Ninaamkiwa sana na watu,najiuliza nimeanza kuzeeka au inakuaje naamkiwa sana kila ninakopita napewa SHIKAMOO!?

Mtaani siku zote vijana wananitupia shikamoo. Takribani miezi miwili ago "tumeshemshana" viwanja jogging za weekend (mzunguko wa 12 km). Vijana wamefika finish namalizia mineral water.Tangu siku hiyo salamu zimebadilika siyo shikamoo tena - vipi kaka,vipi bro,mzee wa kazi mambo vipi?😊
 
Waungwana wa humu nawasalimu sana

Tangu nirudi kanda ya ziwa mwishoni mwa mwaka 2018 nimekutana na hali ya kuamkiwa sana na watu mabinti kwa wakaka

Kisura mi ni HB haswa nna ndevu kiasi zenye mvi kwa mbali kama zile za Mbowe alipotoka Jela kipindi kile

Mustachi Mdogo Mdogo na vindevu kiasi chini ya lips kama vile vya Ramsey Nouh wa Nollywood

Sasa tangu nirudi tena huku kanda ya ziwa hasa maeneo ninayokaa kaa sana nimekua naamkiwa sana na watu,wengine nikiwaangalia naona wamenizidi umri ila wana niamkia,kuanzia ofisini,mitaani,kwenye vyombo vya usafiri ,bar na sehemu nyingine ninazokuwepo watu wamekua wakinipa sana shikamoo

Sasa najiuliza je sura yangu ya kizee au wananionaje hadi wanipe sana shikamoo!?

Mabinti nao hawapo nyuma kuniamkia sasa sijui wanataka kuninyima nini!??

Wale wakongwe waniambia kuamkiwa sana ishara ya nini? Kiumri nina 32 years tu lakini daaa shikamoo nazopewa utadhani mbabu wa miaka 70

Nini chanzo za hizi shikamoo jamaniii??

Sent using Jamii Forums mobile app
32 halafu una vimvi? Age mate umekwisha
 
Back
Top Bottom