Nina Mashaka na wapiga debe sakata la Ngorongoro

mkalamo

JF-Expert Member
Sep 7, 2013
324
347
Takriban mwezi mmoja na zaidi kumekuwa na harakati mbali mbali kuhusu hifadhi ya Ngorongoro ama wahame au wabaki,huku kila upande ukijenga hoja yake

Pia waziri Mkuu Kasim Majaliwa aliwashauri viongozi wawape elimu wahusika kabla ya kufikia uamuzi wowote

Mimi hayo yote Sina shida nayo ikiwa Kuna Nia njema mbele

Hofu yangu ni mapambano hayo ya propaganda kuongozwa na watu waliowahi kutuamiminisha kuwa wakati wa Magufuli kila Jambo lipo sawa

Mfano gazeti la Jamvi la Habari kupitia mkurugenzi wake Mchange kwa Sasa ndiyo kinara wa propaganda ya Ngorongoro inateketea.

Huyu ndiye wakati wa awamu ya tano hakuna baya lolote na kila aliyeikosoa serikali au kutumbuliwa na Rais wakati huo alikuwa adui yake na gazeti lake lilisimama kumshambulia hata kutweza utu wa mtu.

Leo hii NCAA kupitia wizara ya maliasili wanatuaminisha kuwa kupitia mtu huyu huyu tutarajie jema katika kelele za Ngorongoro ni ajabu sana
 
Kwani lazima kwenye kila mada umtaje Magufuli?

Unawaongeleaje waliompinga Magufuli kwa kila kitu?

Toa chuki moyoni, kisha fuatilia hoja za pande zote kwa umakini
 
Unategemea hawa wachumia tumbo waandike mazuri,wao wamevuta pesa na kutengeneza kipindi sema watu wamewastukia
IMG_20220212_192711.jpeg
 
Back
Top Bottom