Nimweleze mama kuhusu huyu best friend wake?

Omba toba juu yako,juu ya Baba yako,juu ya mama yako,juu ya Judy mama yako mdogo. Kwa kile kilichosababisha baba yako akamuacha mama yako tubu, Ingia maombi ya kuwatenganisha kwa jina LA Yesu aliehai kwa kuwataja majina yao. Hakikisha unajua kusali na unasali kwa imani. Haichukui Muda wanachofanya ni wanastail mauti na wamekwisha kufa katika ulimwengu wa kiroho ni wafu wanaozikana. Mpe Yesu wataachana tu hiyo ni roho ya zinaa kwa msaada wa maombi japo utaomba wewe 0767451444 na kama we we ni mwislamu sifahamu sasa jinsi ya kutatua.
Yaani nyie walevi wa Yesu sijui mkoje!!? Sio kila kitu ni cha kuhusishanisa na Yesu. Hivi vitu vinahitaji busara we unamleta Yesu hapa. Na ndio maana mnatuharibia ndoa kwa kuwateka wake zetu na kuwashauri ujinga eti ndo Yesu anavyotaka mwisho wa siku ndoa ikivunjika wake zetu mnatembea nao au wanatembea na watumishi wenu. Shame!!

Mpe ushauri wa busara mwenzio, sio kuleta utapeli hapa
 
Anza kuwashirikisha ndugu wa Mama yako unaojua watakupa sapoti.. au wale rafiki zake unajua wana wema.. huyo mwanamke kwa biashara anataka kuteka vyote vya Mama yako.. hao huwa hata kuua wanaua ili waendeleee na pia wapate mwanaume kimoja.. sio muchezo huyo.. ana plani yake.. na kuzidisha urafiki ndio watu wasimmfikirie vibaya lolote likitokea.. kama unampenda Mama yako utamuokoa kutoka kwa huyo shetani.. usije kulia ukatupwa nje akimbadilisha Baba yako.. mweleze kwa njia yoyote ile.. mwambie upo nae asiwe na wasiwasi.. biashara ni pesa za Baba yako zinaenda kwa huyo Mama pia.. usije juta.. mwambie asap.. usisikilize hao wanasema eti waache.. utajuta milele ulishimdwa kummwambia hadi ikawa hivi au vile.. biashara ataanzisha zake mwenyewe..
 
Aisee. Hapo jaribu kuwa sure na hiyo investiment ya Judy kwa Mama yako. Pia let your dan know kwamba unajua everything and make him responsible for anything wrong in your mom's investiment incase akiwa conned or otherwise.

Pia avoid to tell anything your mom kuhusu that affair.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
sidhani kama kuna mtu ameishia pale umesema aishie kama hapendi story ndefu,ila embu fikiria mama yako anakuja fahamu mwenyewe alafu anajua na wewe ulikua unafahamu.
 
Mwandiko km wa @lara1 i do miss her kwakweli...
All in all dia Ann. .pole sanaaa..
Kazia hiyo mchepuko aisee.
Pia mama anza kumpa tips za kikulacho
Ili ajiongeze
Kutafuta mwenyewe,
Daah..maisha haya! !
 
Anza kuwashirikisha ndugu wa Mama yako unaojua watakupa sapoti.. au wale rafiki zake unajua wana wema.. huyo mwanamke kwa biashara anataka kuteka vyote vya Mama yako.. hao huwa hata kuua wanaua ili waendeleee na pia wapate mwanaume kimoja.. sio muchezo huyo.. ana plani yake.. na kuzidisha urafiki ndio watu wasimmfikirie vibaya lolote likitokea.. kama unampenda Mama yako utamuokoa kutoka kwa huyo shetani.. usije kulia ukatupwa nje akimbadilisha Baba yako.. mweleze kwa njia yoyote ile.. mwambie upo nae asiwe na wasiwasi.. biashara ni pesa za Baba yako zinaenda kwa huyo Mama pia.. usije juta.. mwambie asap.. usisikilize hao wanasema eti waache.. utajuta milele ulishimdwa kummwambia hadi ikawa hivi au vile.. biashara ataanzisha zake mwenyewe..
Best word ever... una akili sana mkuu
 
Mwambie mamako ukweli hasa hapo pa investment huyo mama wa kambo atakuja kupindua
 
Anza kuwashirikisha ndugu wa Mama yako unaojua watakupa sapoti.. au wale rafiki zake unajua wana wema.. huyo mwanamke kwa biashara anataka kuteka vyote vya Mama yako.. hao huwa hata kuua wanaua ili waendeleee na pia wapate mwanaume kimoja.. sio muchezo huyo.. ana plani yake.. na kuzidisha urafiki ndio watu wasimmfikirie vibaya lolote likitokea.. kama unampenda Mama yako utamuokoa kutoka kwa huyo shetani.. usije kulia ukatupwa nje akimbadilisha Baba yako.. mweleze kwa njia yoyote ile.. mwambie upo nae asiwe na wasiwasi.. biashara ni pesa za Baba yako zinaenda kwa huyo Mama pia.. usije juta.. mwambie asap.. usisikilize hao wanasema eti waache.. utajuta milele ulishimdwa kummwambia hadi ikawa hivi au vile.. biashara ataanzisha zake mwenyewe..
Best advice indeed
 
thanks sana. itabidi nijaribu kukaa na Judy tuelezane faida na hasara ya haya mambo hasa ktk investment yao.
I hope hujatumia calculator hehehehehe*
Usiomgee na huyo Judy kuhusu biashara anaweza tafta namna ukapotea duniani Bora, then amumalize na huyo mamako. Michepuko ni hatari
 
Salaam Aleikhum…….

Huu uzi ni kwa ajili ya kuomba ushauri. Nina Imani wapo humu watu wenye mitazamo ya kuona kwa mapana madhara au faida ya hili jambo. Nimejaribu kuwaza kwa Zaidi ya miezi minne sasa namna nzuri ya kumweleza mama yangu kuwa rafiki yake mkubwa, yaani shosti shosti kweli, ndiye anayemzunguka kwa kutoka kimapenzi na baba.

Naomba nieleweke kuwa lengo langu sio kutoa shutuma za usaliti wa baba, maana kwanza naelewa sio mchepuko wake wa kwanza (au pekee), pili men ambao hawana nyumba ndogo hawafiki hata asilimia moja, na tatu huyu shosti wa mama hajaanza leo kutoka na mzee (don’t get me wrong, simkandii mzee. my dad is one of the best people I have ever known, sio kwa kuwa ni baba yangu, ila huyu mzee ni Zaidi ya binadamu, pamoja na mapungufu yake). Lengo langu ni atleast kuvunja huu urafiki wa mama na mchepuko wa baba (who by the way ni pisi moja kali mno).

Hii ni kwa sababu, ingawa wamekua mashost kwa muda mrefu, ila miezi ya karibuni wamekua Zaidi ya marafiki. Wameanza mipango ya kufanya investment za pamoja. Sasa hii inanipa wasiwasi mom anaweza pata Zaidi ya mshtuko akija kugundua. My plan is atleast ajue huyo sio shosti tu, ni mke mwenza. Nilishajaribu kumface huyu shosti wa mama ofisini kwake, alichonijibu niliona kabisa hana mpango wa kuachana na mzee, yeye anamuita kwa jina la kwanza, Paul (sio jina halisi).

Kwa wasiopenda stori ndefu mnaweza ishia hapa na kunipa ushauri wa nini cha kufanya. Ila kwa wanaoweza kuendelea ningependa kutoa background information ya hii triangle.

My mom alinipata mimi akiwa na miaka ishirini kamili, akiwa bado ni mwanafunzi wa diploma. My dad wakati huo alikua ndo amepata kazi serikalini. wamezidiana miaka mitano tu na kwa sasa dad ana miaka 48. Huyu shosti yake mama kanizidi mimi miaka 12 (najua nimewapa kazi ya kukokotoa hahaha, ndo lengo langu). Nilipokua na miaka nane hivi, dad alipata kazi ya uhadhiri nje ya nchi (hapahapa Africa), so baada ya kama mwaka kule, akafanya mpango mom akapata pia kazi ubalozini, so tukawa wote nje ya nchi for years.

Baadae mom akarudishwa wizarani hapa DSM, so ikanibidi nirudi nae. Lakini kabla ya uhamisho, kuna dada aliletwa kuwa mtumishi ubalozi wanchi tuliyokuepo. Huyu dada ndo huyu shostito wa mama. So urafiki wao ulianza kitambo, na hata baada ya kurudi Tz na yule dada kubaki kule, waliendelea kuwasiliana kama marafiki. Kwa kuwa kabla ya mama na mimi kuondoka kule, huyu dada alikua keshapazoea home, nadhani hata baada ya kuondoka mazoea yaliendelea na nahisi mahusiano yake na dad ndo yalianza kipindi hiki.

Mzee aliendelea kukaa huko kwa miaka kadhaa, hadi mimi namaliza form four alikua bado kule. Na kila nilipokua naenda nlikua namkuta yule dada yuko involved sana na mzee. Yaani kunipokea airport watakuja wote, kama ni shopping tunaenda wote, tukiamua kwenda dinner mahali atakuepo, yaani ingawa nilikua bado katoto ila nlijua tu mzee anakula huyu dada. Ila wala sikua na shida sana. Kwa sababu, dada mwenyewe alikua ananijali mnoo yani, nikienda nae shopping ntanunuliwa nguo za fashion current, vipodozi, viatu ….. I really liked her, so akawa kama dada ambaye sikuwa nae, ingawa mwenyewe alipenda nimuite ma’mdogo. So nikawa namuita ma’mdogo Judy (sio jina lake). So hata nikiwa home na mom, akipiga simu mara zote alitataka tuongee pia, so mama alikua ananipa simu napiga nae stori.

Nikiwa kidato cha tano ndo mzee alirudi rasmi bongo. Na wala haikupita hata mwaka, Judy nae akarudi bongo. Akaniambia ameacha kazi ili ajikite kwenye biashara. Nikaona anafocus na maisha. Ila baadae nikajua aliacha kazi ili awe karibu na mzee, ingawa ni kweli alianzisha biashara na in terms of money, anafanya vizuri. Judy aliporudi ndo ukaribu na familia yetu ukaongezeka, weekend nyingi yupo na mama, au atanipigia simu niende kwake, hii hasa nlipoanza chuo. Cha ajabu mara nyingi mzee akisafiri, na yeye after few days utasikia anasema anasafari ya kibiashara.

Ukaribu na mama umekua Zaidi ya urafiki. Kuna kipindi mama alikua na matatizo flani, Judy alijitoa utadhani ni tatizo lake, ikiwepo kutoa pesa zake, kusafiri na mama mpaka India kwa matibabu ambako alikaa Zaidi ya miezi mitatu, mpaka waliporudi wote. So she is close to her.

Siku nilipohakikisha kuwa wana uhusiano, ni jioni ya siku ya Valentine’s day nikiwa mwaka wa pili. Judy alinipigia simu kuniuliza kama nitaenda kwake, maana nilishazoea kwenda sometimes bila hata taarifa. Siku hiyo kwa kuwa kesho yake nlikua na test, nikamwambia sitaenda, basi akanitania “au utakua kwa shemeji?”, nikamwambia hapana nina mtihani, akasema sawa basi ananiondoa kwenye share ya chakula cha jioni, nikamwambia poa.

Kumbe lengo la kunipigia simu ni ili kupata uhakika wa kumleta dad home kwake. Sasa mimi baada ya ile simu nikaanza kujisikia noma, kwanza Judy alishawahi nikuta angle mbaya na jamaa mmoja hivi, ingekua sio ajabu kama angekua kijana umri sawa na wangu, ila mkaka kanizidi miaka inayoonekana kabisa hahahha(hii ni story ya siku nyingine panapo majaaliwa), so wasiwasi wangu ilikua atahisi niko kwa huyu jamaa, alafu anaeza mwambia mzee. So nikachukua uamuzi wa kwenda.

Ilikua mida ya saa mbili usiku. Cha kwanza kuona ni gari ya mzee imepaki kwa nje, nikapiga simu haikupokelewa, bahati nzuri mlango wa kupita watu kwenye geti kubwa haukua umefungwa, so nikasukuma nikaingia, nje ya mlango wa mbele ya nyumba nikaona viatu vya mzee. Ingawa sikua na sababu ya kususpect chochote, maana inaweza kuwa mzee kaja na maza kumtembelea Judy, ila kuna ka hisia ka curiosity kakanijaa, sikugonga mlango, nikazunguka dirishani (mtanisamehe jamani), ingawa sikupiga chabo, ila sauti nilisikia. Nlichofanya nikarudi mbele ya nyumba nikakaa nisubiri wamalize.

Nlivyoona activities za sebuleni na jikoni zimeanza ndo nikagonga mlango. Kama kawaida wakajidai ndo kwanza mzee kafika, alipita tu kupeleka some documents na nini, I decided to go along with their story… So ingawa nimefahamu kwa muda mzee anatoka na Judy, ila ile kuconfirm ikanifanya nianze kujihisi guilty kila nikimuangalia mama. Nahisi kama na mm namsaliti vile. But nikaona ni busara kukaa kimya, akijua ajue mwenyewe. Ila nikapunguza mazoea na Judy, sana mpaka akawa anauliza kulikoni.

Sasa miezi michache iliyopita ndo wakaanza mipango yao ya kuinvest pamoja. Na sio investment ndogo, ni zile za ukitapeliwa unaua mtu. Yaani my mom ni kama ameweka all that she has.. ninachojiuliza, akijua huyu anayeinvest nae ni mke mwenza si atachanganyikiwa akili… moyo wangu unaniambia napaswa kuvunja huu urafiki wa kinafiki, ila pia mama hana rafiki mwingine aliye close kama Judy naona kama her life itakua boring hivi…..

Niliamua kwenda ofisini kwa Judy one day, nlimwambia najua anatoka na dad na nikamuomba aache kumsaliti rafiki yake…. Judy akakaa kimya kwa muda mrefu, nikaona kabisa maneno yamemuingia maana machozi yakawa yanamdondoka, akawa hawezi sema chochote ingawa nligoma kuondoka mpaka anihakikishie atamuacha mzee. Judy akawa ameinamisha tu kichwa hasemi kitu, nikaona hapa napoteza muda nikamuaga nikimwambia she should be ashamed of herself.

Baada ya siku mbili alinitafuta akaniomba tuonane mahali, sikua na haja ya kukataa. Tulikutana moja ya fukwe za kigamboni, baada ya kufika, tumekaa muda wala hasemi kitu. Nikataka kuondoka, akanizuia…

Ann mwanangu, najua ushakua mtu mzima sasa unaelewa kuhusu hisia za mapenzi, mimi na Paul tumependana kwa muda mrefu, na usione kama najitetea ujinga ila I really love him, he is my first man na sina haja ya kuwa na mwanaume mwingine. Nawaza kila siku kuhusu my future, ila I don’t see it without him….”

sijui nikueleze vipi uelewe, maana najua kama mtoto unamfikiria mama yako Zaidi, lakini believe me, I love your mom too, I respect her Zaidi ya rafiki ni kama dada yangu. Ingekua simuheshimu ungeshaona Ann, ila haitatokea kumvunjia heshima hata siku moja…. Mara nyingi nimekua upande wa mama yako hata pale Paul anapokua kinyume nae, sometimes Paul anataka kulala kwangu lakini mm ndo nimekua namgombeza na kumwambia aheshimu mkewe….”

“Najua ni ngumu kueleweka bt please usinihukumu kwa kushindwa kuzuia hisia zangu”


nikadakia, “sawa, lakini huoni unasaliti urafiki wenu, amekua best friend kwako and ulichoona ni kumchukulia mmewe, of all the men duniani ndo ukaamua kufall kwa Paul (nikajikuta na mm natumia jina la kwanza la mzee)”

Judy akaniangalia then akasema, “so unataka nifanyeje Ann, ndo nishajikuta this deep, ingekua mwanzoni mwanzoni labda ningeweza, bt mm na mama yako tumejikuta urafiki wetu unazama sana baada ya mm pia kuwa nishazama sana kwa paul, what should I do?”

jibu lilikua ni moja tu, “chagua moja Judy, be with my dad or be with my mom, you can’t have it both ways”…….

Judy akafikiria kama dkk tano nzima, then kikaona kafunika uso wake kwa mikono akaanza kulia tena, huku akisema kwa kurudiarudia “I cant, I cant, I cant………”

nikaona hapa natwanga maji kwnye kinu.

So guys, najua siwezi tenganisha mahusiano ya Dad na Judy, bt atleast mnaweza nishauri namna ya kumuweka Judy mbali na mama…. How do I do this?
Utulivu alionao baba yako ni kwa sababu ya huo mchepuko wake! Ukivuruga tu familia inasambaratika, ilimladi anamuheshimu mama yako acha yalivyo, utakuja kunishukuru badae!
 
Heshimu maauzi ya wazazi wako acha waenjoy mapenzi ili mradi tu mama yako hajawahi kuumizwa kaa kimya na ungalie usiwe we ndio ukawa mtu wa Kwanza kumuumiza je ww nikuulize huyo bwana wako Kama Ana mke wake jeeee huoni na ww kunamwingine unamuumiza?
 
Imagine,
Judy (ambaye ni pisi kali kwenye mid 30's) ana mchepuko mwingine tofauti na Paul. Huo mchepuko una pisi nyingine ambayo iko kwenye early 20's.Labda mchepuko huo wa Judy ulikufahamu wewe kupitia yeye. Judy alipokukuta kwenye kona mbaya na mwanaume (aliyekwenye mid 30's) aliumia, kwakuwa ndiye mchepuko wake na huenda angemwabia Paul ili avunje uhusiano wenu bila kujua , Paul angekuwa anadumisha penzi baina ya mchepuko wake na mchepuko wa mchepuko wake.
Ingekuwa familia moja interesting Sana!
 
Jambo mdogo wangu?

1. Judy na baba yako wana mtoto?
2. Ushawahi kujiuliza kwa nini wewe ni mtoto pekee kwao? Baba, mama na Judy?
3. Kwa miaka zaidi ya 10 unafikiri mama yako hajashtukia au kafunika kombe mwanaharamu apite?
4. Unafikiri kama Judy angekua na nia mbaya na familia yenu angeshindwa kuwavuruga maana yeye kaishi na baba yako muda mrefu kuliko mama yako.ß

Kwa umri wa Judy miaka 35 hana sehemu ya kwenda baba yako ndio kila kitu chake na familia yenu ni yake. Usiingilie huu uhusiano kaa mbali.

Ila kama unaweza mshauri mama yako kwenye biashara kuhusu kuwa makini na mikataba fanya hivyo lakini angalia usije kuleta taharuki.....

Tell Judy you won't tell anybody about unachojua ila asimuumize mama yako kwenye biashara.
 
Salaam Aleikhum…….

So guys, najua siwezi tenganisha mahusiano ya Dad na Judy, bt atleast mnaweza nishauri namna ya kumuweka Judy mbali na mama…. How do I do this?
You sound young but very intelligent... nishakupenda tayari!! Saint Anne, nishakutana na First Born mwenzangu huyu!!

Anyway, back to the topic!!

First of all, FAMILIA NDO KILA KITU!!

Uhusiano wa baba yako na rafiki mkubwa wa mama yako UNAHATARISHA uimara wa familia... kama sio leo basi kesho, it's a matter of time!!

Kutokana na hilo, unatakiwa kufanya lolote liwezekanalo kuhakikisha your family isn't at risk, whether risk hiyo kutokea leo au kesho!! It's tricky, ukimwambia mama yako kuna hatari ya kuleta mvuruigano mkubwa wa kifamilia kwa sababu ingawaje cheating is just cheating lakini cheating inayofanyika dhidi ya mtu wako wa karibu inauma maradufu kuliko cheating dhidi ya mtu "baki"!

Kwa maana nyingine, ukimwambia mama yako sasa, lakini hata usipomwambia bado kuna uwezekano mkubwa atakuja kugundua tu kwa sababu hakuna mapenzi yaliyo rahisi kufichuka kama yale ya ku-cheat na mtu wako wa karibu!!

Mbaya zaidi, mother akija kugundua mwenyewe halafu akajua kwamba ulikuwa unajua lakini ukakausha, utetezi wako kwamba hukutaka kuleta mtafaruku utakuja kumwingia akilini baadae sana kwa sababu hakuna chochote ambacho mama yeyote angependa kuona kama mwanawe kusimama wima kwa ajili yake no matter what!!!!

Now tell me: Baba na Kimada wake ni religious?!

Endapo kwa kiasi fulani ni religious hata kama u-religious wa kwenda kanisani/msikitini mwaka mara moja, ningekushauri kaonane na kiongozi wa dini!! Na vile vile wanaweza wasiwe religious lakini wakawa ni watu wenye maadili hata kama ni ya kuunga unga!!! Mtu wa aina hiyo atamheshimu tu Kiongozi wa Dini hata kama sio wa imani yake provided ni kiongozi anayeheshimika na jamii!

Ukishakutana na kiongozi wa dini, mwambie kutokana na unyeti wa jambo lenyewe umesita kumwambia mama yako au ndugu yeyote kwahiyo unamuomba kiongozi husika awaite Mshua na Kimada wake bila ya wao kufahamu kwamba wewe ndie ume-initiate huo wito!!

Siku atakayokutana nao, nawe utaibuka kwenye mshauri husika!!

Kiongozi wa Dini anaweza kukushauri usiwepo siku ya kusikiliza hauri lakini sisitiza uwepo ili kumtia aibu baba na huyo kimada, na kama wanajiona wao ndo wanajua kupenda sana kuliko wengine basi wayaseme mbele yako!!!

Aidha, bila kujali Mzee wa Kanisa atawaeleza nini wewe utatakiwa kutoa msimamo wako kwamba ukigundua kwamba hawajaacha mahusiano yao hautakuwa na choice nyingine zaidi ya kuita kikao kingine cha ndugu wa pande zote mbili... yaani ndugu upande wa mama yako na wale wa baba yako, na kwamba utakuwa tayari hata kutafuta mawasiliano ya wazee wa kimada ili kuwaeleza ni namna gani binti yao anavyohatarisha ndoa ya mtu anayejifanya ni rafiki yake wakati kumbe ni nyoka tu kwa sababu haupo tayari kuona mtu anayejifanya ni rafki wa mama anaamua kwa makusudi kuvuruga familia yenu!

Unatakiwa kuwa detrmined wakati unaongea... uongee kama anavyoongea Tundu Lissu na sio kama Mzee wa Dakika ya 89!!

Aidha, sisitiza kwamba, najua mtaona mkiendeleza kwa siri sitafahamu, but trust me, NITAFAHAMU TU kwa sababu yule yule ambae mwanzoni aliniambia kuhusu uhusiano wenu, nina uhakika ataniambia tena na tena kwa sababu nae anachukizwa na mfanyacho...

Anyway, hapo juu ni bluffing lakini itawapa hofu kwamba kumbe kuna mtu wasiyemjua anayefahamu nyendo zao bila wao kujua!!

Assumption yangu ni kwamba, Mshua na hata Kimada wakiona umefanya uthubutu wa kukutana hadi na Kiongozi wa Dini bila ya wao kujua, basi wataamini huwezi kushindwa kufanya lolote lile sawa na hilo!! Kama wana busara, I doubt kama watakuwa tayari kudhalilika mbele ya Kiongozi wa Dini na tena wadhalilike mbele ya wanafamilia!!

Anyway, hiyo ni njia ya Zama za Mwalimu, au njia ya ki-Saint Anne!!

Je, unataka mbinu nyingine? Kama ndiyo, unataka mbinu ambayo ni psychological torture au unataka njia ya kijasusi? If the answer is YES, then be my guest!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom