Mie mwanaume hanipigi aisee kama hunitaki si uachane na mimi kwani lazima kuishi na wewe eti UNIPIGE?? Kwanza anaanzaje kunyoosha hicho kimkono chake?? Ashindwe na alegee
Tatizo kila akidundwa ananihadithi afu nasikia hasira mana hataki kuondoka..angekuwa hasemi sawa..ndugu zake wote wanajua ila wakitaka kumvamia mwanaume binti anakataa oooh mwacheni jamani..alishaambiwa na ndugu zake kama vipi tutakupangishia nyumba uhame na mwanao ye hataki afu akipigwa anahadithi..inaniudhi sana
Nishasema mwanaume hagusi mwili wangu kwa kichapo na huo ndio msimamo wangu. Kama kuna wanaopigwa ni wao mimi never never!!!
Eti anipige ha kisa nini??? Huko huko na kupiga wanawake mimi noooooooooooooooooooooooooooooo
Huyo dada alianza kupigwa hata kabla ya ndoa, lakini akakubali kuolewa na vipigo vyake! Mwache mwenzio na ndoa yake!! Ningekuwa mimi ningemwambia asinisimulie tena, maana hakuna maana ya kusimulia!
Maneno mazito hayo KH. Nakuunga mkono kabisa. Yanini mtu akusimulie vipigo/mateso yake ndani ya ndoa kama huna msaada wowote kwake maana kila unalomshauri analipiga chini.