Nina sababu za kutoshiriki Sensa!

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,286
4,493
Serikali Haina pesa za kuboresha huduma za afya na mazingira ya Kazi na mishahara pamoja allowances kwa Drs, serikali Haina nia ya kuongezea waalimu mishahara! Sababu Haina uwezo. Mimi na familia yangu Hatushiriki sensa sababu huenda serikali Haina pesa
 
ni kweli, naona bora waiahirishe hadi tishio la malawi liishe na la ninyi mliotangaza kugomea nalo liishe
 
Huwezi kugomea kula chakula cha mchana et kwasababu hukuwa na uwezo kununua chai asubuhi. Namaanisha kama serikali hii DHAIFU imeshindwa kukuhudumia bas ipe nafas serikal ijayo 2015. Kubalini kuhesabiwa ili kiongozi anayekuja awe data kamili za kimaendeleo. Msikate tamaa, nchi ni yenu na itajengwa na sisi wenyewe hasa kwa kuyazingatia mambo muhimu ya kitaifa kama haya. Ukigoma unamkomoa nan, Jakaya? Pinda? Wasira? Ane Makinda? Jaji Werema? Nape? Au nan? Nakukumbusha tu kuwa hao wote hawatazitumia hizi takwimu za sensa 2012, kwani wao walishasema MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA, na ndo imebaki miaka mitatu. Tukubali yaishe tulikosea kuwachagua baadh ya watu katika utawala huu, hatuna budi kupanga mikakati mipya kwa serikali ijayo. TUKAHESABIWE NA TUUNDE KATIBA IMARA, TUTAFIKA TU.
 
umenena mkuu, kumbuka sensa inafanyika mara moja tu kila baada ya miaka kumi, sasa wewe ukikataa kuhesabiwa usidhani utawakomoa magamba tu bali unawakomoa hata chadema, cuf n.k mwaka 2015 kwa sababu wakichukua nchi hawawezi kufanya sensa yao na watategemea data kutokana na sensa hii
 
Chiya Chibi umeongea sahihi, ila hapo kwenye kuwachaguwa nadhani uliwachaguwa peke yako, mimi sijawahi kumpigia kura huyu Mkwele kwa chaguzi zote mbili, hata Mkapa sikuwahi kumpigia kura kwa chaguzi zote mbili. kwa kifupi nilishakuwa na aleji na Magamba tangu tuanze mfumo wa vyama vingi.
 
Back
Top Bottom