Nina Mkosi na Wake za Watu

Mtoto Wabibi

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
451
294
Nimekuwa nikipata sana wake za watu katika mahusiano kuliko wasichana ambao hawajaolewa.

Hii hali imeanza kuniogopesha sana.mara kwa mara hata tukutane na mdada iwe popote pale na nikimtongoza nakuta ni mke wa mtu na mara nyingi huwa wawazi kwangu kuwa wameolewa na hunikubali na kuendelea kuiba tu. Imefika mahali naogopa kwani huwa wanajisahau sana na kuniona kama mume halali.Na mara nyingi wanalazimisha penzi hata kwa kunihonga tu na wana wivu sana wa mapenzi kwangu(mchepuko)

Kinachonishtua ni kwamba mara nyingi nikitongoza wasichana ambao hawajaolewa hunikataa lakini nikitongoza tu mke wa mtu yani haichukui wiki nimemaliza kila kitu. Mimi ni mvivu sana wa kutongoza na kumfatilia mwanamke kwa muda mrefu .kwangu Kutongoza hadi hamu ya kula nyama inijie ndio huwa nakumbuka kumbe kuna viumbe wanaliwa. kuna wengine wanaojitongozesha kwangu lakini wengi wao ni wake za watu.

Hii ni nuksi sasa kwanini wake za watu wanipende na kunikubali sana kuliko hawa wasichana ambao hawajaolewa yani nikiwa nao ni stress tu na bahati mbaya hawanikubali nikiwatongoza na wanamapenzi ya kuigiza tu.kwahiyo nikipata hatudumu kabisa na mwishowe naangukia kwa wake za watu.

kumbuka:sijaoa na nipo ugenini kikazi na bahati nzuri sijawahi kukamatwa tu lakini nimetumia sana haya madawa.Mke wa mtu ni mtamu lakini omba usikamatwe.poleni wenye wake zenu.natambua nimeomba makofi polisi.

Nitajitoaje kwenye hii nuksi ya kupendwa na wake za watu halafu mitego ya mwanamke ni balaa sana kama akiamua tu kukuhitaji/kukupenda kutoka ni kazi. Kwanini hii nyota ninayo mimi na sio wewe...?
 
tafuta mwanamke aliyekuzidi umri na ambae hajaolewa, na pesa ipo!..
wish you luck my friend!
 
Au una vijimelea vya Umarioo kama ndivyo wasichana wadogo hutowapata kwa sababu wao pesa mbele lakini majimama watakupa sanaaa
 
kamanda wa polisi mkoa wa
Mwanza, Ahamed Msangi alimtaja
aliyeuawa katika tukio la
fumanizi kwa jina moja la Idd
(35), fundi kinyozi, mkazi wa
kijiji cha Kome wilayani Ukerewe. Alisema mtu huyo aliuawa kwa
kupigwa hadi kufa na watu wenye
hasira baada ya kutuhumiwa
kufumaniwa akifanya mapenzi na
mke wa mmoja wa mwana kijiji. Kwa taarifa zaidi nunua gazeti
lako la Mwananchi au soma
mtandaoni kupitia
source.
GAZETI LA MWANANCHI
 
Nimekuwa nikipata sana wake za watu katika mahusiano kuliko wasichana ambao hawajaolewa.

Hii hali imeanza kuniogopesha sana.mara kwa mara hata tukutane na mdada iwe popote pale na nikimtongoza nakuta ni mke wa mtu na mara nyingi huwa wawazi kwangu kuwa wameolewa na hunikubali na kuendelea kuiba tu. Imefika mahali naogopa kwani huwa wanajisahau sana na kuniona kama mume halali.Na mara nyingi wanalazimisha penzi hata kwa kunihonga tu na wana wivu sana wa mapenzi kwangu(mchepuko)

Kinachonishtua ni kwamba mara nyingi nikitongoza wasichana ambao hawajaolewa hunikataa lakini nikitongoza tu mke wa mtu yani haichukui wiki nimemaliza kila kitu. Mimi ni mvivu sana wa kutongoza na kumfatilia mwanamke kwa muda mrefu .kwangu Kutongoza hadi hamu ya kula nyama inijie ndio huwa nakumbuka kumbe kuna viumbe wanaliwa. kuna wengine wanaojitongozesha kwangu lakini wengi wao ni wake za watu.

Hii ni nuksi sasa kwanini wake za watu wanipende na kunikubali sana kuliko hawa wasichana ambao hawajaolewa yani nikiwa nao ni stress tu na bahati mbaya hawanikubali nikiwatongoza na wanamapenzi ya kuigiza tu.kwahiyo nikipata hatudumu kabisa na mwishowe naangukia kwa wake za watu.

kumbuka:sijaoa na nipo ugenini kikazi na bahati nzuri sijawahi kukamatwa tu lakini nimetumia sana haya madawa.Mke wa mtu ni mtamu lakini omba usikamatwe.poleni wenye wake zenu.natambua nimeomba makofi polisi.

Nitajitoaje kwenye hii nuksi ya kupendwa na wake za watu halafu mitego ya mwanamke ni balaa sana kama akiamua tu kukuhitaji/kukupenda kutoka ni kazi. Kwanini hii nyota ninayo mimi na sio wewe...?
Sasa kama wanakuambia ni wake za watu kwanini usiachane nao kabla hamjazini??ONYO:unachokifanya utafanywa,na wewe
 
Back
Top Bottom