Nina dhamira ya kushika dola 2020 - Mashinji

mkolaj

JF-Expert Member
Mar 24, 2014
3,020
1,087
Katibu Mkuu mpya wa Chadema, Dk Vincent Mashinji ametamba kuwa licha ya umri mdogo alionao na kipindi kifupi cha uanachama ndani ya chama hicho, ana uwezo, nia, dhamira na lengo la kukiandaa kushika dola mwaka 2020.

“Nilikuwa mwanachama wa Chadema asiye na kadi ya uanachama kwa kipindi kirefu, baadaye bila malipo, kushawishiwa wala kutumwa, mimi na wasomi wenzangu tuliandaa na kutekeleza mikakati ya kukijenga chama nje ya mfumo rasmi wa chama,” ni kauli ya Dk Mashinji wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza Kuu la Chadema juzi usiku.

Daktari huyo wa binadamu aliyetambulishwa jana kwenye mkutano wa hadhara jijini Mwanza, alisema baada ya kukutana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, yeye na wenzake walikutanishwa na aliyekuwa Katibu Mkuu, Dk Wilbrod Slaa.

“Baada ya kutusikiliza na kuelewa mikakati yetu, Dk Slaa alituhoji iwapo sisi ni wanachama hai wenye kadi za Chadema. Swali lililotushtua kwa sababu miongoni mwetu hakuna aliyekuwa na kadi,” alisema na kuendelea.

“Tulimjibu Dk Slaa kuwa uanachama wetu uko mioyoni; hoja aliyoikubali, lakini akatuelekeza kujiunga na kuchukua kadi rasmi kwa sababu yapo majukumu ambayo hatuwezi kuyatekeleza bila kuwa wanachama hai,” alisema na kuongeza:

“Nilichukua rasmi kadi ya Chadema Machi Mosi, 2013 kutekeleza ushauri wa Dk Slaa,” alisema Dk Mashinji, mwenye umri wa miaka 43.

Ilani ya chama

Aliongeza: “Kwa sababu nilishiriki kuandaa ilani ya uchaguzi na sasa nimekabidhiwa jukumu la kuwa Katibu Mkuu wa chama, nitasimamia utekelezaji wa ilani hiyo katika halmashauri zote za wilaya zinazoongozwa na Chadema.”

Aliwataka mameya na wenyeviti wa halmashauri zilizo chini ya chama hicho kuisoma, kuilewa na kuitekeleza ilani hiyo aliyosema sehemu kubwa imeigwa na CCM ili kuwaonyesha wananchi tofauti ya vyama hivyo kivitendo linapokuja suala la maendeleo na maslahi ya umma.

Mshikamano kuelekea 2020

Akizungumzia mkakati wake kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2020, Dk Mashinji alisema dhamira yake kuu ni kuwaunganisha wanachama, viongozi, wapenzi na wafuasi wa Chadema kwa kutoa fursa kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake kufikia lengo la kushika dola miaka mitano ijayo.

“Kila mwana Chadema aweke lengo la kukijenga chama tayari kwa ushindi 2020. Tuige tabia ya maji mtoni ambayo kila tone dogo hujiunganisha na tone lingine na kufanya mafuriko makubwa yanayotembea,” alisema.

Mashinji ni nani?

Akisimulia historia yake fupi, Dk Mashinji alisema alizaliwa mjini Musoma mkoani Mara, makuzi yake ni jiji la Mwanza na kusomea Uganda namna ya kuishi katika mazingira magumu, zikiwamo vurugu.

“Ninachomaanisha ni kutuma salaam kwa watani zetu kuwa mimi siyo mtu legelege hata kidogo,” alisema na kuibua shangwe ukumbini.

Alisema kwa kuzaliwa mkoani Mara, amefanikiwa kubeba tabia ya ujasiri, uthubutu na kutohofia lolote wanalosifika kuwa nalo watu wa mkoa huo na papo hapo amerithi tabia ya upole, lakini wenye msimamo wa jamii ya mkoa wa Mwanza na kuahidi kuzichanganya pamoja katika uongozi wake.

Maoni ya wachambuzi

Wakitoa maoni yao wachambuzi wa masuala ya siasa wamesema chama hicho kinahitaji mtu atakayekijenga ili kiendelee kuwa chama chenye nguvu nchini.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu), Gaudence Mpangala alisema chama hicho kinahitaji mtu mwenye msimamo na uwezo wa kukabiliana na mbinu kali za chama tawala CCM.

Alisema katibu mkuu ndiye mtendaji wa chama, kwa hiyo nafasi hiyo inahitaji mtu mwenye uwezo wa kuwaleta watu pamoja na kukifanya chama kuwa kimoja.

“Siwezi kumzungumzia huyu aliyeteuliwa jana (Mashinji) kwa sababu simfahamu. Bila shaka Baraza Kuu limeona anafaa ndiyo maana amepitishwa. Wengi tulitarajia watu wenye majina makubwa kushika nafasi hiyo,” alisema Profesa Mpangala.

Hata hivyo, alisema hajashtushwa na uamuzi huo kwa sababu waliompitisha wanamfahamu vizuri na wanaamini atatekeleza majukumu yake vizuri.

Katibu Mkuu wa NCCR – Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema nafasi ya katibu mkuu wa chama inahitaji mtu mkali ambaye atawasimamia watendaji wengine wa chini yake, maadili na katiba ya chama chake.

“Siwezi kumzungumzia huyo (Mashinji) moja kwa moja kwa sababu simfahamu. Lakini ana kazi kubwa ya kukijenga chama chake na kuhakikisha kwamba katiba ya chama inafuatwa,” alisema.

Nyambabe aliongeza kuwa ana imani Mashinji atafanya kazi vizuri kwa sababu viongozi wa juu wa Chadema wameridhia uteuzi wake.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Emily Jonathan alisema hana uhakika kama Mashinji anaweza kuvaa viatu vya Dk Slaa kwa sababu katibu huyo mkuu wa zamani wa Chadema alikuwa na nguvu na ushawishi wa kipekee katika uongozi.

Alisema pengo la Dk Slaa limeonekana wakati wote tangu alipoondoka Chadema. Alisema mtu wa kuziba pengo hilo anatakiwa kuwa na haiba yake au kuwa na mtindo mwingine wa uongozi ambao utamfanya kuwa na ushawishi kwa wanachama na viongozi wenzake.

Chanzo: Mwananchi
 
“Nilikuwa mwanachama wa
Chadema asiye na kadi ya
uanachama kwa kipindi kirefu,
baadaye bila malipo, kushawishiwa
wala kutumwa, mimi na wasomi
wenzangu tuliandaa na kutekeleza
mikakati ya kukijenga chama nje ya
mfumo rasmi wa chama,” ni kauli ya
Dk Mashinji wakati akizungumza na
wajumbe wa Baraza Kuu la Chadema
juzi usiku.
.
Alikuwa mhujumu serikali aliyekuwa ndani ya serikali.Na wengi wa team Lowasa ndio ilikuwa kazi yao.Kuivuruga na kuihujumu serikali wakiwa ndani ili ionekane serikali ya CCM haiwezi kazi wakati wataalamu kama huyu wakipewa klazi mahospitalini walikuwa wakihujumu kila kona kwa kutoa huduma duni kuudhi wagonjwa nk ili mradi serikali ya CCM ionekane dhaifu wakiandaa mazingira ya upinzani kushinda.

Mungu hawafichi wanafiki.Laana za wagonjwa waliokufa mahospitalini kwa migomo aliyoandaa na iliyoratibiwa na CHADEMA maiti zilizokufa kule ziliko damu zao zitaendelea kulia na kumwomba mWenyezi Mungu asiache kuwashughulikia CHADEMA na huyo katibu mkuu .

Wote waliohujumu serikali wakiwa ndani ya serikali Mungu hatawaacha hivi hivi kwani waliumiza wananchi wengi wasiokuwa na hatia kwa milengo ya kisiasa.
 
Alikuwa mhujumu serikali aliyekuwa ndani ya serikali.Na wengi wa team Lowasa ndio ilikuwa kaz\i yao.Kuivuruga na kuihujumu serikali wakiwa ndani ili ionekane serikali ya CCM haiwezi kazi wakati wataalamu kama huyu wakipewa klazi mahospitalini walikuwa wakihujumu kila kona kwa kutoa huduma duni kuudhi wagonjwa nk ili mradi serikali ionekane dhaifu wakiandaa mazingira ya upinzani kushinda.

Mungu hawafichi wanafiki.Laana za wagonjwa waliokufa mahospitalini kwa migomo aliyoandaa na iliyoratibiwa na CHADEMA maiti zilizokufa kule ziliko damu zao zitaendelea kulia na kumwomba mWenyezi Mungu asiache kuwashughulikia CHADEMA na huyo katibu mkuu .

Wote waliohujumu serikali wakiwa ndani ya serikali Mungu hatawaacha hivi hivi kwani waliumiza wananchi wengi wasiokuwa na hatia kwa milengo ya kisiasa.
unaongea kama umekalilishwa.

swissme
 
Aliongeza: “Kwa sababu nilishiriki kuandaa ilani ya uchaguzi na sasa nimekabidhiwa jukumu la kuwa Katibu Mkuu wa chama, nitasimamia utekelezaji wa ilani hiyo katika halmashauri zote za wilaya zinazoongozwa na Chadema.”
Ngoja tumsomeshe huyu katibu mkuu
ILANI IPI ALIYOTENGENEZA? Ile WHITE ELEPHANT ambayo haijawahi somwa hata siku moja na kunadiwa na Lowasa mgombea uraisi wao kwenye kampeni zake? Lowasa alikuwa akijinadi yeye kama yeye hakuwahi nadi hiyo ilani!!!! Na alisema hana muda wanaotaka kuijua wakasome kwenye mtandao!!!!!!!

Chama kikishindwa uchaguzi mkuu ina maana na ilani ya chama husika imekataliwa!!! Kusema ataitekeleza wakati asilimia kubwa ya wapiga kura wameikataa haiwezekani.

Ukitaka kujua kuwa huyu katibu mkuu hajui siasa angalia.Ilani yao inasema watatoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu anaweza somesha bure watato wote wa mikoa ya Kilimanjaro,Arusha,Iringa Dar es salaam na kote walikoshinda? Aweza somesha bure wanafunzi wote walioko vyuo vikuu vilivyoko kinondoni na ubungo kama vile chuo kikuu cha Dar es salaam,Chuo cha Tumaini,Kairuki, chuo cha usafirishaji nk

Ilani hiyo ilishakataliwa kwa ushindi wa Magufuli aiweke tu kabatini asubiri uchaguzi ujao
 
SASA HIVI TUNAIFUATA ILANI GANI?
 
ccm chama makini duu! au umetoka usingizini? kama sio usingizini basi umekuja leo kutoka Congo huijui tanzania! ila mimi naomba siku moja polis na jeshi waje watuachie uwanja mbwembwe zao zitaisha yaani tutakuja watahili magovi kwa kisu cha kutu
 
Ngoja tumsomeshe huyu katibu mkuu
ILANI IPI ALIYOTENGENEZA? Ile WHITE ELEPHANT ambayo haijawahi somwa hata siku moja na kunadiwa na Lowasa mgombea uraisi wao kwenye kampeni zake? Lowasa alikuwa akijinadi yeye kama yeye hakuwahi nadi hiyo ilani!!!! Na alisema hana muda wanaotaka kuijua wakasome kwenye mtandao!!!!!!!

Chama kikishindwa uchaguzi mkuu ina maana na ilani ya chama husika imekataliwa!!! Kusema ataitekeleza wakati asilimia kubwa ya wapiga kura wameikataa haiwezekani.

Ukitaka kujua kuwa huyu katibu mkuu hajui siasa angalia.Ilani yao inasema watatoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu anaweza somesha bure watato wote wa mikoa ya Kilimanjaro,Arusha,Iringa Dar es salaam na kote walikoshinda? Aweza somesha bure wanafunzi wote walioko vyuo vikuu vilivyoko kinondoni na ubungo kama vile chuo kikuu cha Dar es salaam,Chuo cha Tumaini,Kairuki, chuo cha usafirishaji nk

Ilani hiyo ilishakataliwa kwa ushindi wa Magufuli aiweke tu kabatini asubiri uchaguzi ujao

Kupitia maandishi yako nimeona una nakisi kubwa ya Ulewa madhumuni na namna ya kutekeleza ilani

Serikali kuu inayokusanya kodi inapaswa kuweka vipaumbele vya matumizi ya kodi za wananchi

Tanzania tunahitaji sana kuwekeza kwenye Elimu na Afya.

Ripoti iliyozinduliwa Juzi na Mkuu wa UN Tanzania juu ya Maendeleo ya Binadamu Duniani kwa mwaka 2015 inaonyesha kwamba uwekezaji kwenye Elimu umekuwa instrumental katika maendeleo ya binadamu kwa hiyo Katika ilani ya CHADEMA ilikuwa sahihi kabisa kuweka mbele suala la Elimu

Katika Halmashauri tunazoongoza tumeweka mkakati thabiti wa kutekeleza Ilani hii
 
Ngoja tumsomeshe huyu katibu mkuu
ILANI IPI ALIYOTENGENEZA? Ile WHITE ELEPHANT ambayo haijawahi somwa hata siku moja na kunadiwa na Lowasa mgombea uraisi wao kwenye kampeni zake? Lowasa alikuwa akijinadi yeye kama yeye hakuwahi nadi hiyo ilani!!!! Na alisema hana muda wanaotaka kuijua wakasome kwenye mtandao!!!!!!!

Chama kikishindwa uchaguzi mkuu ina maana na ilani ya chama husika imekataliwa!!! Kusema ataitekeleza wakati asilimia kubwa ya wapiga kura wameikataa haiwezekani.

Ukitaka kujua kuwa huyu katibu mkuu hajui siasa angalia.Ilani yao inasema watatoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu anaweza somesha bure watato wote wa mikoa ya Kilimanjaro,Arusha,Iringa Dar es salaam na kote walikoshinda? Aweza somesha bure wanafunzi wote walioko vyuo vikuu vilivyoko kinondoni na ubungo kama vile chuo kikuu cha Dar es salaam,Chuo cha Tumaini,Kairuki, chuo cha usafirishaji nk

Ilani hiyo ilishakataliwa kwa ushindi wa Magufuli aiweke tu kabatini asubiri uchaguzi ujao
Nadhani unahitaji kujisomesha wewe mwenyewe ile ahadi ya kusomesha bure ni iwapo CDM ikishika dola, jiongeze acha hoja mufilisi!
 
Alikuwa mhujumu serikali aliyekuwa ndani ya serikali.Na wengi wa team Lowasa ndio ilikuwa kazi yao.Kuivuruga na kuihujumu serikali wakiwa ndani ili ionekane serikali ya CCM haiwezi kazi wakati wataalamu kama huyu wakipewa klazi mahospitalini walikuwa wakihujumu kila kona kwa kutoa huduma duni kuudhi wagonjwa nk ili mradi serikali ya CCM ionekane dhaifu wakiandaa mazingira ya upinzani kushinda.

Mungu hawafichi wanafiki.Laana za wagonjwa waliokufa mahospitalini kwa migomo aliyoandaa na iliyoratibiwa na CHADEMA maiti zilizokufa kule ziliko damu zao zitaendelea kulia na kumwomba mWenyezi Mungu asiache kuwashughulikia CHADEMA na huyo katibu mkuu .

Wote waliohujumu serikali wakiwa ndani ya serikali Mungu hatawaacha hivi hivi kwani waliumiza wananchi wengi wasiokuwa na hatia kwa milengo ya kisiasa.
Kama unaweza panda ukazibe
 
Back
Top Bottom