Nimshtaki nani?

Nimshtaki nani?

kabiriga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
1,163
Reaction score
1,214
Kati ya mambo yanayo nikela katika makampuni ya simu ni kuruhusu sisi watumiaji wa simu za mkononi kupokea msg za matanggazo mbali mbali ata yasiyo tuhusu.
Kati ya matangazo ambayo ni kero kubwa kwangu nadhani na kwa watumiaji wa simu za mkononi wengine ni matangazo ya hizi kampuni zinazo endesha michezo ya kubashiri.Unakuta kwa siku unapokea msg nyingi wakati wewe sio mhusika kwa maana sio mpenzi wa michezo ya kubashiri.

Kutokana na usumbufu huo ninaoupata unaotokana na matanggazo nisiyo yahitaji ndipo nikapata wazo la kuwashitaki hao wanaonitumia msg nisizo zihitaji ili ili kuondoa hii kero ya kila siku na kutoa funzo ili kama watuma msg za namna hiyo wahakikishe wanatuma kwa wahusika tu na sio kila mtu bila ridhaa yake. Wajuzi wa sheria za mtandao aomba kujua ni nani wa kushitakiwa kati ya kampuni ya simu husika na kampuni za michezo ya kubashiri.
 
Back
Top Bottom