nimeishi na waMarekani katika nchi yao kwa miaka mingi, nikiwafundisha na kujumuika nao kwa namna mbali mbali. Naweza kusema nawafahamu, na suala la safari za JK katika nchi za nje, naweza kuliongelea kwa kutumia mfano wa Marekani.

Rais Kikwete ameshatembelea Marekani mara kadhaa, tangu awe rais. Binafsi, naona safari zake ni za manufaa. Kwanza, waMarekani kwa ujumla hawazijui nchi za Afrika kwa majina. Sana sana wanajua tu Afrika. Kuja kwa JK daima imekuwa ni fursa nzuri ya waMarekani kuijua na kuikumbuka nchi inayoitwa Tanzania. Kwa vile JK ni mtu mkubwa, ujio wake unatangazwa vilivyo, na hivi wahudhuriaji wanakuwa wengi. *Fursa ya kuitangaza Tanzania inakuwa kubwa zaidi kuliko kama angekuja mbunge au waziri kama wanavyotaka baadhi ya Watanzania. Sio rahisi mbunge au waziri aje Marekani aweze kuwavuta watu kama anavyowavuta JK.

Watanzania wanaoishi Marekani wanayo fursa ya kuitangaza Tanzania, na wako wanaofanya hivyo, kwa kadiri ya uwezo wao. Lakini mtu kama Rais Kikwete anapokuja, suala hili linakuwa na mafanikio mara dufu. Kinachosaidia zaidi ni kuwa JK ana mvuto wa pekee kwa watu. Wamarekani walishangaa kuona alivyokuwa na uhusiano wa karibu na Rais Mstaafu Bush. Na hilo niliwahi kuelezwa pia na mzee mmoja Mmarekani, ambaye ni balozi mstaafu na mtu mashuhuri. Tayari, dalili zinaonekana kuwa JK na Rais Obama wataelewana vizuri. Kwa mtazamo wangu, ziara za JK zinatuweka waTanzania kwenye chati inayohitajika vichwani mwa watu wa huku nje.

Suala la uwezo wa JK kuitangaza Tanzania nililishuhudia alipofika katika jimbo la Minnesota, Septemba 26, 2006. JK alitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Thomas, mjini Minneapolis. Baada ya Chuo kutoa wasifu wa JK na msingi wa kumpa tuzo hiyo, JK alitoa hotuba ambamo aliwaelimisha watu wa Minnesota kuhusu hali halisi, uwezo, malengo na mahitaji ya Tanzania na Afrika. Alielezea utajiri na fursa zilizomo katika nchi yetu na bara letu. Katika kuiongelea Tanzania, alitaja rasilimali tulizo nazo, kama vile madini, ardhi ya kilimo, vivutio vya utalii, na taratibu muafaka za kuwezesha uwekezaji. Aliongelea pia hali ya kijamii na kisiasa, kuwa ni nchi ya amani, *ukifananisha na nchi zingine. Alisisitiza kuwa mazingira ya uwekezaji na ubia ni mazuri katika Tanzania na kuwa yanazidi kuboreshwa.

Hakuishia hapo, bali aliezea pia matatizo na mahitaji. Alisema kuwa pamoja na rasilimali zake, Tanzania haina uwezo wa kuziendeleza ipasavyo bila ushiriki wa wengine. Alisema kuwa Tanzania inahitaji mitaji na wawekezaji. Alisisitiza kuwa Tanzania si maskini anayehitaji kuhurumiwa na kutupiwa misaada. Inachohitaji ni washiriki katika kuufanyia kazi huu utajiri na kuleta faida kwa pande zote.

Kwa namna hii, JK alituweka Watanzania na Waafrika katika akili za WaMarekani, kwa namna tofauti na walivyozoea. Wao wamezoea kuisikia Afrika, na wengi wanadhani Afrika ni nchi ndogo, ambayo ni hoe hae kwa dhiki, njaa, maradhi na vita. JK alijenga picha tofauti miongoni mwa wali0hudhuria. Kwa yeyote anayewafahamu waMarekani, huu ni mchango mkubwa wa fikra, hasa tukizingatia kuwa vyombo vya habari viliripoti vizuri ujio wake.

Rais Kikwete alikuja na ujumbe mkubwa kutoka Tanzania, hasa wafanyabiashara. Kuja kwake na ujumbe wa wafanyabishara kulimaanisha kuwa Tanzania inataka kufanya biashara, si kuomba misaada. Ilifanyika semina kuhusu masuala ya biashara na uwekezaji Tanzania. WaTanzania wengi wanaoishi huku Minnesota walihudhuria, na walikiri *kuwa semina hii ilikuwa muhimu sana. Kwa maoni yangu, JK alitekeleza vizuri jukumu lake.

Kilichobaki ni upande wetu waTanzania. Ingekuwea bora kama *waTanzania waliohudhuria wangefanya utaratibu wa kuwaelezea wenzao ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria, ili *kuyatafakari na kuyafanyia kazi yale ambayo yalitokana na ujio wa JK. Ulihitajika utaratibu wa sisi waTanzania kuendeleza mawasiliano na waMarekani, baada ya JK kuwahamasisha. Sisi tungepaswa tuikuze ile mbegu ambayo JK alikuwa ameipanda.

Lakini waTanzania hatukujizatiti kufanya hayo. Inawezekana wako wanaoendeleza masuala aliyoanzisha Rais Kikwete, lakini sio kama jumuia. Labda wako ambao wanafuatilia, lakini hakuna taarifa. Hatuna vikao ambapo tunaelimishana na kuhamasishana. Tunakutana tu kwenye misiba au sherehe. Kama vile ilivyo Tanzania, kwenye sherehe waTanzania tunajitokeza kwa wingi. Lakini kwenye masuala ya kushirikiana katika maendeleo, ni wazi tunahitaji kujirekebisha.

Ziara ya JK ilileta msisimko miongoni mwa watu wa Minnesota, na iliripotiwa vizuri katika vyombo vya habari. Ilikuwa ni juu yetu waTanzania kutumia fursa hii iliyotengenezwa na JK ili kuendelea kuwa karibu na watu wa Minnesota, na kuwa nao bega kwa bega, kupanga mipango na mikakati ya uwekezaji, ubia, biashara, na kadhalika.

Kwa maoni yangu, wale wanaosema JK anazunguka nchi za nje kuomba omba misaada hawasemi ukweli. Kuhusu hoja kuwa kazi ya kuzunguka nje JK awaachie wengine, sina hakika kama tutapata mafanikio kama anayoyapata yeye. Ikiwa tutamleta mbunge au waziri, sina hakika ni waMarekani wangapi watavutiwa kuja kumsikiliza. Wanaosema JK akae nchini ashughulikie matatizo ya ndani, huenda wana hoja, lakini, kwa mtazamo wangu, si rahisi kutenganisha mambo ya ndani na ya nje. Pengine kwa kujishughulisha na mambo ya nje Rais *Kikwete anajenga mazingira mazuri ya kutusaidia kwa mambo ya ndani. Vile vile Tanzania ina viongozi wengi au watu wengi ambao tunawaita viongozi. Hao wanafanya kazi gani? Kwani ni lazima awepo JK kuwaelekeza watu wa wilayani au mkoani wajibu wao? Je tunamhitaji rais aje kuwahamasisha watu wazoe taka taka mitaani, au waendeshe magari kwa uangalifu? Tunao viongozi wengi, kuanzia mtaani hadi kwenye ngazi ya Taifa. Wanafanya nini, na wanashindwa nini mpaka awepo rais?

Watanzania tumezoea kukaa vijiweni na kutoa lawama kwa wengine. Nayachukulia malamiko kuhusu safari za nje za JK kwa msingi huo. Kama kila mwananchi na kiongozi angewajibika pale alipo, nchi yetu ingekuwa mbali. Lakini hii tabia ya kumlaumu rais na kumtaka awepo nchini kutuelekeza namna ya kusafisha mitaro iliyoziba ni visingizio vya waTanzania ambao wanapenda zaidi kukaa vijiweni na kukosoa kuliko kuwajibika.

Joseph L. Mbele
1520 St. Olaf Avenue
Northfield MN 55057

Phone: 507 403 9756
 
Ni mwendesha warsha ndogondogo zisizo na tija
 
Mbona maelezo yako yameja blablaaaa, Lete statistical data za mafanikio aliyoyaleta Physically, ukilinganisha na safari alizo safiri na gharama zake.Ni wapi umewaona wawekezaji wamarekani waliokuja tanzania kuwekeza kutokana na safari za kikwete?? Misaada ya wamarekani yenyewe TZ ni hivyo vyandarua tuu??? Tunataka utupe takwimu za maendeleo ya kiuchumi yaliyoletwa na hao wamarekani kwa safari za kikwete badala ya kutuambia ametunukiwa udaktari na kujulikana.Haina tija kwetu.Hivi ni yeye tuuu ndio anajua kupanda ndege kuliko maraisi wote Africa?

Tunataka takwimu za maendeleo aliyoyaleta kwa safari za US! sio kutuambia tunajulikana, than what? au kutunukiwa Udaktari then what?
 
It so painful kama proffesor atakua na ufinyu wa kufkiri na kupembua mambo!
 
Mbona maelezo yako yameja blablaaaa, Lete statistical data za mafanikio aliyoyaleta Physically, ukilinganisha na safari alizo safiri na gharama zake.Ni wapi umewaona wawekezaji wamarekani waliokuja tanzania kuwekeza kutokana na safari za kikwete?? Misaada ya wamarekani yenyewe TZ ni hivyo vyandarua tuu??? Tunataka utupe takwimu za maendeleo ya kiuchumi yaliyoletwa na hao wamarekani kwa safari za kikwete badala ya kutuambia ametunukiwa udaktari na kujulikana.Haina tija kwetu.Hivi ni yeye tuuu ndio anajua kupanda ndege kuliko maraisi wote Africa?

Tunataka takwimu za maendeleo aliyoyaleta kwa safari za US! sio kutuambia tunajulikana, than what? au kutunukiwa Udaktari then what?

Mkuu umekuja kwa jazba mpaka unanitisha na mimi
 
nimesoma between lines maelezo ya huyu jamaa nikagundua kwanza jina la uprofesa ni la utani i mean huwa anataniwa kuwa yeye ni prof. vinginevyo we need statistical data za matumizi ya rais with regards na kilichopatikana kwa hao wamarekani,vinginevyo ni yale yale ya kujenga hoja dhaifu kuutetea udhaifu.
 
Huyu ni Professa? seriously?

where is Kiranga ? lol
 
Last edited by a moderator:
nimesoma between lines maelezo ya huyu jamaa nikagundua kwanza jina la uprofesa ni la utani i mean huwa anataniwa kuwa yeye ni prof. vinginevyo we need statistical data za matumizi ya rais with regards na kilichopatikana kwa hao wamarekani,vinginevyo ni yale yale ya kujenga hoja dhaifu kuutetea udhaifu.

Ni bora unisaidie wewe maana mimi nimekosa hata jinsi yakuumba swali ili nijibiwe linalonishinda
 
Mimi nakubali kafanya safari nyingi katengeneza faida sawa sasa akae tule hiyo faida. Hamna sababu kwenda tena huko apumzike kivulini hapo magogoni ale faida basi na mishahara tulipane kama huu wa mwezi wa kumi.
Na wewe uje utusomeshe huku wenzako wengi hawajui kusoma uje uongeze nguvu. Ondoka huko kama shule huku umasaini zipo tena fulu eisii. Kule ufipa, usukumani kule kwa wazigua kule mswaki, kule ubena njoo usomeshe wenzako huku.
 
Ni prof wa chuo cha St. Olaf na ni mwandishi ana kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural differences. ni mshiriki wa mikutano ya washauri wa programu ya Associated Colleges of the Midwest (ACM) ambayo uleta wanafunzi Tanzania
 
Huyu anatafuta namna ya kujikimu kisiasa akirudi nchini baada ya kutumia Akili yake kuijenga Marekani...
Ni mganga njaa tu huyo.
 
Mbona maelezo yako yameja blablaaaa, Lete statistical data za mafanikio aliyoyaleta Physically, ukilinganisha na safari alizo safiri na gharama zake.Ni wapi umewaona wawekezaji wamarekani waliokuja tanzania kuwekeza kutokana na safari za kikwete?? Misaada ya wamarekani yenyewe TZ ni hivyo vyandarua tuu??? Tunataka utupe takwimu za maendeleo ya kiuchumi yaliyoletwa na hao wamarekani kwa safari za kikwete badala ya kutuambia ametunukiwa udaktari na kujulikana.Haina tija kwetu.Hivi ni yeye tuuu ndio anajua kupanda ndege kuliko maraisi wote Africa?

Tunataka takwimu za maendeleo aliyoyaleta kwa safari za US! sio kutuambia tunajulikana, than what? au kutunukiwa Udaktari then what?

Profesa wa ungwini facts zake ziko subjective. Anaweza kum discuss JK kama ana mdiscuss character wa kitabu akakwambia "there are no right answers, it depends on how you make the case"

Maandiko yote hamna hata figure.

If there is a case to be made for JK travels, it is not this one.
 
Huyu ni Professa? seriously?

Watu kwa kuchonga, siwawezi!

Huyu ni profesa kweli, na uprofesa wake ni juu ya "hadithi za kale"

Sasa safari za JK zimemrudisha kwenye safari za Sindbad Baharia na Safari za Gulliver

Hata kama haipatikani faida ya moja kwa moja, kunapatikana ufahari na umaarufu....

:shut-mouth:
 
Kuna vitu very simple mno kwa huyu professa vinashangaza

Je nchi zoote ambazo ni maarufu kwa wamarekani,Rais wao huwa anakwenda Marekani kutembelea?
Wamarekani wanaenda kwa mamilioni kutembelea Thailand,Jamaica,South africa,Egypt na zingine

Yeye hajui kuwa kuna nchi zinatumia mabilioni ya pesa kwa kujitangaza
mfani Singapore wanatumia zaidi ya dollar milioni 50 kila mwaka...kwa kujitangaza
sasa yeye aliambiwa na nani nchi hutangazwa na ziara za Rais?
 
Well said mkuu maana nimeshindwa hata kumdescribe maana anashusha hadhi ya Uprof kabisa au ndo anatuthibitishia ukiwa prof unakuwa outbrain
 
Watu kwa kuchonga, siwawezi!

Huyu ni profesa kweli, na uprofesa wake ni juu ya "hadithi za kale"

Sasa safari za JK zimemrudisha kwenye safari za Sindbad Baharia na Safari za Gulliver

Hata kama haipatikani faida ya moja kwa moja, kunapatikana ufahari na umaarufu....

:shut-mouth:

Gee..
yeye kwa usomi wake alipaswa kujua lengo la ziara hizi ni nini kabla ya kusema faida zake

kama lengo ni kutangaza nchi....je hivi ndo best way ya kutangaza nchi?

Wanaotangaza nchi zao wanafanya hivi?

Hawezi hata ku google top ten countries zinazospend kwenye kutangaza utalii kwa nchi zao duniani?
 
Kuna vitu very simple mno kwa huyu professa vinashangaza

Je nchi zoote ambazo ni maarufu kwa wamarekani,Rais wao huwa anakwenda Marekani kutembelea?
Wamarekani wanaenda kwa mamilioni kutembelea Thailand,Jamaica,South africa,Egypt na zingine

Yeye hajui kuwa kuna nchi zinatumia mabilioni ya pesa kwa kujitangaza
mfani Singapore wanatumia zaidi ya dollar milioni 50 kila mwaka...kwa kujitangaza
sasa yeye aliambiwa na nani nchi hutangazwa na ziara za Rais?

I wish wewe ndo ungekuwa Boss wake, maana hata hajui nini maana ya promo na marketing especialy kwenye country level. Huyu ni mtalii tu
 
Back
Top Bottom