Nina wasiwasi na kipimo cha dna .

gagonza

JF-Expert Member
Oct 18, 2009
309
98
Ndoa zimevurugika sana,huku kwetu wanawake watatu wamefukuzwa sababu dna imesema watoto siyo wa hao jamaa, mama mmoja alikuwa na watoto watatu wote dna imesema siyo wa huyo jamaa,kama siyo mashine basi wataalamu tulionao hawawezi kuitumia vizuri.
 

sixgates

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
3,979
1,652
sikuelewi unachotaka kusema kwamba sababu imetokea huko kwenu kuna mama mwenye watoto 3 na DNA inasema sio wa huyo jamaa ndio kipimo cha kusema DNA ina hitilafu au hatuna wataalamu wazuri?..mim nlifikiri mmefanya vipimo kwingine mkafalsefy majibu yaa awali...hao ni wa huyo jamaa kwa mrengo wa kijamii but he is not a biological father.
 

kookolikoo

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
2,732
589
sikuelewi unachotaka
kusema kwamba sababu imetokea huko kwenu kuna mama mwenye watoto 3 na
DNA inasema sio wa huyo jamaa ndio kipimo cha kusema DNA ina hitilafu au
hatuna wataalamu wazuri?..mim nlifikiri mmefanya vipimo kwingine
mkafalsefy majibu yaa awali...hao ni wa huyo jamaa kwa mrengo wa kijamii
but he is not a biological father.

jamaa kabambikiwa watoto!
 

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,598
1,533
Mkuu gagonza, hebu pelekahii mada kule Habari na Hoja mchanganyiko, sio siasa.

Sasa sijui shida iko wapo, isifanye jambo kwa kutegemea majibu TU yale unayoyataka.Ukipima tegrmea mambo mawili. Sababu uliyoeleza hapo juu haitoshi kusema kuna shida katika DNA Testing.

Lakini pia, mchakato mzima wa kupima DNA unautambua, watu wanaweza kubadilisha majibu sababu ya RUSHWA.hio imetokea sana.
 
Last edited by a moderator:

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,872
4,530
Kwa Bongo lolote lawezekana. Wengine wanaweza kuwa na ujuzi wa kuitumia lakini wakahitaji rushwa na bila kutoa rushwa wakakubambikia majibu. Ni matatizo matupu kuwa na nchi yenye utamaduni wa kipumbavu na kifisadi kama yetu.
 

iseesa

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
943
212
Ndoa zimevurugika sana,huku kwetu wanawake watatu wamefukuzwa sababu dna imesema watoto siyo wa hao jamaa, mama mmoja alikuwa na watoto watatu wote dna imesema siyo wa huyo jamaa,kama siyo mashine basi wataalamu tulionao hawawezi kuitumia vizuri.

Mods hii nayo inastahili kuwepo kwwenye JUKWAA LA SIASA?
 

Lyimo

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,824
2,016
Ni ngumu kwa mtoa mada kuja na hitimisho hili. Hiki kipimo huwa ni sahihi kwa 99.99%. Hivyo inawezekana hatuna wataalamu wazuri, reagents/markers zimekuwa handled vibaya, unaweza kuta hata baadhi ya wamama watoto siyo wao (kubadilishiwa mtoto wakati wa kuzaliwa inawezekana hilo, hasa kwa hawa manesi wetu wasio na motisha wanaweza jichangana tu), pia inawezekana ni kweli pia hao wamama wamedanganya, kwani hadi kuamua kwenda kudhibitisha kwa mkemia mkuu tayari kulikua na viashiria.

Pata habari za baby switching hata dunia ya kwanza huko yanatokea. Paula Johnson News - The New York Times
 

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,611
7,788
.....unaweza kuta hata baadhi ya wamama watoto siyo wao (kubadilishiwa mtoto wakati wa kuzaliwa inawezekana hilo, hasa kwa hawa manesi wetu wasio na motisha wanaweza jichangana tu), ...
Hili nalo linawezekana sana hapa bongo. Naamini katika huko kupima DNA huwa wanaliangalia na hili. Najiuliza tu kama ikitokea wote sio mtoto wenu inakuwaje?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom