Vyeo walivyonavyo wamevipata kutokana na vitendo vyao vya kujikomba, kujipendekeza na kusifia kwa unafiki. Je, wataachaje kufanya vitendo hivyo wakati ndivyo vinawapatia shibe yao ya kila siku???Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa upumbavu ni sifa sawa na ilivyo ufupi au urefu; yaani huwezi kuubadili. Ina maana, kwa tafsiri ya Mwalimu Nyerere, mpumbavu huwezi kumbadilisha akawa mwerevu.
...
Kwa nchi zilizostaarabika na kuendelea, mtaji mkubwa kabisa kwa Serikali ni ELIMU KUBWA walizonazo Wananchi wao. Lakini kwa nchi ambazo hazijastaarabika na zilizo duni kwa maendeleo, mtaji mkubwa kabisa kwa Serikali ni UJINGA MKUBWA ULIOTOPEA walionao wananchi wake.Cha kushangaza ujinga huu unazidi kushika Kasi hapa nchini. System imefanya makosa makubwa sana kuruhusu chama kimoja kukaa madarakani muda mrefu, tena kwa shuruti. Sifa za kijinga zinazidi kushika kasi baada ya kuwa na uhaba wa mafanikio tarajiwa. The worse is yet to come.
Bams, tuna taifa la watu wa ajabu sana. Wanafurahia kufanya siasa kwenye maafa!!! Kwa maana nyingine serikali ya CCM inaombea maafa mengine yatokee ili wapate nafasi ya kufanya siasa. Cha ajabu wamezuia vyama vingine visiende na viongozi wa Chadema wamezuiriwa kuingia Hanang. Hivi kweli tunabaguana hadi kwenye misiba?? Hivi wanadhani wananchi ni wapumbavu kiasi hichoMwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa upumbavu ni sifa sawa na ilivyo ufupi au urefu; yaani huwezi kuubadili. Ina maana, kwa tafsiri ya Mwalimu Nyerere, mpumbavu huwezi kumbadilisha akawa mwerevu...
Mkuu Tindo,Tanzania hakuna Cha system bali kundi la wahuni wafaidika na mfumo huu wa utawala,Kuna hitajika nguvu ya umma kuleta mageuzi ndani ya taifa hili.Cha kushangaza ujinga huu unazidi kushika Kasi hapa nchini. System imefanya makosa makubwa sana kuruhusu chama kimoja kukaa madarakani muda mrefu, tena kwa shuruti. Sifa za kijinga zinazidi kushika kasi baada ya kuwa na uhaba wa mafanikio tarajiwa. The worse is yet to come.
Kweli kabisa, huwa nasema bila machafuko au mapinduzi ya kiheshi tusitegemee mabadiliko yoyote ya maana.Mkuu Tindo,Tanzania hakuna Cha system bali kundi la wahuni wafaidika na mfumo huu wa utawala,Kuna hitajika nguvu ya umma kuleta mageuzi ndani ya taifa hili.
"Katika nchi za Afrika hakuna Serikali, bali kuna magenge ya watu walioshika silaha na kupora rasilimali za nchi ili kujinufaisha wao wenyewe binafsi pamoja na vibaraka wao."Mkuu Tindo,Tanzania hakuna Cha system bali kundi la wahuni wafaidika na mfumo huu wa utawala,Kuna hitajika nguvu ya umma kuleta mageuzi ndani ya taifa hili.
Ukweli ulio wazi ni kwamba,watu wanao mzunguka Rais Honorable causa ni reflection ya Raisi mwenyewe,hivyo basi hakuna haja ya kumtafuta mchawi kwa kumung'unya maneno wakati mchawi yupo dhahiri kabisa.
Nelson Mandella kasha wahi sema "ni vema viongozi wajao wa kiafrika kuwa na akili zaidi kuliko sisi wapigania uhuru maana yajayo yanahitaji akili na ujasili"
Sasa hawa tulio nao ni wapumbavu.
Yaaani porojo zako zote ulizo piga hapa ni kwa kuwa tu mh Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania anapongezwa kwa kazi nzuri na maelekezo yake watendaji wa serikali kwa ajili ya kuwasaidia wahanga na majeruhi wa mafuriko ya Hanang eneo la kateshi. Kinachokutesa wewe siku zote ni chuki zako binafsi kwa mh Rais na li roho lako baya lililojaa wivu hasa baada ya kuona mh Rais akiendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya watanzania.
Mtu mwenye akili timamu siku zote,huwa hapendi sifa za kijinga ambazo mwisho huutweza utu,lakini kwa mtu mpumbavu sifa huwa sehemu ya maisha yake ili kuficha udhaifu au madhaifu yake.Upo sahihi.
Nina hakika kama Rais asingekuwa anapenda huu upuuzi wa sifa za kinafiki, lazima ungekoma.
Mwalimu Nyerere, wakati wa uongozi wake walitokea watu wanafiki wakawa wanajikomba kwake, wakamwita ni Musa wa Tanzania. Mwalimu alichukia, aling'aka hadharani. Akasema lile kuniita mchongameno nimekubali, lakini hili la Musa, sitaki, sitaki kabisa kulisikia. Hakuna aliyemwita tena kwa jina hilo.
Kuna watu kwa kutaka kujipendekeza kwa mwalimu, wakawa wanabwagiza kwenye mikutano kwa kusema, 'zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM', mwalimu akang'aka, akawauliza, yaani zidumu fikra za mwenyekiti hata zisipokuwa sahihi? Ndipo wakabadilisha wakawa wanasema, zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM.
Mara baada ya uhuru, wapo walioanza kumwita Mwalimu Nyerere, Mheshimiwa, Mwalimu akakemea na kusema kuwa waheshimiwa ni wananchi. Akawaambia wamwite 'ndugu', kama hawataki kumwita ndugu, wamwite Mwalimu.
Lakini haya ya sahizi, tena mengine hayana hata heshima kabisa, yanang'ang'ania yaitwe "mheshimiwa".
Siku zote matendo ya wasaidizi huashiria hulka za mkubwa wao. Kama Rais asingekuwa anapenda kusifiwa na kutukuzwa, kusingetokea tena mtu wa kumfanyia hayo.