Nina wasiwasi na ajira ya Mkurugenzi Mkuu TANESCO

Oh! Hivi Dk.Magufuli alipataje habari kuhusu hujuma za wahandisi kufungulia maji ya Bwawa la Mtera ili kina cha maji kibaki chini walazimike kuzima mitambo ya kuzalisha umeme Mtera,walifanya hivyo wakiwa na lengo la kunufaisha IPTL na wafanya biashara wanao import mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL,hii kashifa sio ndogo - unless kama Mramba alitoa taarifa hizo kwenye vyombo vya dola lakini kama alishindwa kubaini hujuma zilizo kuwa zinafanywa na Wahandisi wenzake huko Mtera Dam, basi hapo tukubali kwamba kuna tatizo kubwa kwenye masuala ya uwajibikaji si bure.
Wenye chuki na wivu mpo weng, huu ni umbea haishangazi.

Docta hafanyii kazi umbea bali taarifa kamili
 
Jamani hata raisi anaweza kukosea yeye sio Mungu.
Nashauri TANESCO/BODI YA TANESCO waunde tume kuchunguza tuhuma kwa sababu pamoja na uinjinia wangu bwawa la Mtera sio kama bwawa la kufugia samaki.

Huwezi kufungua maji bila kuleta madhara kwa watu wanaoishi chini ya mto huo.
 
Amekufanya nini Mkurugenzi wa watu jamaa mpole sana huko ni kumchumia mtu dhambi nadhan haulijui shirika vizuri
 
We mtoa mada inaonekana wazi unachuki binafisi na ajira za watu maana mwenye akili timamu hawezi kurupuka kama ww na kuongea utumbo kama wako. Na kabla hujaandika huo uhozo wako jiulize kwanza uneisaidia nini tanesco ili iweze kuendeleea zaidi nadhani we ni miongoni mwa watu wanao ihujumu miundo mbinu yake ili isiendelee.
 
Jamani kwani huyu Rais wetu mbona mnatumia vibaya kwani unafikilia yeye amekuwa ni mtu wa kukurupuka kama wewe unavyo kurupuka kupost vitu usivyo vijua ili mladi na wewe ionekane umepost kitu cha maana kumbe utumbo.
 
Naona kama kuna hali ya kutakiana mabaya kama ikithibitika ana makosa basi utafanyika utaratibu kama wa TRA nadhani wengi wetu tunataka mema nchi yetu ni kila alie husika kufanya hujuma aadhibiwe.
 
hivi karibun imeskika kaul nzito ya kwamba karibu yote mabwawa yamejaa maji na hakuna tena haja ya mugao wa umeme lakin imekuwa kinyume kwan umegeuka kuwa miradi ya maboss ya shilika hili la u
mma.na tarifa zilizozagaa wamekuwa wakifungulia usiku huo umeme.

Naomba kuwasilisha

Pamoja na uinjinia wangu bwawa la Mtera sio kama bwawa la kufugia samaki.

Huwezi kufungua maji bila kuleta madhara kwa watu wanaoishi chini ya mto huo.
 
Back
Top Bottom