Jibu lako hili hapa kwamba ss Tanzania si wakwanza ila una mawazo mgando
Nukuu ya Ismail Jusa :.. "Uzoefu wa nchi nyingi umeonesha kwamba hatua mbili ni lazima zifanyike kabla ya dola kuanguka. Kwanza, vyama vya upinzani viunganishe nguvu zake; na pili, chama dola kigawike. .. Hatua hizo ndizo zilizoving'oa vyama vya KANU nchini Kenya, UNIP na hata MMD nchini Zambia pamoja na MCP nchini Malawi. Hata Zimbabwe katika uchaguzi wa mwanzo ambao ulikipa ushindi MDC dhidi ya ZANU-PF cha Robert Mugabe, hali ilikuwa hivyo hivyo kabla ya Mugabe kuamua kuitia nchi katika machafuko makubwa ili aendelee kubaki madarakani. Mfano wa karibuni kabisa ni wa Nigeria pale chama cha APC cha Rais Muhammad Buhari kilipofanikiwa kukin'goa chama cha PDP cha Goodluck Jonathan na watangulizi wake. Tukio la Olesagun Obasanjo kuchana kadi yake ya PDP ndiyo iliyohitimisha safari ya chama hicho kuondoka madarakani. Ni katika muktadha huo, naona kwamba njia pekee ya kukiondoa madarakani CCM na mfumo wake dhalimu na kandamizi, ambao ndiyo unaolea ufisadi na rushwa, kuua uwajibikaji hapa nchini na hatimaye kuwaingiza Watanzania katika umasikini wa kutupwa wakati nchi yenyewe imejaa utajiri wa kila aina, ni kuunganisha nguvu za vyama vya upinzani na kugawanyika kwa CCM yenyewe. Kuundwa kwa UKAWA na sasa kupasuka kwa CCM kwa hatua ya Mhe. Edward Lowassa na kundi kubwa linalomuunga mkono ndani ya chama hicho kukihama na kujiunga na UKAWA ni fursa ya kihistoria ambayo tunapaswa kuikumbatia ili CCM ifuate mkondo wa vyama dola vyengine vya Afrika na kuipa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nafasi ya kupata MWANZO MPYA utakaotukwamua katika mkwamo huu tuliokwamishwa na CCM. Viongozi wakuu na wakongwe wa siasa za CCM wanapoliona ANGUKO LA CCM tujue sasa zama zake zimefikia kikomo na TANZANIA MPYA INAKARIBIA KUZALIWA. * Karibu Edward Lowassa * Ahsante UKAWA-#‎UkawaniUshindi