Nimueleweje na nifanyaje?

Nimueleweje na nifanyaje?

mumemwema

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
2,094
Reaction score
1,580
Hello wana Jamiiforums

Mimi ni mwanamke Wa miaka 25-30 . Kama miezi kadhaa nimejuana na huyu Kaka ni mkarimu kwa Kweli na ni mcha Mungu, hii ndio sababu kubwa ambayo imenivuta kwake. Kitu ninachokipenda kingine yaani ananifanya na kuwa free kutania na kuchekeshana kwa sana ma hii Mimi huwa Napenda sana.

Okay sababu iliyonileta hapa ni hivi tuna week ya pili sasa inakwenda hela mawasiliano. Ninakuwa Nina wasiwasi kuhusu hali yake kwa maana si kawaida yake .

Nimepiga simu lines zake zote moja inaita ni ya kikazi Inakata tuu haipokelewi na nyingine ni private haupatikaniki. Ikabidi nimtafute Rafiki yake ambaye akishawahi kunitambulisha mwake na wanafanya kazi pamoja . Nimemuuliza akaniahidi kunifuatilia.

Alichoelezwa kawa Huyu MTU amekwenda likizo. Kumbuka hajawahi kuniambia kuhusu hilo na si kawaida yake. Mimi Bado sikuachia hapo nikaendelea kupiga simu ile ya kikazi kuna MTU alipokea mwanamme akaniambia kuwa huyu MTU hayupo.

Elewa Mimi Niko nnje ya Tz kidogo. Nimeandika SMS nyingi hazijibiwi. FB messages pia hazijibiwi . Nimemuomba msamaha nilipomkosea kwenye FB messages na kwenye SMS lakini wapi Bado kimya . Anajibu messages za wengine FB lakini sio zangu.

Leo nimeingia FB kutizama kama messages yeyote lakini Bado hamna lakini niliona aliingia . Baadae tena nikaingia FB tena kwenye kukaa , nikamuona online nikaita jina lake kwenye messenger Wala hajajibu chochote na hakukaa sana akatoka online.

Hebu niambieni wanaume na wanawake wenzangu nifanyeje? Na Je nimemkosea nini Huyu jamaa yangu? Nia yake ni nini ? Je Kweli anania nzuri na Mimi? Saa nyingine natamani nichukue tuu ndege nije lakini siwezi .

Je niwe na subira nae au niendelee na maisha yangu? Kusema Kweli Nina connection nae moyoni . katika mahusiano yetu, pamoja si ya muda mrefu tumeongea mengi sana kuhusu maisha na familia pamoja na maendeleo . Hata sijui nifanyeje.

Na kama amepata mwingine aniambie tuu ili nijue kuliko kuumia moyoni .

Mchepuko Mimi siwezi .

Nawasikiliza ndugu tafadhali.

Asante
 
Hello wana FJ.

Hapao kwenye wino kuna error, lakini sio mbaya najua yote ni stress tu kasababisha huyo kijana mpole, lakini si unajua wanasema kimya kingi kina mshindo, kaa usubiri uone may be utajua nini kinachoendelea by the way pole sana
 
Acha kupaka rangi upepo wewe...

Unamaanisha nini? Kama kuhusu mchepuko ni Kweli siwezi. Sijawahi na ninamuomba mungu aniendeleze hivyo . kwa maana najua how much it hurts nimeumizwa before kwa hiyo hiyo michepuko . Na niliachana na ex wangu kwa sababu ya hiyo hiyo michepuko . Kwa hiyo kama utaamini sawa kama hutaamini pia sawa. Siwezi kukulazimisha . Asante.
 
Hapao kwenye wino kuna error, lakini sio mbaya najua yote ni stress tu kasababisha huyo kijana mpole, lakini si unajua wanasema kimya kingi kina mshindo, kaa usubiri uone may be utajua nini kinachoendelea by the way pole sana

Ahhaaaa umegundua eehee, Nashukuru kwa kuelewa mdear. Yaani Niko so stress nimemiss Kweli sauti yake honestly .
 
Maana yake ushaachwa...

Unamaanisha nini? Kama kuhusu mchepuko ni Kweli siwezi. Sijawahi na ninamuomba mungu aniendeleze hivyo . kwa maana najua how much it hurts nimeumizwa before kwa hiyo hiyo michepuko . Na niliachana na ex wangu kwa sababu ya hiyo hiyo michepuko . Kwa hiyo kama utaamini sawa kama hutaamini pia sawa. Siwezi kukulazimisha . Asante.
 
Maana yake ushaachwa...

Samahani kwa kukushutumu , nisamehe sana. Asante kwa kunitafsiria , maana ya ule ujumbe wako . Sasa nifanyaje kama keshaniacha? Si aniambie basi ili nielewe . Hapa ndio huwa nashangaa sana kuhusu sisi binadamu yaani hata sijui tukoje . Nashukuru sana Asante .
 
Mmh hii scenario mbona kama naifahamu vile! Ungeweka tu nchi ningepata uhakika!

Anyway, POLE SANA! Umemiss sauti yake, lakini huna jinsi. Fanya shughuli zako, akijisikia atarudi, utajua kilichomsibu!
 
Mmh hii scenario mbona kama naifahamu vile! Ungeweka tu nchi ningepata uhakika!

Anyway, POLE SANA! Umemiss sauti yake, lakini huna jinsi. Fanya shughuli zako, akijisikia atarudi, utajua kilichomsibu!

Ni wewe nini ? Weka jina lako, na acha kuchezea maisha na moyo ya watu .
 
Pole sana kwa maumivu...natamani nikupe nguvu ya kumpotezea maana mtu kama huyo hana nia na wewe..atakuja kukuzingua zaidi..
 
Jina langu hilo hapo juu!

Wala usihofu, huo muda wa kuchezea maisha ya watu, badala ya kuyahangaikia yangu yasikimbie, nautoa wapi!

Ni wewe nini ? Weka jina lako, na acha kuchezea maisha na moyo ya watu .
 
mapenzi ni mtihani mkubwa sana, pole dada angu uyo jamaa hana mapenzi na wewe, endelea na mambo mengine.
 
loveissweet

pole sana, mpaka hapo ushapata jibu kuwa uyo hana nia njema na wewe, angalia upande mwingine, haya mapenzi ya kukutana kwenye mitandao ni shida tupu.
 
Last edited by a moderator:
Badili jina, like: loveissour inaweza kukupunguzia mawazo mpendwa!!
 
Back
Top Bottom