Nina mil. 7 , nahitaji gari hili zinatosha kweli

ibesa mau

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
2,109
1,697
Nimeingia mtandaoni nimeona toyota ist used usd 1,188, shipping cost usd 880 , CIF 2468 . na limetembea mile 32,000 . je kwa fedha hiyo m.7 naweza kulipia tra na usafirishaji na gharama zote nyinginezo . kwa wanao fahamu wanisaidie kukokotoa gharama za tra ili nisije agiza halafu nikalitekeza tra bure. Naombeni msaada kwa wanaojua na tena nataka kujua kama japan used car iliyotembea mile hizo hazisumbui wakuu.
 
Kuna aliyenunua Toyota Carina kwa milioni 8 hapo Dar, jaribu kuulizia kama kuna anayeuza.
 
Weka kwanza 9.4m kibindoni ndio uagize gari yako mkuu, la sivyo tra watalipiga mnada kwa wewe kukosa hela ya kuligombolea, itaingia storage huko ICD kisha utalikimbia mwenyewe.
 
hiyo usd 2468 ni cif ( gharama ta kununua na kulisafirisha hadi bandarini dar) ambayo ukiiweka kwenye tshs ni kama milion 5 na nusu.

tra hapo nae mwandalie hela nyingine maana anachukua kodi kama milion 5 na nusu hivi...

na kuna vurugu za bandarini za tpa nae mwandalie kama 1m ivi..

jumla milion 12
 
Back
Top Bottom