Nina hizi Stress, nisaidieni kimawazo

Itzmusacmb

JF-Expert Member
Jun 22, 2016
1,531
1,133
KUMBUKA:Kama hujisikii kunishauri na upo hapa kukosoa naomba usisome hii post


Wana JF nina stress. Kwanza mzazi wangu hana uwezo na mimi nataka kusoma so nikiangalia wenzangu ambao tulisoma wote O-level wapo chuo wanasoma diploma na bachelor and mimi nipo home tu, in addition sina kazi na nimetafuta kazi mpaka nimechoka (japo cjakata tamaa ) na cjafanikiwa napata mawazo sana.

Kadhalika sina sina rafiki wa kukaa nae kunipa ushauri maana sisi vijana wa siku hizi kwanza wavivu, tunataka short cut so story zao ni uhuni, mapenzi, muziki na mipira tuu vitu ambavyo havitanijenga na nikisema nitafute wenye mawazo mbadala wote huwa bize na kazi zao so in this case nabaki tuu na strees tuu mpaka nakosa hamu ya kula.

Najiona sina sababu ya kuishi na nikiona mtu aliye na mafanikio mwenye rika langu (22yrs) nataman kufa yani.

Nawasilisha
 
KUMBUKA:Kama hujisikii kunishauri na upo hapa kukosoa naomba usisome hii post


Wana JF nina stress kwanza mzazi wangu hana uwezo na mm nataka kusoma so nikiangalia wenzangu ambao tulisoma wote O lever wpo chuo wanasoma diploma na bachelor and mm nipo home tuu, in addition sina kazi na nimetafuta kazi mpaka nmechoka (japo cjakata tamaa ) na cjafanikiwa, kadhalika sina sina rafiki wa kukaa nae kunipa ushauri maana sisi vijana wa cku hizi kwnza wavivu,tunataka short cut so story zao ni uhuni,mapenzi,muziki na mipira tuu vitu ambvyo havitanijenga na nikisema nitafute wenye mawazo mbadala wote huwa bize na kazi zao so in this case nabaki tuu na strees tuu mpka nakosa hamu ya kula, na najiona cna sabab ya kuishi na nikiona mtu aliye na mafanikio mwenye rika langu (22yrs) nataman kufa yani ,
Nawasilisha
Pole sana mkuu!
Jiite jina lako kimoyomoyo na jiitikie mwenye ( yaani utambue kwanza wewe ni nani) kisha inua macho yako kwa muumba akuoneshe njia na afanye pasipo na njia pawe na njia upite. God be with you.
 
Usikate tamaa, fanya biashara yoyote hata ndogo na USICHAGUE kazi kubali hata kutumwa so utafanikiwa mi nimejisomesha mwenyewe kwa kufanya biashara ndogo ndogo yupo rafiki yangu pia kajisomesha sekondary mpaka chuo kikuu kwa kuuza genge la matunda so jitume kamata fursa na acha ujuaji
 
Pole sana mkuu, cha msingi usikate tamaa, wengi walikuwa kama wewe lakini Mungu wetu ni mwema na mi nadhani ni swala la wakati, Mungu ana kusudi juu ya kila kiumbe chake, hawezi kukuacha uteseke kwa muda mrefu maana yeye hufanya njia pasipokuwa na njia,,,,,,, tunakuombea na tuko pamoja katika sala
 
una spirit nzuri utatoka kwa kuwa umeonyesha nia ya kutaka kutoka na unaumia kuwa masikini...
miaka 22 sio mingi kiasi chakukufanya uumie kwamba umefeli kimaisha, yaani maisha ndio unayaanza sasa, hao wenzako waliofanikiwa jifunze kutoka kwao, lakini pia inawezekana hawana hata discipline ya maisha ila ni system tu waliyoikuta kwenye familia yao imewabeba
kama una utaalamu wowote ule ingia mtaani uutumie, unaweza ukawa hata fundi garage,seremala,computer mfugaji au mkulima na ukatoka vizuri tu kama ukizingatia nidhamu
elimu unaweza ukajiendeeza kupitia kwa watu na mitandaoni, sio lazima uwe na diploma au degree na hizo sio guarantee za kutoka maaana mtaani wapo wengi wenye viwango hivyo wameshindwa kutusua...cha muhimu ni kazi, maarifa na nidhamu baasi utatoka
 
Pole sana mkuu!
Jiite jina lako kimoyomoyo na jiitikie mwenye ( yaani utambue kwanza wewe ni nani) kisha inua macho yako kwa muumba akuoneshe njia na afanye pasipo na njia pawe na njia upite. God be with you.
Asante aisee
 
Mkuu maisha hayana fomula ila ukiamua na usipokata tamaa unatoka au kuna unafuu utaupata katika maisha yako.Wakati nilipokuwa na umri wako na nilikuwa nina maisha kama yako nilishawahi kutoa ushuhuda wangu humu humu JF. Baba yangu alikuwa hana uwezo na sikuwa na mtu wa kunisadia kuniinua as along as nilihitaji kusoma zaidi ili nije kuwa saidia wazazi wangu.Kumbuka sina ujuzi wowote wa elimu zaidi ya elimu yangu ya kidato cha nne.So nikatafuta vibarua vya hapa na pale nikawa msaidizi wa dereva katika magari ya mizigo.Nikajitahidi kubana matumizi na kufanya kazi kwa juhudi zangu zote mpaka nikapata pesa iliyoniwezesha kusoma chuo mpaka sasa hivi ninamshukuru Mungu wadogo zangu wote nimewasomesha nimebaki na mmoja tu ambaye yupo O level ingawa natarajia naye atamaliza kama wenzake ili na yeye akajitegemee.
Hiyo ni njia yangu iliyonifikisha hapa nilipo nina nyumba moja pia nina shamba lipo chanika nina fuga kuku ,mbuzi na ng'ombe pia nina miradi tofauti . Cha msingi usikate tamaa kijana huo umri ni mdogo sana jitahidi kutafuta vibarua huenda ukatoka kimaisha kwa njia nyingine sio mpaka usome sana maisha ni juhudi zako tu kijana.
 
22 yrs midogo sana,,,,, if education is expensive try ignOrance,,,,, umri huo wenzio wanawaza kitabu we uNawaza utajir na mali....
 
Back
Top Bottom