Nimwambie au ninyamaze? Nimechanganyikiwa

Nimwambie au ninyamaze? Nimechanganyikiwa

Mitihani

Senior Member
Joined
Sep 17, 2013
Posts
158
Reaction score
46
Habari wana Jf.

Naombeni ushauri kuhusu hili nimechanganyikiwa. Nina mdogo wangu yupo kwenye ndoa mwaka wa 12 sasa na ana watoto 3. Yeye na mumewe wanaonyesha wanaishi vizuri, yaani mume anamjali. Tatizo ni wiki 2 zilizopita nimeambiwa na mmoja wa ndugu za mumewe kwamba mume wake anatembea na mwanamke mwingine ambaye ndugu wa mume wengi wanamjua kwa kuwa huyo kimada alijipendekeza hadi kwa mama wa mume na mama kwa kupewa vizawadi au kwa roho mbaya akamkubali huyo bi mdogo na kuanza kumtambulisha kwa ndugu zake kama mke wa pili wa mwanae.
Huyo kimada kwenye sherehe za ndugu wa mume huwa anakwenda wakati huohuo na mdogo wangu yupo ila sasa yeye hamjui, maskini yeye yupo busy ukweni akifanya lile na lile kumbe anajichora tu bila kujua. Huku mama mkwe akiwepo na kuangalia tu pamoja na ndugu wengine wanaojua hilo. Na wakati mwingine huyo kimada anaenda hadi kulala kwa ndugu wa mume na anapokelewa vizuri kwa shangwe.

Huyo mdogo wangu hana ugomvi wowote kwa hao ndugu wa mume akiwemo mama mkwe wake, yaani wakimwona wanamchekea vizuri na kumkumbatia na wanashirikiana naye kwa mambo mbalimbali iwe shida au raha kuonyesha wanampenda na wamemkubali wakati huohuo wanamzunguka.

Sasa basi mmoja wa hao ndugu imekuwa ikimuuma hiyo hali ila kumwambia mke halali anashindwa ndo kanitafuta mimi dada mtu kanipa mchapo mzima na nimeonyeshwa huyo kimada na kuchunguza nimegundua ni ukweli mtupu. Sasa nimekuwa na mtihani mkubwa je nimwambie mdogo wangu hali ilivyo au nifanyaje?

Wao kama familia wanaishi vizuri kwa amani yaani mume anamjali.ile mbaya waweze sema ni ndoa ya amani na ukaitamani lkn mume na nduguze ndo wanamzunguka kiaina hiyo.
Siyo ndugu wote wa mume wanafanya hivyo ila kuna kikundi kama cha watu 7 ndo wapo busy na huyo kimada na wakati huohuo wakimfanya rafiki na kumpenda mke halali.

USHAURI TAFADHARI NIMWAMBIE MKEWE?
 
Usimwambie ndugu yangu kwa kawaida wanasema mambo ya wawili huwa hayaingiliwi hasa kwa kuwa ushasema wanapendana sana,hapo ukimwambia atakuona mchawi wa ndoa yake,tulia japo unaumia hakuna mwanzo usio na mwisho na haukuna siri ya watu wawili na zaidi ya hapo,tulia tuli na wakati ukifika yeye mwenyewe atajionea na atajua achukue uamuzi gani.
 
@Mitihani hii ya dunia, sio mzuri sana katika ushauri hasa wa namna hii, ila ikiwa huyo shemegio mnaelewana vizuri, mwite na uongee nae peke yake ukimueleza kila unachojua ikiwezekana iselete tatizo awepo pia mwenzio, kisha mtamsikiliza anasemaje....?
 
Sijaelewa vizuri hapa, yaani niwaite wote wawili niwaeleze pamoja au niongee na shemeji yangu tu?
 
Usimwambie ndugu yangu kwa kawaida wanasema mambo ya wawili huwa hayaingiliwi hasa kwa kuwa ushasema wanapendana sana,hapo ukimwambia atakuona mchawi wa ndoa yake,tulia japo unaumia hakuna mwanzo usio na mwisho na haukuna siri ya watu wawili na zaidi ya hapo,tulia tuli na wakati ukifika yeye mwenyewe atajionea na atajua achukue uamuzi gani.

Sawa nimekuelewa ila je akija kujua kwamba mimi niliambiwa na sikumwambia?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Sijaelewa vizuri hapa, yaani niwaite wote wawili niwaeleze pamoja au niongee na shemeji yangu tu?

Kama mnaelewana na shemejio nadhani ni wazo zuri ukaongea naye yeye kwanza, kwenda kwa mdogo wako moja kwa moja ni hatari
 
mwite Shemeji yako mweleze aache hiyo tabia.tena kuwa serious! Mimi huwa najiuliza siku zote kwann baadhi ya ndugu wanafurahia michepuko ya ndugu zao?wanasahau kuwa nao wanawatoto wa kike au watakuwa nao ambao watatendwa !kwanini wamkaribishe makwao?hovyo kabisa
 
Yaani mimi mwenyewe inaniuma sana, zaidi ninapomwangalia mamamkwe wake. Badala ya kusimamia ndoa ya mwanae yeye ndo kinara wa kuiharibu. Mbaya zaidi anajifanya anampenda mkwewe.
 
Hii ni ngumu...hapo ukimwambia na mambo yakiharibika wewe utaonekana mfitini umewatenganisha lakini fact ni kwamba unatakiwa umwambie kama dada yake na kama unajali maslahi yake kwasababu akija kujua ulikuwa unajua na ukimficha ataumia sana!unachoweza kufanya ni kutuma anonymous message kwake ili walau azinduke!
 
Yaani mimi mwenyewe inaniuma sana, zaidi ninapomwangalia mamamkwe wake. Badala ya kusimamia ndoa ya mwanae yeye ndo kinara wa kuiharibu. Mbaya zaidi anajifanya anampenda mkwewe.

Kama unampenda ndugu yako mwambie now vinginevyo na wewe mnafiki..umewajua adui wa ndugu yako ..mueleze awajue na yey
 
mwite Shemeji yako mweleze aache hiyo tabia.tena kuwa serious! Mimi huwa najiuliza siku zote kwann baadhi ya ndugu wanafurahia michepuko ya ndugu zao?wanasahau kuwa nao wanawatoto wa kike au watakuwa nao ambao watatendwa !kwanini wamkaribishe makwao?hovyo kabisa

Naunga mkono. Ongea na shemeji yako,hatua atakayochukua ndo utajua ana nia ya kulinda ndoa yake ama la! Nae huyo ndugu wa mume kiherehere alishindwa kuongea na ndugu yake hadi akaja kukuambia wewe? Yan hapa hata ukisema ukae kimya utateseka sana kwaajili ya mdogo wako lol wanaume hawa!
 
Mmmmmmmmmkh! Ukiambiwa mumeo ana nyumba ndogo ULIZA INA VYUMBA VINGAPI? Afu kuna mambo yanachekesha. Ukute yu huyo ndugu wa mume kaona mdogo wako anajishaua shaua, kujishebedua, yeye ndo yeye mwenye mume wengine wote wana migumegume, nyooooo! KAKAA CHINI KATUNGA INSHU NZIMA KUMJAMBISJA JAMBISHA TU BAAAAAS! Basi na mdogo wako nae badala ya kujambishwa kaharisha kabisaaaa! Ndugu woooote mmoja tu ndo aijue hio ishu? Halooooo!

Afu KUTAKA KULA NYINGI KULIWA KINGI! We una bwana, anakujali, watoto wanaenda chooni fresh kila siku na moseji, mi peparoni, micartless sijui, una drive, kodi ya nyumba huijui, bills unazisikia, ada unaitamka tu hio umepewa ila HURIDHIKI KABISAAAA,! HATA MIFUPA ANAYOPEWA MMBWA INAKUUMA ROHO NA KUKUTOA NAFSI! 99 ulivopata wewe huvioni kabisaaa ila hicho 1 alichopewa nyumba ndogo ndo UNAKIKOMALIAAAA! Ungratefull creature. Wewe unatembelea BMW ukisikia mwenzio kapewa ki Starlet utalazwa kwa pressure

Nyumba ndogo haesabu 99 ulivopata wewe Mke, yeye hana hiana kashukuru kwa yote, ana jihumble, na ku jinyenyekeza mpaka mwisho. IN THE END WOTE WANAWAKE EXCEPT ALIKUONA WEWE MAPEMA KABLA YA MWENZIO OR YOU JUST GOT LUCKY. Ndo sazingine mume anakukomoa kwa kukosa shukrani na kuamia nyumba ndoho ampe yale 99 yako ili ukianza kuchonga kupewa 1 inakuwa halali yako kabisaaa.

NAJUA WAKE ZA WATU MTASEMA ITS NOT AOUT THE MONEY ITS ABOUT PRINCIPLE AND RESPECT! PRINCIPLES ARE OVERATED THESE DAYS.
 
Ongea na mume wa mdogo wako. Muweke kitimoto umuulize nini anachotaka, na umwambie kuwa asipoacha utaongea na mdogo wako.

Ukiweza ongea na huyo hawara pia.
 
Mjulishe ndugu yako, lakini mtengenezee mazingira mazuri ambayo hatopata pressure ukimwambia, hilo si la kunyamaza kwasababu mwisho wa siku atalisikia na ukichelewa sana huyo kimada ataleta watoto hapo ndani, bora lijulikane mapema, kuna wanaume ambao hawapendi shari kiasi cha uchafu wao ukisikika nyumbani basi ndio mwanzo mwisho wa kuendelea sasa inawezekana na yeye wa style hiyo ukawa umeokoa jahazi
 
Naunga mkono. Ongea na shemeji yako,hatua atakayochukua ndo utajua ana nia ya kulinda ndoa yake ama la! Nae huyo ndugu wa mume kiherehere alishindwa kuongea na ndugu yake hadi akaja kukuambia wewe? Yan hapa hata ukisema ukae kimya utateseka sana kwaajili ya mdogo wako lol wanaume hawa!

Huyo ndugu wa mume aliyeniambia ni shemeji yake yaani ni mke wa binamu yake naye alishindwa kumfwata.
 
Ongea na mume wa mdogo wako. Muweke kitimoto umuulize nini anachotaka, na umwambie kuwa asipoacha utaongea na mdogo wako.

Ukiweza ongea na huyo hawara pia.

Huko kwa hawara uthithubutu maana utaanzisha jipya hiyo familia isiyojua mke halali watakupelekesha mpk utajuta, ogopa sana watu wanaozuzuka na zawadi ndogo ndogo, wanakuwa washari sana maana wameshazoea kupewa vya haramu
 
Back
Top Bottom