Nina maswali kadhaa hapa

Nina maswali kadhaa hapa

Kuna higher consiosness ambayo ni Chanzo cha uhai na uumbaji wote,hakuna kitu kimetokea kwa bahati mbaya aka boom bang theory.

The Real Source(Chanzo Halisi) ni kimoja tu na hana mwanzo wala mwisho ni eternity.
Hii ni logical fallacy ya special pleading.

Unasema "Hakuna kitu kimetokea kwa bahati mbaya" inakuwaje hicho "chanzo halisi" kitokee chenyewe tu, kwa bahati mbaya?

Hicho "chanzo halisi" kabla ya kutokea kilikuwa wapi?

Huko kilikokuwa kulitoka wapi?

Chanzo cha "chanzo halisi" ni nini?
 
Moja ya maswali tata yanayoonyesha Dunia na vitu vyake havikutokea bila sababu . Lazima kuna aliyeweka mifumo yote.

Mimi huwa naangalia mwili wangu ulivyo tata naelewa kwamba si rahisi kujitokeza tu.

1. Kwanini kuvurugwa kwa pingili moja ya uti wa mgongo iharibu mfumo wangu wote wa kutembea au kusogeza mwili wangu ?

2. Kwanini kwenye goti hakuna mfupa wote unaounganisha upande wa chini na juu lakini ninaweza kusimama wima?
3. Mechanism ya mfumo wa hewa na chakula. Kwanini uko vile? Ni nani alifanya kusiwe na mwingiliano kiasi kwamba chakula au kiminika kikipa kwenye koo la hewa mfumo wa mwili unakitema kwa kupaliwa?

4. Ni nani aliye install thermostatic mechanism kwenye mfumo wa tumbo kiasi kwamba ukinywa kitu cha moto utumbo au tumbo haviungui au kugandishwa na kinywaji cha baridi?

5. Nani aliweka chakula kitengeneze virutubisho mwilini na kisha kitoke kama kinyesi? Au umuhimu wa maji mwilini kisha kuwa mkojo?

Maswali ni mengi ingawa mengine yanajibiwa na science lakini mwishowe lazima tuamini kuwa kuna master mind wa vitu vyote
Kusema kwamba lazima awepo aliyeweka mifumo yote ya Dunia. Halafu hapohapo unalazimisha huyo aliyeweka mifumo hiyo asiwe na chanzo, nikufanya logical fallacy inaitwa special pleading.

Yani unataka Dunia iwe na chanzo, Halafu chanzo cha dunia kisiwe na chanzo. Kwamba chanzo hicho kiwe kilitokea tu, from nowhere.

Special Pleading Fallacy

Special Pleading is a fallacy in which a person applies standards, principles, rules, etc. to an opposing position whilst expecting their own position to be exempt from the same rules without adequate justification for the exemption. providing.

Ndicho ulichokifanya wewe.
 
1. Kwanini ulimwengu unaonekana umetengenezwa mahsusi kwaajili ya kuishi?
  • Constants za fizikia kama gravity, strong force, proton mass n.k. ziko sahihi mno.
  • Kwa nini kila kitu kiko "timing" ya kutosha kutuwezesha kuishi?
Kwanza ulimwengu haujatengenezwa. Hakuna mtu yeyote mwenye uthibitisho kwamba ulimwengu ulitengenezwa. Zilizopo ni theories na imani tu, Zisizokuwa na uthibitisho wala ushahidi wa uhakika.
2. Iwapo ubongo ni kemikali tu, kwanini unafikiri unapaswa kuiamini akili yako
Kuamini unaweza kuamini hata uongo. Si kwamba kila ukiaminicho ni kweli. Kinaweza kuwa uongo pia.

Kwa hiyo huwezi kuamini akili yako kwa asilimia mia. Maana akili yenyewe hufika sehemu na kuleta matokeo na majibu ya uongo.

Ndio maana licha ya kuwa binadamu ana akili, lazima afanye utafiti, udadisi na uchunguzi ili kuhakiki na kuthibitisha kile akili ikiaminicho ni ukweli au ni uongo.

Huwezi kuamini akili tu, hivihivi bila uhakiki.

Hivyo hupaswi kuiamini akili yako tu, hivihivi bila uhakiki na uthibitisho.
- Kama mawazo ni matokeo ya michanganyiko ya kemikali, si unaweza kukosea bila sababu?
- unajuaje fikra zako ni za kuaminika?
Fikra si za kuaminika, ndio maana licha ya kuwa tuna fikra, tunahitaji kufanya utafiti, kuchunguza hizi fikra zetu kama ni za ukweli au ni za uongo.
3. Uwepo wa sheria unatokana na nini kama hakuna sheria - Muweka?
Sheria tumeziweka sisi wenyewe binadamu ili ziweze kutuongoza kwa pamoja.

Maana bila sheria kila mtu ana namna yake ya kuishi maisha ambayo inaweza kuleta mgongano.

Bila sheria, mtu angeweza kuamua kubaka tu, Halafu akaona ni sawa tu kwa fikra zake. Au mwingine angeamua kuua wengine bila sababu yoyote kwa kuamua tu. Na kwa vile sheria hamna akaona yupo sawa tu.
• Kama kuna laws of nature, kuna chanzo chake?
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na chanzo, Hata chanzo cha kila kitu kitahitaji kuwa na chanzo chake kingine.

Kwa hivyo kutakuwa na "msururu" mrefu wa vyanzo vingi visivyo na mwisho.

Ulimwengu hauna chanzo. Ulimwengu ni self-existing. Hauhitaji chanzo.

Ukiweka ulazima wa chanzo, kila kitu kitahitaji kuwa na chanzo, Hata chanzo chenyewe lazima kiwe na chanzo chake kingine na kingine na kingine na kingine. Pasipo kukoma.
• Seria zinawezaje kuwepo bia akili ya kuzitunga?
Sheria zimetungwa na binadamu.

Akili ipo kwa binadamu.

Ndio maana sheria zikatungwa kwa akili za wanadamu.
4. Je sayansi inaweza elezea kila kitu?
Hapana sayansi, Haiwezi kuelezea kila kitu.

Yani vitu tunavyo vijua ni vichache sana. Kuna vitu vingi sana katika universe hatuvijui.

Tusivyo vijua ni vingi sana kuliko tunavyo vijua.

Hatuwezi kujua tusivyo vijua, ila tuna endelea kupunguza tusivyo vijua kwa utafiti, udadisi, uchunguzi na majaribio zaidi.

we cannot solve the ultimate mysteries of nature because we ourselves are the part of mystery we are trying to solve.
-Kuna hisia, maadili, uzuri, namba, mantiki... vitu ambavyo si vya kimwili.
-Je, sayansi inaweza kufafanua vyote?
Hapana.
5. Kwanini binadamu wote wanahisi kuna kiwango cha haki?

  • kila mtu hupinga dhula, hata wanyang’anyi.
  • Je hisia ya haki na udhalimu inatoka wapi?
Hakuna binadamu yeyote apendae kufanyiwa ubaya au dhulma.

Hiyo ni asili ya kila binadamu.

Wala haitoki popote pale. Kwa sababu tayari ipo ndani ya kila binadamu.
6. Kwanini tunashauku ya mambo ya kiroho
  • Historia nzima binadamu amekuwa akiabudu au kuamini nguvu ya juu.
  • kwanini hamu hii IPO ndani ya binadamu?
Baada ya binadamu kujiuliza maswali mengi ambayo maswali mengine, walikosa majibu.

Wahuni wachache wakaja na idea ya Mungu. Baada ya akili zao kuchoka kufikiri wakaunda dhana ya Mungu.

Yani kila walichoshindwa kukipatia majawabu, wanasema ni Mungu.

Ndo dini zikaanzia hapohapo.

ila kiuhalisia, Mungu hayupo na roho haipo.

Mambo ya kiroho ni illusions tu.
7. Kwanini mwanafalsafa mkubwa kama
Einstein, Newton, Galileo aliamini kuwa kuna akili nyuma ya ulimwengu?
Kila mtu anaweza kuamini chochote apendacho lakini ili hicho kinacho aminiwa kiwe ni "ukweli" lazima pafanyike utafiti utakao leta uthibitisho wenye uhakika.

Kwa hiyo Albert Einstein au huyo jamaa Galileo "kuamini tu" kuna akili nyuma ya ulimwengu HAKUFANYI kuwapo akili nyuma ya ulimwengu.

Lazima uthibitisho uwepo. Sio kuamini tu, bila uthibitisho.
-Je, hawa walishindwa kufikiri?
_ Au waliona kitu kingine cha ndani?

8. Kwanini atheist aamini kitu kisichoonekana ( electrons, gravity)
Lakini akatae Mungu kwasababu haonekani?
Gravity na electrons sio vitu vya kuaminiwa kiimani ni vitu ambavyo vipo na vinathibitishika vipo kisayansi.

Huyo Mungu hayupo na wala huwezi kuthibitisha yupo.

Hakuna uthibitisho wowote ule, kwamba kuna Mungu. Ni imani uchwara tu, zisizo na uthibitisho.

Hakuna Mungu.

Mungu hajawahi kuwepo na hayupo.

Ukibisha thibitisha Mungu yupo kwa uhakika kabisa sio kwa imani.
-Electrons hazionekani kwa macho, tunaziamini kwa madhara yake.
-Mungu pia huaminiwa kwa matokeo yake kwenye maisha
-TOFAUTI IKO WAPI?
Kwanza thibitisha Mungu yupo, Kabla ya kusema unaamini matokeo.

UTA AMINIJE MATOKEO YA KITU AMBACHO HUNA UHAKIKA KAMA KIPO KWELI?

Unathibitishaje hayo matokeo ni Mungu na si kitu kingine?
9. Bila Mungu, kuna tofauti gani ya ki objective kati ya mema na mabaya?

  • kama hakuna standard ya juu, mema na mabaya yanakuwa mawazo tu?
  • Je ubakaji, mauaji, udanganyifu ni mabaya au tunadhania ni mabaya tu?

10. Kwanini binadamu wana dhamira
(Conscience)?

  • Nini kinakufanya ujisikie vibaya pale ukifanya kosa?
  • Evolution pekee inaweza elezea hilo?

11. Je upendo unaweza kuwa kemikali tu?

  • Unapompenda mtu, ni sumu ya dopamine tu?
  • Hiyo inatosha kuelezea kila kitu?
Mungu hayupo na hajawahi kuwepo.

secretarybird
 
1. Kukosekana kwa ushahidi kamili hakumaanishi uthibitisho wa kinyume. Kunamaanisha bado ni eneo la mjadala kati ya sayansi, falsafa na imani.

3.
Ni kweli kwamba sheria za kijamii huandikwa na binadamu ili kuongoza maisha ya pamoja. Hilo halipingwi.

PLakini swali la msingi si nani aliandika sheria, bali ni kwa nini sheria fulani zinachukuliwa kuwa sahihi na nyingine si sahihi.

Sheria zinaweza kuandikwa na binadamu, lakini haki na uovu haviandikwi kwa kura ya maoni.
 
Kwanza ulimwengu haujatengenezwa. Hakuna mtu yeyote mwenye uthibitisho kwamba ulimwengu ulitengenezwa. Zilizopo ni theories na imani tu, Zisizokuwa na uthibitisho wala ushahidi wa uhakika.

Kuamini unaweza kuamini hata uongo. Si kwamba kila ukiaminicho ni kweli. Kinaweza kuwa uongo pia.

Kwa hiyo huwezi kuamini akili yako kwa asilimia mia. Maana akili yenyewe hufika sehemu na kuleta matokeo na majibu ya uongo.

Ndio maana licha ya kuwa binadamu ana akili, lazima afanye utafiti, udadisi na uchunguzi ili kuhakiki na kuthibitisha kile akili ikiaminicho ni ukweli au ni uongo.

Huwezi kuamini akili tu, hivihivi bila uhakiki.

Hivyo hupaswi kuiamini akili yako tu, hivihivi bila uhakiki na uthibitisho.

Fikra si za kuaminika, ndio maana licha ya kuwa tuna fikra, tunahitaji kufanya utafiti, kuchunguza hizi fikra zetu kama ni za ukweli au ni za uongo.

Sheria tumeziweka sisi wenyewe binadamu ili ziweze kutuongoza kwa pamoja.

Maana bila sheria kila mtu ana namna yake ya kuishi maisha ambayo inaweza kuleta mgongano.

Bila sheria, mtu angeweza kuamua kubaka tu, Halafu akaona ni sawa tu kwa fikra zake. Au mwingine angeamua kuua wengine bila sababu yoyote kwa kuamua tu. Na kwa vile sheria hamna akaona yupo sawa tu.

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na chanzo, Hata chanzo cha kila kitu kitahitaji kuwa na chanzo chake kingine.

Kwa hivyo kutakuwa na "msururu" mrefu wa vyanzo vingi visivyo na mwisho.

Ulimwengu hauna chanzo. Ulimwengu ni self-existing. Hauhitaji chanzo.

Ukiweka ulazima wa chanzo, kila kitu kitahitaji kuwa na chanzo, Hata chanzo chenyewe lazima kiwe na chanzo chake kingine na kingine na kingine na kingine. Pasipo kukoma.

Sheria zimetungwa na binadamu.

Akili ipo kwa binadamu.

Ndio maana sheria zikatungwa kwa akili za wanadamu.

Hapana sayansi, Haiwezi kuelezea kila kitu.

Yani vitu tunavyo vijua ni vichache sana. Kuna vitu vingi sana katika universe hatuvijui.

Tusivyo vijua ni vingi sana kuliko tunavyo vijua.

Hatuwezi kujua tusivyo vijua, ila tuna endelea kupunguza tusivyo vijua kwa utafiti, udadisi, uchunguzi na majaribio zaidi.

we cannot solve the ultimate mysteries of nature because we ourselves are the part of mystery we are trying to solve.

Hapana.

Hakuna binadamu yeyote apendae kufanyiwa ubaya au dhulma.

Hiyo ni asili ya kila binadamu.

Wala haitoki popote pale. Kwa sababu tayari ipo ndani ya kila binadamu.

Baada ya binadamu kujiuliza maswali mengi ambayo maswali mengine, walikosa majibu.

Wahuni wachache wakaja na idea ya Mungu. Baada ya akili zao kuchoka kufikiri wakaunda dhana ya Mungu.

Yani kila walichoshindwa kukipatia majawabu, wanasema ni Mungu.

Ndo dini zikaanzia hapohapo.

ila kiuhalisia, Mungu hayupo na roho haipo.

Mambo ya kiroho ni illusions tu.

Kila mtu anaweza kuamini chochote apendacho lakini ili hicho kinacho aminiwa kiwe ni "ukweli" lazima pafanyike utafiti utakao leta uthibitisho wenye uhakika.

Kwa hiyo Albert Einstein au huyo jamaa Galileo "kuamini tu" kuna akili nyuma ya ulimwengu HAKUFANYI kuwapo akili nyuma ya ulimwengu.

Lazima uthibitisho uwepo. Sio kuamini tu, bila uthibitisho.

Gravity na electrons sio vitu vya kuaminiwa kiimani ni vitu ambavyo vipo na vinathibitishika vipo kisayansi.

Huyo Mungu hayupo na wala huwezi kuthibitisha yupo.

Hakuna uthibitisho wowote ule, kwamba kuna Mungu. Ni imani uchwara tu, zisizo na uthibitisho.

Hakuna Mungu.

Mungu hajawahi kuwepo na hayupo.

Ukibisha thibitisha Mungu yupo kwa uhakika kabisa sio kwa imani.

Kwanza thibitisha Mungu yupo, Kabla ya kusema unaamini matokeo.

UTA AMINIJE MATOKEA YA KITU AMBACHO HUNA UHAKIKA KAMA KIPO KWELI?

Unathibitishaje hayo matokeo ni Mungu na si kitu kingine?

Mungu hayupo na hajawahi kuwepo.

secretarybird
Mkuu umenena vizuri sana, na hii ndiyo sababu huwa naku-tag au wakati mwingine nafuatilia maandiko yako humu.

Shukrani sana 🙏.

Scott junior
 
8.
  • Sayansi inaweza kueleza gravity inafanyaje kazi, lakini
    haiwezi kujibu kwa nini sheria hizo zipo kabisa
  • Inaweza kueleza electrons zinavyotenda, lakini
    haiwezi kueleza kwa nini kuna kitu badala ya hakuna kitu
 
Kauli “Mungu hayupo na hajawahi kuwepo” ni dai la uhakika, lakini halina uthibitisho wa uhakika pia.

Kwa hiyo nalo ni msimamo wa imani ya kifalsafa, si hitimisho la kisayansi.

Kama ambavyo huwezi kuthibitisha Mungu yupo kwa maabara,

vivyo hivyo huwezi kuthibitisha kwa uhakika kwamba hayupo.
 
Hakuna binadamu yeyote apendae kufanyiwa ubaya au dhulma.

Hiyo ni asili ya kila binadamu.

Wala haitoki popote pale. Kwa sababu tayari ipo ndani ya kila binadamu.

KWANINI ASILI IWE NI YA LAZIMA KWA KILA BINADAMU?
 
1. Mazingira wezeshi kwa ajili ya viumbe hai ni adimu sana ulimwenguni. Sayari yetu pekee ndo imeonekana kuhifadhi viumbe hai kati ya nyingi zinazochunguzwa na wanasayansi.

2. Kwasababu ina uwezo wa kuchambua jambo mpaka kufikia suluhu bora. Ina uwezo wa KUDADISI.

3. Unatokana na jamii. Sio binadamu tu, viumbe wote wanaoishi kijamii huishi kiutaratibu.

4. Hapana.

5. Inatokana na maadili ambayo pia yanatokana na ujumuikaji wetu.

6. Tunayofahamu kuhusu ulimwengu ni machache kuliko tusiyoyafahamu. Tunatafuta majibu kwa namna mbalimbali.

7. Ni jinsi walivyoamua kuifafanua dunia/maisha(worldview). Malezi, makundi na mapito mbalimbali huchangia.

8. Mambo yaliyo bayana na yawezayo kuthibitishwa kiwepesi kama mifano uliyotoa hayaaminiwi yanajulikana. Mambo yasiyo bayana kama miungu, mapepo, na vibwengo ndo huaminiwa.

9. Tofauti itakuwepo kimapokeo(subjective) kulingana na malezi, tamaduni, na taratibu za jamii yako.

10. Maadili. Kadri binadamu alivyozidi kubadilika kiakili, alitengeneza taratibu bora za kujumuika na kusaidiana na wenzake ili aweze kutawala mazingira zaidi na kuongezeka bila tabu.

11. Upendo ni suala la kibaiolojia na kimaadili pia. Ipo wazi.
 
1. Kukosekana kwa ushahidi kamili hakumaanishi uthibitisho wa kinyume. Kunamaanisha bado ni eneo la mjadala kati ya sayansi, falsafa na imani.
Ukisema Mungu yupo, ina maana tayari unajua yupo. Sasa thibitisha ulijuaje Mungu yupo?

Ukidai kitu fulani kipo, ina maana ulishawahi kukiona ukajua kipo.

Sasa, thibitisha huyo Mungu yupoje?

Ulijuaje na unathibitishaje huyo Mungu yupo kweli na si imani za kusadikika tu?
3.
Ni kweli kwamba sheria za kijamii huandikwa na binadamu ili kuongoza maisha ya pamoja. Hilo halipingwi.

PLakini swali la msingi si nani aliandika sheria, bali ni kwa nini sheria fulani zinachukuliwa kuwa sahihi na nyingine si sahihi.
Sheria zote ziliandikwa na binadamu.

Na binadamu tuna mapungufu yetu.

Ndio maana sheria zingine hazina "usahihi" kwa sababu zilitungwa na binadamu wenye mapungufu.

Ndio maana muda mwingine sheria hubadilishwa, ili ziwe sahihi.
Sheria zinaweza kuandikwa na binadamu, lakini haki na uovu haviandikwi kwa kura ya maoni.
Asili ilivyokaa ukiwa mnyonge na lege lege utaonewa na kukosa haki.

Ndio maana haki haiwezi kupatikana kwa asilimia mia. Kwa sababu asili haipo hivyo.
 
8.
  • Sayansi inaweza kueleza gravity inafanyaje kazi, lakini
    haiwezi kujibu kwa nini sheria hizo zipo kabisa
Ndio maana nilikwambia, Tusivyo vijua ni vingi sana kuliko tunavyo vijua.

Hatuwezi kujua tusivyo vijua, ila tuna endelea kupunguza tusivyo vijua kwa utafiti, udadisi, uchunguzi na majaribio zaidi.
  • Inaweza kueleza electrons zinavyotenda, lakini
    haiwezi kueleza kwa nini kuna kitu badala ya hakuna kitu
Kitu lazima kiwepo, ndio kiweze kuelezewa kipoje na kuthibitishwa.

Kama kitu hakipo, hakielezeki na hakithibitishiki kwa namna yoyote ile.

Huwezi kuthibitisha kisicho kuwepo. Kwa sababu hakipo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika kipo.
 
Kauli “Mungu hayupo na hajawahi kuwepo” ni dai la uhakika, lakini halina uthibitisho wa uhakika pia.
Madai ya kwamba "Mungu yupo" yalianzia kwenu nyie waamini Mungu. Sio kwetu sisi wakana Mungu.

Madai ya kwamba "Kuna Mungu" niya kwenu nyie Theists. Sio madai yetu sisi Atheists.

Sisi Atheists tunapinga madai yenu ya kwamba "Mungu yupo" kwa kukanusha kusema "Mungu hayupo"

Kwa hivyo ninyi Theists ndio mnapaswa kuthibitisha madai yenu ya huyo Mungu.

Ukishindwa kuthibitisha Mungu yupo, ina maana madai yako ni ya UONGO na huyo Mungu unayedai yupo, Hayupo.

Anything asserted without evidence can be dismissed without evidence.
Kwa hiyo nalo ni msimamo wa imani ya kifalsafa, si hitimisho la kisayansi.
Kwanza Falsafa inamtaka mtu anayedai kitu kipo, ndio atoe uthibitisho.

Sio yule ambaye anasema hakipo. Wewe unayesema kipo, ndio unapaswa kutoa uthibitisho.
Kama ambavyo huwezi kuthibitisha Mungu yupo kwa maabara,

vivyo hivyo huwezi kuthibitisha kwa uhakika kwamba hayupo.
Kama huwezi kuthibitisha Mungu yupo ni kwamba hayupo.

Sasa wewe huwezi kuthibitisha Mungu yupo, Halafu hapohapo unakataa hayupo. Huoni kwamba unaji contradict mwenyewe?

Burden of proof (law) - Wikipedia Burden of proof (law) - Wikipedia
 
Hakuna binadamu yeyote apendae kufanyiwa ubaya au dhulma.

Hiyo ni asili ya kila binadamu.

Wala haitoki popote pale. Kwa sababu tayari ipo ndani ya kila binadamu.

KWANINI ASILI IWE NI YA LAZIMA KWA KILA BINADAMU?
Ndivyo tulivyo ikuta kwa kila binadamu.

Labda tufanye uchunguzi wa kina zaidi kuichunguza tena hiyo asili ndani yetu.

We cannot solve the ultimate mysteries of nature because we ourselves are the part of mystery we are trying to solve.
 
MFANO
1. Binadamu ilikuwaje tukawepo?
Hakuna ajuaye.

Tumejikuta tayari tupo ulimwengu bila kujua ilikuwaje kuwaje.

Tunachojua ni kwamba tunazaliana wenyewe kwa wenyewe.

Kujua Ilikuwaje kuwaje hadi tunazaliana, Nobody knows.

Hatuwezi kujua tusivyo vijua ila tuna endelea kupunguza tusivyo vijua kwa utafiti, udadisi na uchunguzi.
2. Damu imeundwa na nini?
Hili ni swali la kibaiolojia zaidi.

Biology imeelezea vizuri.

Google utapata majibu.

Nadhani hata secondary ulifundishwa suala la damu na mzunguko wake mwilini.
3. Uhai ni nini na umeanzia wapi?
We are self-existing.

Uhai unatoka kwa kiumbe hai.

Uhai umeanzia na unaanzia kwa kiumbe hai.

Hata wewe ulianzia kwa wazazi wako, Baba na Mama yako.

Kila kiumbe kilianzia na kinaanzia kwa wazazi wake.
 
Back
Top Bottom