Nimshauri Nini Rais wangu??

Nimshauri Nini Rais wangu??

Mbogela

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2008
Posts
1,384
Reaction score
260


Kutokana na kasi ya Magufulication inavyozidi kupamba moto nimejikuta nikianza kupata wasi wasi na hofu ndani mwangu ambayo sijajua inatokana na nini.


Kazi ya Magufuli ni nzuri na inatia matumaini kwa watanzania kwa kuleta mapinduzi, mabadiliko au mageuzi katika watendaji wa sekta ya umma. bado hatujaona mabadiliko ya kisera.


Lakini kwenye suala la mabadiliko ya kiutendaji tumeona kuna watu ambao lazima wachukuliwe hatua, hatua za kinidhamu na wengine wanapaswa kuchukuliwa hata hatua za kijinai.


Shida yangu ni kuwa ili Rais awe effecient katika hatua anazochukua anahitaji kutengeneza supportive structures, au tuite functional machines zitakazomsaidia ku-push hii ajenda yake ya mabadiliko ya kiutendaji kwa watumishi wa umma na wadau wengine.


Katika taarifa ya habari ya upotevu wa Macontainer zaidi ya 2300 unaweza kuona kutakuw ana mlolongo mkubwa sana wa wahusika. Kwa maana hiyo hawa watu wanahitaji Kukamatwa na Polisi, alafu kesi yao ipelelezwe na Polisi wakishirikiana na TAKUKURU na watu wa Usalama wa Taifa, baada ya upelelezi na ukusanyaji wa ushahidi na vielelezo faili zao zipelekwe kwa mwendesha mashtaka (DPP) ambaye kwa kushirikiana na mwanasheria wa serikali wata-proscute.


Kesi za hawa watu zitasikilizwa Mahakamani, mahakama gani?? Kisutu?? Mahakama Kuu?? au watakaa ndani wakisubiri kuanzishwa kwa mahakama maalum ya mafisadi???


Sasa Shida yangu ninaona vita vimeanza wakati bado hizi structure zetu ambazo zinapaswa kumsaidia Rais hazijakaa sawa. Nina wasi wasi kuwa hawa jamaa sijui wa PCCCB, Mahakama, Polisi na waplelezi, Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali na Mwendesha Mashtaka hawajajiandaa kukabiliana na uwingi na ukubwa wa kesi hizi zinazoangukia kwenye aidha uhujumu wa uchumi (Sheria ya kushughurikia hili ipo) au Ufisadi (Sijui kama kuna sheria juu ya hili) lakini tunawez apia kuwaona watuhumiwa sawa tu na watuhumiwa wa makosa ya ugaidi (Sheria ipo ila tutapoteza mwaka kubishana maana ya neno Ugaidi)


Nilikuwa ninadhani Rais Mh. Dr. John Pombe Magufuli afanye kama kuwapa somo hawa watendaji wakuu wa hizi taasisi zinazopaswa kumsaidia. Awaambie how serious he is, hawa jamaa wasije wakadhani business as usual maana nao wakishasikia kesi kama hizi wanajua hapa ndio pa kutokea, wanajua ndio muda wao wa kupiga bingo. Utasikia jamaa aliyesaidia kutorosha macontainer 360 kesho kashinda kesi, mara yule wa macontainer 2300 na yeye katoroka mikononi mwa polisi, au PCCB wanalalamika kuwa wameshindwa kumpeleka mahakamni sijui nani wamepoteza vielelezo. Hatutapenda kusikia habari kama hizi.


Mpaka sasa ni wizara moja tu, wizara ya Uchukuzi hapo hajafika wizara ya Maliasili na Utalii, Hajaingia kwenye milango ya wizara ya Nishati na madini, ninaamini kabisa presida na PM wakizitembelea wizara hizi mara kadhaa wakaweka mambo sawa tutakuwa na makesi mengi sana na watuhumiwa lukuki wa kujibu Tuhuma zao. Sasa kama Vyombo vya dola vya kumsaidia rais vitakuwa bado havijakaa sawa, watendaji wake wapo wapo tu Tutaweza kweli kushinda vita hii??


Nilikuwa nafikiri Rais usafishaji wa bandari na sehemu zingine zilizochafuka uende sambamba na usafishaji wa hivi vyombo vya dola.
 
ungejiuliza taarifa hizi wamezipata wapi?:maana si umekiri hamna vyombo vya dola vya kuaminika.
 
Namshauri kuwa usanii hausaidii na kama HAPA KAZI TU kwa nini hasianze na nyumba za serikali 258billion kakuja kibindoni.shika MAPAPA SIO VIDAGAA..


swissme
 


Wasivunje TANESCO it does not make sense at all shirika tayari lina assets zake za uzalishaji ata kama wanataka kubaki na shughuli ya ku manage the national grid ni bora wakavunja hiyo sehemu ya usambazi ikaitwa jina lingine TANESCO ibaki kama sehemu ya uzalishaji ikiwa bado chini ya serikari regardless of other private organization watakao changia pia kwenye national grid.

Yaani kuzigawa assets za TANESCO (ata huyo katibu kusema hilo neno anaona aibu kwenye video) ni ufisadi tu and it does not make sense at all kwanini watu wengine waje waweze TANESCO ishindwe kwa mitambo hiyo hiyo ata kama serikari ina lengo ya kuona kuna shirika linalo control national grid; this is absurd.

Kama tuna akili timamu lazima tujiulize mbona ni sector inayovutia wawekezaji wengi sana wakigeni halafu sisi tunataka kugawa asset za shirika zilizopo tayari ukizingatia kuna gesi ya serikari pia ambayo inaweza patikana na nafuu na kuongeza faida za shirika na mapato ya serikari kwa muda mrefu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom