Nina maswali mengi kuhusu sarafu yetu

Nina maswali mengi kuhusu sarafu yetu

KUNGURUHAFUGIKI

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
346
Reaction score
74
Habari zenu wakuu nisaidieni mambo haya
1. Hivi PESA tunazotumia huwa zinatengenezwa nchini mwetu au nchi nyingine?

2. Na vitu gan vinashusha thamani fedha ya nchi yetu?

3. Na kama inatengenezwa Tanzania kwa nini zisitengenezwe nyingi ili nchi isiwe na madeni na kuomba msaada

4. Na bajeti inayopangwa bungeni ni fedha zinatumiwa kwa mwaka au?
 
habari zenu wakuu nisaidieni mambo hay a
1. hivi PESA tunazotumia huwa zinatengenezwa nchini mwetu au nchi nyingine?

2. na vitu gan vinashusha samani fedha ya nchi yetu?

3. Na kama inatengenezwa Tanzania kwa nini zisitengenezwe nyingi ili nchi isiwe na madeni na kuomba msaada

4. Na bajeti inayopangwa bungeni ni fedha zinatumiwa kwa mwaka au?
.....Ndugu yangu ukifuatilia mambo ya ''nji'' hii utakuwa chizi....
we tafuta ugali wako, ukipata sawaaa ukikosa sawaaa.
 
Mkuu KUNGURUHAFUGIKI

1. Pesa za nchi yetu huwa zinatengenezwa na makampuni na makampuni haya yana sifa ya kutengeneza sarafu na aina nyingine ya vitu muhimu wakiwa na sifa kuu ya kutoweza kutoa nakala yake mtaani kirahisi ndio maana ni ngumu kutengeza noti bandia isiwe na mashaka japo maamuzi ya kiasi gani kitengenezwe/kichapishwe ni ya serikali yetu.

2. Thamani ya fedha inashushwa na vingi lakini kikubwa hasa kwa nchi yetu ni kuingiza vitu vingi kutoka nje kuliko sisi tunavyouza kwenda nje hivyo kusababisha 'deficit balance of payment'

3. Pesa zinazochapishwa lazima ziendane na uhalisia, mfano serikali ikiamua ichapishe pesa nyingi, wananchi watakua na pesa nyingi sana kununua vitu vilevile ambavyo uzalishaji wake haujaongezeka hivyo wauzaji watapandisha bei na baada ya muda hutaona faida ya kuwa na pesa nyingi, mchezo wa kuchapisha ukiendelea utaenda na laki mbili kununua chungwa ambalo leo linauzwa Tshs 100-200.

4. Bungeni ni kama ulivyosema ni bajeti, bajeti ni makadirio ya mapato na matumizi na mwaka wa fedha kwa serikali unaanza 1 July-30 June hivyo ni kwa mwaka japo makadirio sio lazima yatimie, yanaweza kuzidi ama kupungua hivyo bajeti ni mipango ya shughuli utazofanya kwa mwaka na wapi utapata fedha ya kutekeleza mipango husika.

Ni matumaini yangu nimekupa mwanga..
 
Habari zenu wakuu nisaidieni mambo haya
1. Hivi PESA tunazotumia huwa zinatengenezwa nchini mwetu au nchi nyingine?

2. Na vitu gan vinashusha thamani fedha ya nchi yetu?

3. Na kama inatengenezwa Tanzania kwa nini zisitengenezwe nyingi ili nchi isiwe na madeni na kuomba msaada

4. Na bajeti inayopangwa bungeni ni fedha zinatumiwa kwa mwaka au?

mkuu PROFESSOR Lipumba njoo hapa , umshushie nondo za uchumi. juu ya hzi mambo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu KUNGURUHAFUGIKI

1. Pesa za nchi yetu huwa zinatengenezwa na makampuni na makampuni haya yana sifa ya kutengeneza sarafu na aina nyingine ya vitu muhimu wakiwa na sifa kuu ya kutoweza kutoa nakala yake mtaani kirahisi ndio maana ni ngumu kutengeza noti bandia isiwe na mashaka japo maamuzi ya kiasi gani kitengenezwe/kichapishwe ni ya serikali yetu.

2. Thamani ya fedha inashushwa na vingi lakini kikubwa hasa kwa nchi yetu ni kuingiza vitu vingi kutoka nje kuliko sisi tunavyouza kwenda nje hivyo kusababisha 'deficit balance of payment'

3. Pesa zinazochapishwa lazima ziendane na uhalisia, mfano serikali ikiamua ichapishe pesa nyingi, wananchi watakua na pesa nyingi sana kununua vitu vilevile ambavyo uzalishaji wake haujaongezeka hivyo wauzaji watapandisha bei na baada ya muda hutaona faida ya kuwa na pesa nyingi, mchezo wa kuchapisha ukiendelea utaenda na laki mbili kununua chungwa ambalo leo linauzwa Tshs 100-200.

4. Bungeni ni kama ulivyosema ni bajeti, bajeti ni makadirio ya mapato na matumizi na mwaka wa fedha kwa serikali unaanza 1 July-30 June hivyo ni kwa mwaka japo makadirio sio lazima yatimie, yanaweza kuzidi ama kupungua hivyo bajeti ni mipango ya shughuli utazofanya kwa mwaka na wapi utapata fedha ya kutekeleza mipango husika.

Ni matumaini yangu nimekupa mwanga..

ya mkuu umenifungua hapo
 
na vipi kuhusu MAKAMU wa raisi, waziri mkuu na raisi wanalipwaje mshahara
 
Mkuu Casuist....hayo makampuni ambayo yanatengeneza pesa..yanalipwa nn....au in terms of what!??
 
1. Pesa hutengenezwa na makampuni ya kutengeneza pesa. Pesa ni bidhaa kama zilivyo bidhaa zingine kwa maana hiyo nchi inapohitaji kutengeneza pesa zake huitisha zabuni na kampuni yenye kushinda hupewa.
2 Pamoja na sbb zilizosemwa rushwa/ufisadi huchangia kushuka fedha thamani. Lakini pia kushamili kwa biashara haramu huongeza wingi wa hela kwenye mzunguko hali ambayo huchangia kushuka kwa thamani ya pesa.
3. Kwenye uchumi kuna "dhana inaitwa mahitaji na uzalishaji". Kwa maana hiyo mahitaji yanatakiwa yaendane na uzalishaji. Kimoja kikizidi basi mushkeli hutokea. Ndio maana huwezi kutengeneza hela kuzidi mahitaji.
4. Bajeti ya serikali kwa tafsiri lahisi ni mpango wa serikali wa mwaka mmoja wenye kuonyesha utaratibu mzima wa mapato (vyanzo vya pesa) na matumizi yake. Pesa hizi zinatakiwa zipatikane na kutumika ndani ya mwaka mmoja.
Makampuni haya hulipwa kwa kutoa huduma hii.
 
Nashukuru sana mtoa post,kwa namna moja maswali yangu yaliyo nitatza kwa miaka 20, sasa yamejibiwa ,lakini swali moja bado,je kwanini nchi idaiwe madeni ya ndani mfano selikari unakuta inadaiwa na NSSF,LAPF,GEF,PSPF,WAZABUNI,NK.KWanini isichape fedha nyingi na kuwalipa wadeni wake?
 
jamaa kakujibu vizuri kakwambia serikali huchapisha pesa kulingana na uzalishaji na mahitaji yake... so haiwezi kuchapisha pesa nyingi kwasababu tu ilipe madeni, tusije tukawa kama zimbabwe, milioni kumi unanunulia flat screen imeisha...
 
Mkuu Casuist....hayo makampuni ambayo yanatengeneza pesa..yanalipwa nn....au in terms of what!??

Nijuavyo yanalipwa pesa na kwa kuwa yapo ughaibuni yatakuwa yanalipwa kwa pesa ya kigeni, unaweza ukajiuliza kama wanatengeneza fedha kwa nini yasijipigie copy nyingi nyuma ya pazia. Makampuni haya yanaendeshwa kwa sheria na reputation kwao ni kitu muhimu sana pia kuzalisha pesa nje ya mfumo itakupa kazi tena ya kuitakatisha. Kwa baadhi ya nchi kama Marekani mfumo wote mpaka pesa inakamilika ni chini ya usimamizi wa idara zinazomilikiwa na serikali.
 
Mkuu KUNGURUHAFUGIKI

1. Pesa za nchi yetu huwa zinatengenezwa na makampuni na makampuni haya yana sifa ya kutengeneza sarafu na aina nyingine ya vitu muhimu wakiwa na sifa kuu ya kutoweza kutoa nakala yake mtaani kirahisi ndio maana ni ngumu kutengeza noti bandia isiwe na mashaka japo maamuzi ya kiasi gani kitengenezwe/kichapishwe ni ya serikali yetu.

2. Thamani ya fedha inashushwa na vingi lakini kikubwa hasa kwa nchi yetu ni kuingiza vitu vingi kutoka nje kuliko sisi tunavyouza kwenda nje hivyo kusababisha 'deficit balance of payment'

3. Pesa zinazochapishwa lazima ziendane na uhalisia, mfano serikali ikiamua ichapishe pesa nyingi, wananchi watakua na pesa nyingi sana kununua vitu vilevile ambavyo uzalishaji wake haujaongezeka hivyo wauzaji watapandisha bei na baada ya muda hutaona faida ya kuwa na pesa nyingi, mchezo wa kuchapisha ukiendelea utaenda na laki mbili kununua chungwa ambalo leo linauzwa Tshs 100-200.

4. Bungeni ni kama ulivyosema ni bajeti, bajeti ni makadirio ya mapato na matumizi na mwaka wa fedha kwa serikali unaanza 1 July-30 June hivyo ni kwa mwaka japo makadirio sio lazima yatimie, yanaweza kuzidi ama kupungua hivyo bajeti ni mipango ya shughuli utazofanya kwa mwaka na wapi utapata fedha ya kutekeleza mipango husika.

Ni matumaini yangu nimekupa mwanga..

Mkuu naomba unitoe matongotongo kwenye kipengele cha pili,ikiwa uingizaji wa bidhaa nyingi nchini husababisha kushuka kwa thamani ya pesa yetu,Sasa kwanini Kanchi km Burundi wanaotutegemea kwa kila kitu Pesa yao ipo juu kuliko yetu?,halikadhalika Rwanda huko ndo usiseme.Fafanua mkuu!.
 
Nashukuru sana mtoa post,kwa namna moja maswali yangu yaliyo nitatza kwa miaka 20, sasa yamejibiwa ,lakini swali moja bado,je kwanini nchi idaiwe madeni ya ndani mfano selikari unakuta inadaiwa na NSSF,LAPF,GEF,PSPF,WAZABUNI,NK.KWanini isichape fedha nyingi na kuwalipa wadeni wake?

Zimbabwe ilifanya mchezo huo, kilichowatokea nahisi umeshawahi kukisikia na mara ya mwisho nilisikia wanatumia dola ya Marekani kama pesa yao maana pesa ya Zimbabwe ilishuka mpaka ikawa haiwezi kutumika tena.

Mfano rahisi wa kuchapa fedha ni huu, kiwanda cha chumvi Tanzania kinazalisha chumvi kilo 10 ambayo watanzania 10 pekee wanauwezo wa kununua kilo moja kila mmoja kwa Tshs 1000. Serikali ikachapisha fedha na vipato vya wahusika vikaongezeka maradufu, kitachotokea wenye uwezo wa kununua chumvi wataongezeka na waliokuwa wanajibana kununua kilo moja watataka mbili. Kiwanda ni mfanyabiashara na ataona opportunity ya kuongeza bei kwa sababu kwa sasa kilo zake kumi ambazo uzalishaji wake haujaongezeka zitakuwa zinagombaniwa na watu wengi ambao kwa kuwa wana pesa wako radhi kulipa zaidi ili wapewe wao kwanza hivyo muuzaji ataongeza bei na pesa zilizochapwa na serikali zitakuwa hazina faida zaidi ya kuongeza bei za vitu na kuwaathiri sana ambao mzunguko huo haujawapitia.
 
Back
Top Bottom