NINA IMANI NA MHE:MAGUFULI KURUDISHA HADHI YA SHULE ZA SERIKALI.

Dikkala

Member
Jul 8, 2011
15
8
Kwa miaka ya hivi karibuni kila uchao matokeo ya kidato cha nne na sita kwa shule za serikali yanazidi kuporomoka mpaka inatia aibu(IPO WAPI ILBORU? IPO WAPI KIBAHA? IPO WAPI MZUMBE? IPO WAPI PUGU? IPO WAPI AZANIA N.K???) Nilizoea kuona kwenye kumi bora kuanzaia namba moja mpaka kumi shule za serikali hazipumgui nane .Miaka ya nyuma mwanafunzi akichaguliwa shule ya serikali ilikuwa ni furaha kwa familia na jamii inayomzunguka kwa ujumla, lakini kwa miaka hii hali ni tofauti sana, kwenda kusoma shule za serikali inaonekana ni kama umemtupa kijana wako na humuandalii maisha bora ya baadae hii ni kutokana na hali mbaya ya matokeo kwenye shule za serikali kutokana na mazingira ambayo sio rafiki kuanzia mwalimu mpaka mwanafunzi mwenyewe. Ikiachwa kuendelea hivi ni hatari sana kwa ustawi wa Taifa kwani wenye uwezo wa kuwapeleka shule binafsi ni wachache ukilinganisha na watanzania wengi ambao hawawezi kumudu gharama zake tasfiri yake ni kwamba ukiwa maskini kuna uwezekano mkubwa kukosa elimu bora na matokeo yake kukosa viongozi wa baadae kutoka kwenye jamii masikini.Namuomba Mhe Magufuli asaidie kutatua changamoto kwenye sekta ya elimu kwa kuanzia kuboresha maslahi ya walimu na kuweka mazingira rafiki ya kujifunzia vijana wetu kwenye shule zetu za umma. Nina Imani sana na MHE rais atarudisha shule zetu za umma kwenye hadhi yake kama ilivyokuwa awali ili wanufaika tuwe sote(masikini na matajiri).
Nawasilisha.
 
Hali haitabadilika hadi pale kila mmoja wetu atakavyofahamu wajibu wake na katika hili; sehemu kuu nne hazipo responsible kabisa linapokuja suala la elimu! Serikali haitamizi wajibu wake ipasavyo! Halikadhalika, Walimu nao hawatimizi wajibu wao ipasavyo! Baadhi ya wazazi na walezi nao, hawatimizi wajibu ipasavyo vile vile! Tena hawa ndio jipu namba moja la elimu yetu. Majority wanadhani wakishalipa karo, wakagharamia mahitaji ya shule; wanadhani ndo wameshamaliza kazi! Wanasahau wanafunzi wa siku hizi wanamaliza kidato cha nne wakiwa bado stupid, foolish na wasioweza kujiongoza wenyewe! Matokeo yake, wazazi na walezi wanawaacha watoto hawa wajiongoze wenyewe kama mwanafunzi wa chuo!! Mzazi akishaona mtoto ameondoka kwenda shule, anaamini kila kitu kipo poa...!! Nyie wazazi/walezi wenye watoto wanaosoma, ask yourselves ni lini mara ya mwisho ulihakikisha mwanao ameenda shule na akaingia darasani na kutimiza wajibu wake wa darasani! Watoto wanaachwa kama kuku wa kienyeji na matokeo yake; wamejazana kwenye social networks! Si ajabu humu kuna wazazi/walezi wenye watoto walio kidato cha pili hivi sasa! Kama wazazi hawa wameenda shule, wanasubiria mwakani wawaulize watoto "umechukua nini; sayansi, art au biashara?" Si ajabu hapo mwakani akijibiwa nachukua arts atauliza tena "mbona hukuchukua sayansi?" Yaani, hadi sasa hajui na wala hajishughulishi na trend ya mtoto wake! Ukirudi kwa wanafunzi wenyewe, nao hawatimizi wajibu wao lakini hawa inachangiwa sana na irresponsibility ya wazazi na walimu. Labda tu itokee by chance or by means of goodluck kwamba mtoto mwenyewe awe anafahamu nini anakifanya lakini hawa majority wanahitaji strict follow up.

Hivyo basi, Watanzania tusivyobadilika mindset na kufahamu kwamba na sisi wenyewe ni sehemu ya tatizo, basi hizi shule hata zifundishwe na walimu wenye PhD kutoka Havard, bado watoto watafeli tu! Sie wengine tumesoma enzi ambazo, kitu pekee ambacho kinaweza kukupotezea muda ni chandimu ambacho huwezi kucheza usiku, na TV ambayo wakati ule hata vipindo vyenyewe vinaboa! Kinyume chake, hivi sasa watoto wana nyezo za kuwapotezea muda 24/7. Siku moja nilikutana na ugomvi pale Tigo Ghana Branch (ni True Story hii). Mama amekuja na mtoto wake pale about 6-10 years. Chanzo cha ugomvi ni Facebook... mtoto anataka laptop yake lazima iwe connected na Facebook lakini mama hataki. Lakini varangati ambalo mtoto alilianzisha, ikabidi awe connected!
 
Back
Top Bottom