Nina cholestro nitumie dawa gani za vyakula? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina cholestro nitumie dawa gani za vyakula?

Discussion in 'JF Doctor' started by Mbwambo, May 9, 2012.

 1. M

  Mbwambo JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Jamani ninaomba ushauri wenzagu nina cholestro ambayo nimepewa dawa za hospital kuanzia leo kunywa miezi miwili.
  Je kitu gani cha asili nitumie ili itoke mwilini mwangu?
  Asanteni:israel:
   
 2. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,023
  Likes Received: 2,645
  Trophy Points: 280
  Nenda pale Eden Saniturium Clinic Kimara Stop-Over wana dawa za miti shamba ambazo ukitumia ndani ya mwezi mmoja cholesteral level yako itakuwa normal.Wana vipimo kabla ya kutumia na baada ya kutumia dawa,you can check anywhere you like na results zitakuwa positive.
   
 3. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  hapa jf dr sijui kama ni madr wa kienyeji. ila najua umepewa statin, na unatakiwa kunywa usiku. usipofuata masharti ya dr, utapatwa na magonjwa ya moyo. mzaa mzaa tumbua usaha.
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Yupo Mtaalamu wa Dawa za Kiasili humu JF anaitwa MziziMkavu, nadhani akiiona hii mada atakusaidia sana, dawa za hospital ni nzuri lakini zina side effect nyingi, maana unaweza ukawa unatatua tatizo la Cholestro na ukasababbisha tatizo la Figo
   
 5. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Onions contain chemicals which help fight the free radicals in our bodies. Free radicals cause disease and destruction to cells which are linked to at least 60 diseases.

  When a person eats at least 1/2 a raw onion a day, their good type HDL cholesterol goes up an average of 30%. Onions increase circulation, lower blood pressure, and prevent blood clotting.
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Nasikia Kitunguu swaumu na kunywa green tea inasaidia...jaribu kufanyia utafiti
   
 7. Senior Boss

  Senior Boss JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 3,285
  Likes Received: 2,025
  Trophy Points: 280
  Ni PM ntakuunganisha na mtaalamu anae toa ushauri na kuuza bidhaa zilizozibitishwa na zenye ubora kimataifa. Na imani tatizo lako litaisha !!!
   
 8. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Kolesteroli au Helemu ni nini?, bonyeza link ifuatayo ukajifunze kolesteroli ni nini http://maajabuyamaji.net/kolesteroli/ pia katika web hiyo hiyo utajifunza namna ya kuyatumia maji kujikinga na kujitibu cholesterol na magonjwa mengine mengi.

  www.maajabuyamaji.net
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  @Kituko Dawa ya Kuteremsha Cholesterol mwilini Fanya hivi :
  TEMBE 4 Kitunguu Saumu
  * MAJANI YA MVUJE KIASI MAJANI 14
  * (YOUGHUT) Mtindi VIJIKO VYA SUPU 2

  ** CHANGANYISHA KWENYE BLENDA MPAKA VICHANGANYIKE VIZURI IGAWE MARA MBILI.
  KULA ASUBUHI NA USIKU KILA WIKI MARA 3.

  Au hii tumia :
  Chukua majani ya mvuje (fresh) wahindi wanaita currypata na majani ya mchaichai (fresh) chemsha na

  maji ufanye kiasi yasiwe majani mengi yawe kiasi na maji kiasi kisha kunywa gilasi moja, kwa siku mara 3 au 4 na

  peleleza ukifanya haja ndogo utaona mafuta yanatoka au yanang`ara ng`ara yaani ndo mafuta yanatoka tumia kwa

  mwezi kisha kacheki na ukiwa una cholestrol kubwa unaweza kutumia zaidi ya mwezi kisha ukachek. mambo yakustajabisha wengi walotumia wamefanikiwa.


  JARIBU UTAONA MIUJIZA YA Mwenyeezi Mungu
   
 10. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  utakula kila dawa ndugu. We anza tu utaratibu wa ratiba ya mazoezi. Hii itaondoa lehemu pamoja na kuimarisha misuli ya moyo na kusaidia damu kusambaza hewa kila kona ya mwili
   
 11. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Maoni wengi wamekupa "Mvumilivu Wangu", ila ningependa kujua nini kinakusumbua mpaka wakasema una Cholestrol nyingi mwilini na wakakupa dawa utumie?
  Naona wengi wanavutia biashara zao humu ndani JF na nje pia, hata hapo ulipoenda pia wameamua kukulamba pesa zako kwa kukuambia una Cholestrol nyingi.
  Be aware with your health.
   
 12. W

  Wamnetu Member

  #12
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ushauri wangu no kuwa kwanza ubadili mwenendo wa maisha yako na uanze kuishi maisha bora! Acha kula red meat na kama ni lazima ule, basi iwe ya kuchemsha tu bila kuwekwa viungo. Kila mara tumia mafuta ya corn oil au vegetable oil na chakula chako kisiwekwe mafuta mengi; tumia maziwa ya low fat au reduced fat na pia epukana na vyakula vya kukaanga kama vile chapati, maandazi nk. Na mwisho, ujitahidi na mazoezi yawe ya kutembea au jogging - nakutakia kila la kheri.
   
Loading...