Nina matatizo au ana matatizo? Sielewi

Nina matatizo au ana matatizo? Sielewi

Mimi huwa nachukia, mtu unamwambia ninaskia njaa, naye anakujibu hata mimi pia; au ninahisi vibaya basi na yeye anajibu hivyo. Kwanini asikuambie pole kwanza halafu ndio naye aseme shida yake. Sababu ya kumwambia ni kupata tulizo na si kuongezewa matatizo.

Sweetheart Polee sana kwa njaa..Jitahidi ule kidogo au nikuagizie kuku wa kuchoma?
 
Inawezekana wote Hamna tatizo...watu Wengine hawajalelewa kuwa na ustaarabu huo.....kuna watu unamwambia naumwa anakujibu tu 'okay' hajui kusema pole...au ugua pole...mfundishe taratibu ...
kwenye mapenzi hamna kumfundisha mtu maadili ya kuongea na mtu,kama unampenda mtu huwa lugha ya hisia inakuja automatic,kifupi ni kwamba dem ana mtu jamaa akimpigia simu ni kama anamboa.
 
Mwanaume haipendezi kulalamika hivyo, duh.

Wanawake nyinyi mkikosolewa mnakimbilia kusema mwanaume hatakiwi kulalamika. Nani kakwambia wanaume tuliumbwa na mioyo ya jiwe?
 
Sasa badala ya kumwambia mwenyewe unakuja kutuambia sisi, dah!

Sisi tutakusaidia nini sasa kumbadilisha, mwenzio yuko na mchepuko wake, wewe unasumbua sumbua.

Alikuwa hai hai ili asiulizwa huyo nani, na mkianza kuagana yatakuja mambo ya nakupenda wakati pembeni kuna mchepuko.

Ndo mapenzi ya mbali hayo.

Jamani wee~ewe mwenzio kaona hapa ndio pakutolea dukuduku langu sasa wewe mbona wamsutaa mtoto wa mwenzio hivyooo. Si bora umwambie ampe hata talaka 1(rejea) aende kwao akajifunzi au aache kumcall,nk humo ndani wapshane kama mende na hakuna hata kugusana na akiamua analala sebleni na aulizi choochote ndani na akitoka anaenda tafuta kifungua kinywa mbele ya safari,akija jioni aje ameshibaa,nguo zisipofuliwa ajifulie mwenyewe. Kiufupi awe kiimyaaa
 
natamani ningekua na moyo kama wa mkeo, nadhani ningeishi stressfree life aisee
 
Ukitolea mbali msaada utakapopewa hapa, pia jitahidi kutafuta watu wazima waliopo kwenye ndoa kwa muda mrefu, watakusaidia pia kwa mawili machache, itakusaidia sana
 
Nahitaji kupewa thamani kama mume kutoka wake!
Nikimpigia simu asiongee na mm huku akiendelea kuongea na waliokaribu nae kwakuwa Mimi huwa sifanyi hivo!

Tukimaliza kuongea tuagane vzr na siyo kunikatia simu eti kisa alikuwa amemaliza mazungumzo! Kwakuwa huwa sifanyi hivo!

Jukumu la kulinda mustakabali wa mapenzi yetu upo mikononi mwetu sote so ni jukumu la kila mmoja wetu kuzungumza na mwenzie kunapotokea mmoja anakuwa hayupo normal.
Lkn mwenzangu huyu hata kama yeye ndo kanikwaza hashughuliki kutatua tatizo badala yake ananiangalia tu na hata akimbiwa kwamba amenikwaza anakuwa mgumu kuelewa na kutoelewa kwamba hali hiyo inaniathiri na inanifanya nisimuone rafiki Yangu tena!

Hivi mlooa muda mrefu hivi ndivyo muishivyo?
Au hilo siyo tatizo? Mi linaniathiri lkn!

Hivi umewahi kujiuliza kwa nini mzazi hutokea kumwadhibu mwanae? Je nikakwambia kuwa huyo mkeo ni mtoto na amekosea kira mara utanielewa vipi?
 
Babe sio kulalamika..mimi nimpigie mtu aongee na mimi huku anaongea na wenzie usishangae nisipige tena simu...nakuwa napokea tu...na nikipokea the same nakata...tutabaki na sms tu...
Hiyo sasa ni kuzira, kwanini usimpe za uso?
 
Wanawake nyinyi mkikosolewa mnakimbilia kusema mwanaume hatakiwi kulalamika. Nani kakwambia wanaume tuliumbwa na mioyo ya jiwe?

Kwanini usiongee naye na kumwambia hupendi hiyo tabia badala ya kulalamika?
 
Nahitaji kupewa thamani kama mume kutoka wake!
Nikimpigia simu asiongee na mm huku akiendelea kuongea na waliokaribu nae kwakuwa Mimi huwa sifanyi hivo!

Tukimaliza kuongea tuagane vzr na siyo kunikatia simu eti kisa alikuwa amemaliza mazungumzo! Kwakuwa huwa sifanyi hivo!

Jukumu la kulinda mustakabali wa mapenzi yetu upo mikononi mwetu sote so ni jukumu la kila mmoja wetu kuzungumza na mwenzie kunapotokea mmoja anakuwa hayupo normal.
Lkn mwenzangu huyu hata kama yeye ndo kanikwaza hashughuliki kutatua tatizo badala yake ananiangalia tu na hata akimbiwa kwamba amenikwaza anakuwa mgumu kuelewa na kutoelewa kwamba hali hiyo inaniathiri na inanifanya nisimuone rafiki Yangu tena!

Hivi mlooa muda mrefu hivi ndivyo muishivyo?
Au hilo siyo tatizo? Mi linaniathiri lkn!

tafuta nyumba ndogo arafu kuwa kama huna time nae uone
 
Jamani wee~ewe mwenzio kaona hapa ndio pakutolea dukuduku langu sasa wewe mbona wamsutaa mtoto wa mwenzio hivyooo. Si bora umwambie ampe hata talaka 1(rejea) aende kwao akajifunzi au aache kumcall,nk humo ndani wapshane kama mende na hakuna hata kugusana na akiamua analala sebleni na aulizi choochote ndani na akitoka anaenda tafuta kifungua kinywa mbele ya safari,akija jioni aje ameshibaa,nguo zisipofuliwa ajifulie mwenyewe. Kiufupi awe kiimyaaa

JF kila kitu kinaletwa huku, hata ambacho mtu angejiuliza akapata jibu.

Mtu umepiga simu haijapokelewa unakuja kuuliza JF, "hivi ni kwa nini mke/mme wangu hajapokea simu?", au unakuta mtu hajajibiwa SMS anakuja kutuuliza, "mbona hajibu SMS? na yuko online whatsapp?".

Sasa sisi tutajuaje!
 
Dah.. Pole mkuu sio wanandoa tu. Bali hata katika mahusiano kuna watu wa hivyo. Yaan hayuko concerned na mambo yako kabisa...
 
Pole..but note..kuna kipindi wote yaani me na ke tunakuwaga ktk kipindi cha mpito yaani abnormal...sa inabidi uwe makini la sivyo utaumia cku zote za maisha yako ya ndoa
 
Back
Top Bottom