Nina mashaka na hii TIGO BIMA

Nina mashaka na hii TIGO BIMA

Kudo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Posts
1,821
Reaction score
6,122
Wakati fulani nilifuatwa na rafiki yangu mmoja aliehitaji nimpe habari kuhusu hii tigo bima na ufanyaji kazi wake,sikuwa muongo kwake nilimweleza sijui kuihusu hii kitu,akaondoka zake

Hivi karibuni alinipigia simu na kunambia yupo hospital ni mgonjwa anaomba nimwazime pesa kidogo,sikusita nikampa

Sasa jana tena alinifuata na kuniomba radhi kwa kunicheleweshea pesa yangu maana anasubiri alipwe na tigo bima alikwisha jiunga kabla hajaugua,lakini ni zaidi ya miezi miwili sasa hajalipwa na hao tigo,anadai aliombwa vielelezo vyote vya hispital akawapa ila kila siku imekuwa ni blaa blaa tu bila kupewa

Utata nilionao ni kwamba mwanzo anadai alifika tigo shop akazituma hizo vielelezo ila ilichukua zaidi ya Wiki tatu wakiwa kimya alipowapogia wakasema hawajaona kitu wakampa namba ya whatsapp akawatumia sasa hapo ikawa kila siku ni blaa blaa nyingi na hatmae siku za hivi karibuni huduma yao kwa wateja haipokelewi anakaa zaidi ya nusu saa bila majibu

So ambae amejiunga na huduma hii na aliwahi kuhudumiwa kwa kulipwa gharama zake anaeza kunithibitishia hapa kama alifanyiwa hivyo?
 
Tigo bima naona ni kama aina ya mtandao wa uhalifu
Namba yao mwisho inaishia 000
Wanakupa maelekezo at the end wanakwambia ingiza namba ya siri.
Nikawaambia tigo wamekataza kutoa namba za siri.
Wanalazimisha....kumbe wapigaji
Nikawaambia tigo wamekataza kutoa namba za siri.
Wanalazimisha sana aisee.
Kuna rafiki yangu alijiunga, kila akiweka pesa kwenye tigo pesa inaliwa.
Usijiunge....utaumia
 
Mwambie aende kwenye ukurasa wao wa Facebook akatoe malalamiko yake atasaidiwa haraka kuliko kutegemea kupiga 100
 
Tigo bima naona ni kama aina ya mtandao wa uhalifu
Namba yao mwisho inaishia 000
Wanakupa maelekezo at the end wanakwambia ingiza namba ya siri.
Nikawaambia tigo wamekataza kutoa namba za siri.
Wanalazimisha....kumbe wapigaji
Nikawaambia tigo wamekataza kutoa namba za siri.
Wanalazimisha sana aisee.
Kuna rafiki yangu alijiunga, kila akiweka pesa kwenye tigo pesa inaliwa.
Usijiunge....utaumia
Kweli kabisa. Mwezi wangu alijiunga na bima hii, hadi sasa hajapata maelezo yeyote kuhusu ni vipi atafaidika na bima hiyo. TAHADHARI KABLA YA HATARI!!
 
Kuna kazi kubwa sana ya kupambana na adui upumbavu hapa Tanzania
 
Walinishawishi san nijiunge.Nikafata taratbu zote za kujiunga,ikabaki kutuma pesa.Machale yakanicheza,sikutuma!
 
Matatizo mengine tunajitakia tu.

Hivi unaanzaje kujiunga na hiyo kitu?

Huwa wakinipigia kunishawishi majibu nayowapaga huwa wanakata simu bila kuaga.
 
Sawa ni wezi wanakupigia simu wanakueleza vizuri na unaridhika kuwa hata ukiwa na homa wanakulipa sasa umwa halafu piga simu mm nimelazwa hosptali Fulani Nina yatizo Fulani wanakwambia bima hii ukifa ndio wanalipa nimejitoa baada hela Kwisha mwaka
Luna faida gani wakungoje ufe? Matapeli hao
 
Wanapokusajiri hawatoi maelezo kuhusu hiyo Bima, unaambiwa hiyo ni bima ya afya. Baadae ukishalipia tu wanakueleza kuwa magonjwa kama vile shinikizo la damu, moyo, kisukari na mengine yasiyo ya kuambukizwa hayamo katika bima hiyo.
 
Back
Top Bottom