Mpaka ulipofikia elimu yako inakusaidia nini kimaisha? Kusoma tuu kama kasuku hutaki kufanya kazi na kama kazi hakuna kwani hizo pesa za PHD usitafute frame?Nilimaliza Darasa la saba, nikafeli - nikarudia shule nyingine nikapita.
Nikaenda Secondary, form four nikapata div IV ya point 26 nikachaguliwa chuo cha ualimu wa primary- nikagoma kwenda. nikaja DSM kwa mjomba wangu kutafuta maisha.
Nikajiunga na Certificate ya Materials Management mwaka mmoja (chuko nakiweka kapuni) - nikamaliza vizuri, Matokeo yakafaa kujiunga na Diploma.
Nikaomba admission ya Diploma Miaka 2 chuo kingine tofauti sababu nilitaka kusomea uongozi wa biashara (Business Administration), nikamaliza na pass ya B.
Nikatafuta kazi lakini sikubahatika kupata kwa urahisi, nikaona bora niendelee kusoma tena, nikaomba chuo hicho hicho kufanya Bsc in Business Administration miaka 3, nikamaliza na GPA ya kawaida baada ya supplementary 2 nikachomoka na gentleman pass kama wanavyoiita.
Nikatafuta kazi sikupata, ila nikafanya kazi ya muda ya kufundisha secondary miezi 6 nikaona mizinguo tu, nikaona nirudi shule tena, nikaenda chuo kingine (Jina Kapuni) nikaomba nifanye Masters in Public Administration, sikupata sababu kwanza pass zangu hazikuwa za juu kwenye Degree yangu na pili Masters nayoomba ni tofauti na Degree yangu.
Nikaona isiwe shida, nikaomba Postgraduate Diploma ya Public Administration Mwaka mmoja, nikamaliza - nilivyomaliza tu nikaunga Masters in Public Administration - nikamaliza vizuri.
Sasa nataka kufanya PHD, ila kuna muda huwa najishtukia kuhusu elimu yangu, ndiyo maana nimeona niweke hapa ili mnieleze kama ipo Genuine na mimi naweza kujiita msomi wa nchi hii yaani Mwanazuoni?
kujiamini inakuwa shinda, sijisikii vizuri mbele ya wasomi wenzangu maana sijapita A-Level; pili nimepitia mfumo wa Certificates, Diploma - sasa inakukwa shida kidogo kujieleza hasa wakati wa kuomba kazi - inakuwa ngumu kueleweka. kuna muda naona aibu kind of.kwanza nikupongeze kwa kuwa unapenda shule....
kwani kinacho fanya utie shaka huo mtiririko wa elimu yako ni nini.....??
au unahic kwakuwa hikupita A-level....!!
jiamini tu, GPA sio issue saana.......
kwani tafsiri halisi ya elimu ni kile kilichobakia kichwani baada ya kijifunza mambo mengi, soma sana japo inaonekana ww ni kula,kulala na kusoma.....
Pamoja na.elimu uloyonayo bado ni tegemezi.....
nataka nimkamate huyo PHD, maana watu wanatamba naye sana, ili niuhakikishie umma kwamba Darasa la saba failure, form form almost failure sasa ana-hold PHD.Mkuu Fuso,, umeungaunga kama mimi, ila wewe ulikuwa kilaza kuliko mimi! Ha ha ha haaaaaaa (nakutania mkuu) Hongera kwa bidii yako kusaka elimu. Ningependa kukushauri ufanye kazi kwanza ili angalau uwe na uzoefu kwenye eneo mojawapo la kitaaluma maana nina wasiwasi na hizi gentleman zako kama jamaa wanaweza kukufanya uwe lecturer! Vinginevyo hutapata wa kukuajiri labda kama unataka kusoma ili ujiajiri mwenyewe kwenye eneo la utafiti!!
Yaani mkuu mpaka una masters lakini kujiamini kunakosekana? Basi hiyo elimu haitakusaidia bora ujikalie tu home ujigegedee mama yoyo basi! Huko unakoenda ni aibu tupu! Ona akina Mwakyembe na ma-PhD yao wanavyojivua nguo, hapa Tanzania hakuna mwenye PhD aliyeonekana kuwa na busara bora uishie masters uanze kusaka maisha.nataka nimkamate huyo PHD, maana watu wanatamba naye sana, ili niuhakikishie umma kwamba Darasa la saba failure, form form almost failure sasa ana-hold PHD.
Unaonage mkuu wazo langu?
Kiukweli pesa sina, maisha yangu ni ya upweke sababu muda mwingi natumia kusoma, maana akili yangu nayo haishiki kwa urahisi, yaani ni kwa mbinde mno siyo kama wengine anasoma kidogo tu kamaliza, mimi ni kukesha na vitabu.Kusoma sio sifa pesa unazooooo...Maana naona mtiririkoooo icjekuwa unamtegemea baba tafadhal maana utamtoa roho
Haya mambo ya juzi ndiyo yamenifanya nipoteze kuiamini elimu yangu, inaonekana kuna unyanyapaa kwa sisi tuliofeli feli na kusoma kwa kuunga unga!! na najua tupo wengi sana nchi hii.Yaani mkuu mpaka una masters lakini kujiamini kunakosekana? Basi hiyo elimu haitakusaidia bora ujikalie tu home ujigegedee mama yoyo basi! Huko unakoenda ni aibu tupu! Ona akina Mwakyembe na ma-PhD yao wanavyojivua nguo, hapa Tanzania hakuna mwenye PhD aliyeonekana kuwa na busara bora uishie masters uanze kusaka maisha.
Ha ha ha haaaaa,, ila hapo kwenye kurudia ndo kuna changamoto, watu wa zamani kidogo ni wengi mno waliotumia majina ya watu kwenda sekondari ama kwa kurudi aidha kwa kuchukua jina la mtu alishindwa kwenda sekondari wewe unaenda kulipigia shule hilo jina! Ila mwenzetu alikuwa amevuka mipaka, wewe umefeli unaenda kuchukua cheti cha mtu mwingine ili uingie chuo? Hii haikubaliki!Haya mambo ya juzi ndiyo yamenifanya nipoteze kuiamini elimu yangu, inaonekana kuna unyanyapaa kwa sisi tuliofeli feli na kusoma kwa kuunga unga!! na najua tupo wengi sana nchi hii.
nilipokwenda ile shule nyingine kurudia wakanipa jina na mwanafunzi ambaye alikuwa mtoro tangu darasa la tatu hadi la saba hajawahi kanyaga shule, hilo ndilo nikalitumia nikachomoka na ndiyo nalitumia hadi wa leo, kuna muda watu walinishauri nikalibadilishe mahakani ili nirudie la kwangu la zamani - nikastuka nikaona sasa majina mawili watu wangejiuliza nimeyapataje pataje maswali yangekuwa mengi nikaona niache tu.Ha ha ha haaaaa,, ila hapo kwenye kurudia ndo kuna changamoto, watu wa zamani kidogo ni wengi mno waliotumia majina ya watu kwenda sekondari ama kwa kurudi aidha kwa kuchukua jina la mtu alishindwa kwenda sekondari wewe unaenda kulipigia shule hilo jina! Ila mwenzetu alikuwa amevuka mipaka, wewe umefeli unaenda kuchukua cheti cha mtu mwingine ili uingie chuo? Hii haikubaliki!
Sasa mkuu hiyo shule ya mateso hivyo ya nini? Achana na PhD tafuta kazi usake maisha mwisho utakuja kufa na li-PhD lako lisilokuwa na maana hapa!! Umeo au umeolewa? Umri unaenda huo oooohhhhh!!!Kiukweli pesa sina, maisha yangu ni ya upweke sababu muda mwingi natumia kusoma, maana akili yangu nayo haishiki kwa urahisi, yaani ni kwa mbinde mno siyo kama wengine anasoma kidogo tu kamaliza, mimi ni kukesha na vitabu.
Mabashite kumbe mpo wengi!nilipokwenda ile shule nyingine kurudia wakanipa jina na mwanafunzi ambaye alikuwa mtoro tangu darasa la tatu hadi la saba hajawahi kanyaga shule, hilo ndilo nikalitumia nikachomoka na ndiyo nalitumia hadi wa leo, kuna muda watu walinishauri nikalibadilishe mahakani ili nirudie la kwangu la zamani - nikastuka nikaona sasa majina mawili watu wangejiuliza nimeyapataje pataje maswali yangekuwa mengi nikaona niache tu.